Navigate / search

Mambo 5 Ya Kuachanayo Ili ufanikiwe 2017

 

Ninaamini kuwa huu utakuwa mwaka mzuri sana katika maisha yako na utafanikiwa katika mambo mengi ambayo unakusudia kuyafanya kama utazingatia mambo ya msingi ambayo utajifunza leo.Mara nyingi mwaka unapoanza kila mtu huwa anakuwa na hamasa ya kufanya jambo kubwa katika maisha yake na watu huwa na orodha kubwa na nzuri ya mambo gani ambayo wanakusudia kuyafanya aktika mwaka.Kila mtu ifikapo januarya anaona kuna uwezekano mkubwa wa kufanikiwa na kutimiza malengo aliyonayo katika maisha yake.Ili cha kushangaza ni kuwa baaa ya miezi michache watu hawa hujikuta kuwa hawana ile hamasa tena ya kuendelea mbele kama ambavyo walianza hapo mwanzoni.Na hii husababisha watu wengi sana kukata tamaa mapema kabla hata hawajafanikiwa kutimiza lengo moja la mwaka.

Inawezana kwa sasa na wewe umeshaweka mipango yako tayari ya namna ambavyo unataka kufanikiwa katika mwaka huu na una hamasa ya hali ya juu.Hata hivyo kuna mambo ambayo hautaweza kufanikiwa hata kidogo kama haujarekebisha baadhi ya vitu kwenye maisha yako.Katika kufuatilia watu waliofanikiwa na kufundisha watu kuhusu mafanikio,nimegundua mambo matano (5) ambayo kila anayetaka kufanikiwa ni lazima aamue kuachana nayo ili aoongeze uwezekano wa kufikia malengo makubwa zaidi.Hii ni kwa sababu kama utaendelea kuishi kama mwaka uliopita ukiwa na tabia zilezile basi utajikuta unapata matokeo yaleyale na hakutakuwa na mabadiliko yoyote yale katika maisha yako.

Jambo la kwanza ni kuachana na maisha yasiyo na mwelekeo.Kumbuka sikuzote kuwa mwelekeo ni muhimu kuliko kasi yako.Watu wengi sana wanaonekana wako kasi na maisha yao ila hawana mwelekeo.Ni lazima uamue kabisa mwaka huu unapoanza kuwa unataka jambo gani kwa umahsusi wake.Usianze mwaka bila mwelekeo kuhusu kazi yako,biashara yako,uwekezaji,masomo n.k.Jitahidi kutengeneza ramani ya maisha yako kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa kumi na mbili,kwa kila jambo liwekee mkakati maalumu wa namna ya kulifanikisha na kila siku ujue unataka kufanikiwa kwenye nini.Kwa mwaka huu,achana na ile tabia ya kujaribu kuanza kufanya kitu kipya kila baada ya  muda mfupi na mwisho wa siku unajikuta kuwa hakuna kitu cha maana ambacho umefanikiwa kukifanya mwisho wa mwaka unapofika.Jiulize tena leo-Mwelekeo wa maisha yako kwa mwaka huu ni upi?

Pili,achana na tabia ya kupoteza muda katika ratiba zako za kila siku.Kati ya rasilimali muhimu sana katika maisha yako ni muda-Na jinsi unavyotumnia muda wako basi utajulisha kama utapiga hatua ama la.Muda ukishapotea hauwezi kurudi tena.Usikubali kuwa mtu ambaye unapoteza muda wako kwa mambo ambayo siyo ya msingi kwenye maisha yako,amua kwa mwaka 2017 kuwa utakuwa mtu unayetunza muda wako vizuri.Usipoteze muda wako kwa kupiga stori zisizojenga,usipoteze muda wako kwa kuangalia movie kila wakati huku ukiwa hauna nafasi ya kujisomea vitabu vya kukusaidia kufatimiza ndoto zako,usipoteze muda wako kulala masaa kumi kwa siku wakati ungeweza kuutumia kwa kufanya shughuli za kujiongezea kipato-Mwaka huu achana na tabia kupoteza muda,amua kuwa mtu unayejali muda wako.Kila wakati jiulize-Hivi haya ni matumizi mazuri ya muda wangu?

