Navigate / search

Mambo 4 unayotakiwa Kuyafanya Kuhusu Kila Rafiki Uliyenaye

DSC01968

Katika mahusiano yako na watu wengine kila wakati utahitajika kufanya tathmini kujua kama uko katika njia sahihi ama la kisha kuchukua hatua stahiki.Kwa ufupi unatakiwa ufanye kitu kinaitwa “Friendship audit” na “Friendship adjustment” yaani ukaguzi wa urafiki ulionao na watu wengine na pia kufanya marekebisho.Hili ni la muhimu kwa kuwa,kila anayeambatana na wewe kwa namna moja ama nyingine anaathiri maisha yako aidha kwa njia nzuri ama mbaya.Hii ndio maana kuna msemo unasema,nionyeshe rafiki zao name nitakuambia wewe ni mtu wa namna gani.

Kitaalamu,unachotakiwa kufanya kwanza ni kuorodhesha mambo ambayo kwako ni ya muhimu na yanaongoza maisha yako(Values) mfano:Uadilifu,bidii,Ujasiri,Haki n.k kisha unaorodhesha mambo ambayo yanachangia katika mwelekeo wa ndoto yako mfano:kupenda kujifunza,kuamini katika malengo makubwa n.k.Baada ya kuamaliza zoezi hili unatakiwa kuorodhesha rafiki mmoja mmoja na kuangalia ni kwa kiwango gani anakidhi vigezo hivyo ulivyojiwekewa.Matokeo ya zoezi hili yatakupelekea kufanya kati/yote ya mambo haya manne:

1) Kuanzisha urafiki upya(New association)

Hii inamaanisha unaweza kujikuta kuwa watu wote ambao wamekuzunguka na unatumia nao muda hawakidhi kabisa vigezo ambavyo umejiwekea katika kufanikisha malengo yako.Ukishagundua hili unachotakiwa kufanya ni kuangalia namna ya kuanzisha mtandao mpya wa marafiki utakaofidia kile unachokosa katika mtandao wako wa sasa.Ama unaweza kujikuta kuna watu ulishawahi kuwa karibu nao sana huko nyuma ila sasa hamko karibu na unawahitaji,fufua mahusiano yako haya kwa faida yako mwenyewe.
Mfano:Kama wewe unataka kuwa mfanyabiashara wa bidhaa za solar lakini katika mtandao wako wamejaa wafanyabiashara wa mitumba,unahitaji mtandao mpya.

2)Kupanua urafiki na watu Fulani(expanding your relationship)

Ukifanya ukaguzi wa marafiki(friendship audit) unaweza kugundua kuwa huwa unatumia muda mwingi na wale ambao ulipaswa kutumia muda kidogo kwao na unatumia muda kidogo kwa wale uliopaswa kutumia muda mwingi kwao.Baada ya kugundua hilo,utalazimika kufanya juhudi za makusudi kuongeza muda unaotumia ka baadhi ya watu ambao watachangia kwa kiasi kikubwa katika kukusaidia kufikia ndoto yako.Hili lazima ulifanye kwa kukusudia na kujiwekea ratiba,haliwezi kutokea lenyewe tu.

3)Kupunguza uhusiano na baadhi ya watu(Limiting your relationship)

Ukaguzi wa marafiki utakupa picha kuwa kuna watu ambao umekuwa ukiwapa kipaumbele bila kuwa na ulazima wa kufanya hivyo.Kwa kuligundua hilo utalazimika kupunguza muda unaotumia pamoja nao,aidha kwa kupunguza muda wa kukutana uso kwa uso ama hata kwa kuongea ama kuchart kwenye simu au mtandaoni.

4)Kusitisha uhusiano na baadhi ya watu(Discarding your relationship)

UKweli ni kuwa kila uhusiano unahitaji uwekezaji wa muda,nguvu,hisia na pesa.Ukifanya ukaguzi wa marafiki utagundua kuwa kuna baadhi ya marafiki ulionao wanamaliza rasilimali pasipo na ulazima.Kumbuka kuwa kama unataka kufanikiwa huwezi kuwa rafiki wa kila mtu kwa kila wakati,lazima uchague na uwe na mipaka.Ukigundua kuna aina ya uhusiano ambao unakurudisha nyuma,usichelewe:Mara moja sitisha uwekezaji wako katika uhusiano huo.

Kumbuka,wewe ndio mwamuzi wa nani awe karibu nawe na nani awe mbali na wewe.Ila cha kujua ni kuwa,unao uwezo wa kuchagua marafiki lakini hauna uwezo wa kucontrol tabia wanazokuambukiza unapokuwa nao kila siku.
Kadri utakavyofanya zoezi hili mapema ndivyo utakavyopata faida Zaidi.Je,leo unaweza kufanya friendship audit?

See You at the Top

Leave a comment

name*

email* (not published)

website