Navigate / search

Mambo Mawili Muhimu Ya Kuyajua Kama Unataka Kufanikiwa

habits-of-successful-people

Katika kufuatilia maisha ya kila aliyefanikiwa siku zote nimekutana na mikasa ambayo walishwahi kukutana nayo ya kufeli,kukatisha tamaa ama kuonyesha kuwa kile walichokuwa wanakiamini siku zote hakitaweza tena kutokea katika maisha yao.Hata hivyo tofauti yao na wale wanaofeli ni kuwa,watu wa namna hii siku zote walikataa kabisa kukaa chini baada ya kuanguka au baada ya kushindwa kufikia malengo yao.

Ningependa nikukumbushe maneno ya Winston Churchill aliyewahi kusema, “Success is stumbling from failure to failure with no loss of enthusiasm.” Akimanisha mafanikio ni kuvuka kutoka kushindwa hadi kushindwa bila kupoteza hamasa ya mafanikio unayoyatafuta.Siku zote katika maisha yako kumbuka kuwa kuna watu wa aina mbili:

Moja ni watu ambao wataambatana na wewe pale tu ambapo utakuwa unafanya mambo yanayolingana na yale ambayo wao wanafanya.Siku utakapoamua kuanza kufanya mambo makubwa zaidi kuliko ya kwao,wataanza kukuchukia na kukuona hufai kuendelea kuwa pamoja nao.Mara nyingi watu hupenda muendelee kufanana kwa kiwango cha mafanikio,mara utakapojaribu kuwa zaidi yao basi hapo utashangaa wataanza kutengeneza uadui,usishtuke.Uwe tayari kupoteza marafiki wa namna hii.

Mbili ni wale ambao siku zote wataambatana na wewe pale tu watakapoona unakaribia kufanikiwa ama umeanza kufanikiwa.Kuna watu hawatakuwa tayari kuamini ndoto na mawazo yako utakapokuwa unaanza kuyaishi ama utakapoanza kuwaambia.Lakini watu haohao siku zote watakuwa wa kwanza kujibaraguza na kumwambia kila mtu kuwa wao ndio walikuwa sehemu kubwa ya kukusaidia kufanikiwa kufika hapo ulipofika.Watu wa namna hii hutawaona wakati mambo yako ni magumu,huwa wanatokea pale tu ambapo mambo yako yanaanza kunyooka.Imeshawahi kukutokea hii?

Baada ya kutambua aina hizi mbili muhimu za watu katika maisha yako,kuna mambo mawili muhimu unayotakiwa kuyafanya kila siku katika maisha yako kama kweli unataka kufanikiwa kwa kiwango cha juu:

Kwanza ni kuamua kuwa unao wajibu wa 100% kubadilisha maisha yako na sio wajibu wa mtu mwingine yeyote yule.Umaskini na kufeli huanza pale mtu anapoamini kuwa kuna mtu yuko mahali ana wajibu wa kumsaidia.Hii ndio hupelekea watu kuanza kuwalaumu wazazi,kulaumu serikali,marafiki zao hata mabosi wao.Kuanzia leo tambua kuwa wajibu wa kufanikiwa kwako ni wako mwenyewe,fanya maamuzi na chukua hatua bila kusita.Watu wanaongojea kupewa msaada na watu wengine katika maisha yao huwa hawafiki mbali.Je wewe ni mmoja wa watu ambao hulaumu wengine wanapofeli?Badilika kuanzia leo.

Pili ni lazima uwe na mpango mahususi wa kubasilisha maisha yako.Mafanikio huwa hayaji kwa bahati hata siku moja,hutokana na mipango maalumu iliyoainishwa ya kukusaidia kutoka hapo ulipo kwenda kule unakotaka.Kama hadi wakati huu unaposoma andiko hili hauna mpango maalumu wa namna ya kutoka kiwango ulichopo sasa kwenda kwenye kiwango uanchokitamani basi ujue uko kwenye kundi la watu watakaofeli.Ni muhimu uwe na mpango huo tena uuweke kwenye maandishi-Weka muda(mfano mwaka/mwezi/wiki) na uonyeshe utafanya nini katika muda huo ili kuelekea katika kilele cha ndoto yako.kila siku uanpoamka unatakiwa uongozwe na ramani ya maisha yako ambayo ndio mpango wako.Kama huwezi kusema baada ya miaka mitano utakuwa wapi,unafanya nini,unaingiza pesa kiasi gani n.k basi ujue hauna mpango thabiti na huo ndio mwanzo wa kutokufanikiwa.
Endelea kutembelea www.JoelNanauka.Com kujifunza Zaidi.

Ndoto Yako Inawezekana.

See You At The Top.

Comments

Anthony Twipa
Reply

A nice msg

Leave a comment

name*

email* (not published)

website