Tatu,Achana na tabia ya kuendeshwa na misisimko ya maisha ambayo inakutoa Katika malengo yako.Ili ufanikiwe ni lazima uamue kuwa na mtazamo thabiti katika kile ambacho umeamua kukifanya,bila hivyo utakuwa ni mtu wa kutoka kwenye mstari kila wakati.Moja ya kitu ambacho huwa kinwaharibia watu wengi mwelekeo katika maisha yao ni ile hali ya kufanya mambo kwa msisimko bila kujipanga.Wakisikia kuna biashara/Kilimo fulani inalipa vizuri basi wanachukua hela zao zote na wanajiingiza kwenye hiyo biashara na wanajikuta wanapoteza kila kitu.Siku zote kumbuka kuwa hauna uwezo wa kufanya kila kitu na si kila mtu anaweza kufanikiwa katika kila kitu ambacho mwingine anafanya-Amua tangu mwanzo wa mwaka huu kuwa mtu ambaye hautaendeshwa na msisimko wa yale wengine wanayosema na badala yake utajikita katika kutekeleza malengo yako bila kutolewa nje.Misisimko itakuja mingi,ila amua kuachana nayon na jikite kwenye ulichoamua kukifanya.

Jambo la nne,ni kuachana na marafiki ambao wanarudisha nyuma maendeleo yako.Marafiki zako wana uwezo mkubwa wa kukufanya usonge mbele ama urudi nyuma.UKitafakari maisha yako ya mwaka jana utakuwa ni shahidi kuwa kuna marafiki zako wengi ambao wamekuwa sababu ya wewe kuingia katika matatizo ya kibiashara,kifedha,kimahusiano na wengi ambao walikushauri vibaya na ikakupelekea kujikuta katika wakati mgumu.Ni muhimu sana unapoanza mwaka huu uamue kufanya ukaguzi wa mtandao wako wa marafiki na ujiulize wale ambao wamekuwa msaada uendelee nao na wale ambao wamekuwa sio msaada uachane nao ama upunguze ukaribu nao.Huu pia nsdio wakati mzuri wa kujaribu kuangalia aina mpya ya marafiki ambao unatakiwa uwe nao katika maisha yako ili uweze kufikia malengo yako.Ni vigumu kupata matokeo makubwa zaidi yay ale uliyopata mwaka jana kama utaendelea na aina ileile ya marafiki bila kuwabadilisha kabisa.Katika mwaka huu amua kuachana na marafiki wanaokatisha tamaa,wanaokushauri vibaya na ambao wanakuingiza katika matatizo.

Jambo la tano ni kuacha kuishi bila ya bajeti.Kati ya sababu zinazoweza kukuingiza katika matatizo ya kifedha kwenye maisha yako ni hali ya kuishi bila kuwa na bajeti maalumu ya kutumia pesa zako.Hii ndio husababisha watu wengi waingie kwenye madeni na huwafanya kuishi juu ya uwezo wao wa kile wanachoingiza.Kaa chini na upange bajeti yako ya kila mwezi jinsi utakavyoingiza na vile utakavyotumia.Mwaka huu jitahidi sana usiishi juu ya kile unachoingiza kwa mwezi.Ukiweka bajeti yako na ukagundua kuwa matumizi yamekuwa makubwa kuliko kipato chako basi angalia namna unavyoweza kupunguza gharama za matumizi yako ili kwa namna yoyote ile usijiingize katika madeni yasiyo ya ulazima kwenye maisha yako.

Kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO kimechambua mbinu mbalimbali ambazo watu waliofanikiwa wamekuwa wanazitumia ili kufikia kilele cha mafanikio.Unaweza kukipata katika mkoa wowote ulipo,wasiliana nasi kupitia 0655 720 197 na kwa walioko Dar es Salaam unaweza kukipata katika maduka ya vitabu ama ukaletewa pale ulipo kwa bei ileile kupitia namba 0762 224 282.

Nakutakia Mwaka wa Mafanikio.

See You At The Top

@Joel Nanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website