Navigate / search

Mambo Mawili Unayohitaji Ili kufanikiwa Kabla Ya Kupata Pesa

Sina pesa hivyo hakuna kitu ambacho ninaweza kukifanya.Hiki ndio kisingizio cha watu wengis ana inapofikia suala la kuanza kuishi malengo waliyojiwekea na kuchukua hatua wanazopaswa kuzichukua katika maisha yao.Inawezekana hata wewe ni mmoja wa wale ambao huwa kila wakati kisingizio chao kikubwa ni kukosa pesa,na kwa sababu hiyo wamejikuta hawajaanza kuchukua hatua hadi leo.Ingawa pesa ni muhimu sana ,ila ni vyema kujua kuwa kabla haujapata pesa kuna mambo kadhaa ambayo utayahitaji katika maisha yako ili kujihakikishia mafanikio ambayo unayatafauta.

Jambo la kwanza ambalo unahitaji ni kujiamini kwamba unaweza kufanikiwa.Ni vyema kujua kuwa kujiamini kwako ni muhimu sana kwa ajili ya mafanikio yako.Kwa ufupi ni kuwa hauwezi kufanikiwa zaidi ya unavyojiamini.Kuna watu wengi sana wameshindwa kupiga hatua kwendea mbele zaidi ya pale walipo kwa sababu wameshidnwa kujiamini.Mara nyingi hali ya watu kutokujiamini nimetokana na mambo mbalimbali ikiwemo historia za maisha yao,maneno ya kukatishwa tama ambayo walishawahi kuambiwa huko nyuma n.k

Wakati mwingine hali ya kukosa kujiamini inatokana na historia ya kufeli katika jambo fulani ambalo mtu alishawahi kujaribu huko nyuma.Kuna watu wengi sana ambao walishawahi kujaribu mambo kadhaa lakini wakashindwa.Pengine aliwahi kufanya biashara ikafeli,ama aliwahi kufanya mtihani akafeli.Hali hii huwatengenezea watu hali ya kutokujiamini katika maisha yao na huwafanya kutoweza kujiamini tena.Mara nyingi unapozungumzia uwezo wa watu kufanikiwa katika maisha kuana watu wengi sana ambao hujion kuwa wao hawawezi kufanikiwa kabisa,na hii hutokana na mambo ambayo wameyapitia hapo kabla katika maisha yao.Leo ni muhimu sana kujichunguza kama hali ya yale uliyoyapitia huko nyuma kwenye maisha yake imekuwa sababu ya wewe kutokujiamini kuwa uanweza kufanikiwa.Je,unajiamini kuwa uanweza kufanikiwa?

Jambo la pili unalolihitaji kabla hata huajapata pesa ni kuwa na wazo ambalo ni sahihi la kulifanya.Hata kama ukiwa na pesa nyingi kiasi gani,kama hauna wazo muafaka linaloweza kukufanikisha basi itakuwa ni kazi bure katika maisha yako.Kuna watu wengi sana huwa wanadhani hawafanikiwi kwa sababu hawana pesa lakini ukijaribu kuwauliza una wazo gani unalotaka kufanyia kazi basi wengi unakuta hawana wazo linaloeleweka kuhusiana na maisha yao.

Leo ningependa nikushauri upate muda wa kutafakari kwa undani kuhusu wazo ambalo unalo katika maisha yako.Je,wazo lako linaweza kufanikiwa kama ukipata pesa unayotafuta?Kama unataka kweli kufanikiwa basi ni lazima utumie muda wa kutosha kulichambuwa wazo lako kwa kina-Hebu jiulize:Changamoto zitakazokabili wazo hili ni zipi?Nitazitatuaje?Nina maarifa ya kutosha kulitekeleza?Hivi wazo hili lina utofauti gani na wazo kama hili la mtu mwingine?

Kuna watu wengi sana ambao huwa wana mawazo ya kuiga toka kwa wengine.Siku zote kumbuka kuwa kama mtu mwingine ametekeleza wazo fulani na akafanikiwa,hii haimaanishi kuwa na wewe ukilitekeleza wazo kama hilo basi utafanikiwa pia.Sifa ya kwanza ya wazo linalofanikiwa ni kuwa lazima liwe linatokana na hamasa yako ya ndani na sio kuiga tu kile wanachofanya wengine.Leo jiulize-Wazo ambalo unasema uanlo ni la kwako?

See You At The Top

@JoelNanauka

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website