Navigate / search

Mambo 3 Yaliyomsaidia Manny Khoshbin Kutoka Kulala Nje Hadi Kuwa Na Biashara Zake

 

Manny Khoshbin ni mmoja kati ya watu wengi sana ambao wameanzia chini kabisa katika masiha yao na leo wamefika hatua nzuri.Aliingia marekani akiwa na umri wa miaka 14 baada ya kukimbia kutoka katika nchi yake ya Irani ambako kulikuwa na machafuko makubwa sana.

Alipofika marekani alikuwa hawana pesa kabisa na alikuwa hana mahali pa kulala hiyvo iliwalazimu wawe wanalala kwenye gari kabla ya kupata msaada wa kupata makazi.Khoshbin alipata kazi ya kupanga bidhaa katika duka kubwa la Kmart ambako alikanza kulipwa kwa saa.Hata hivyo anasema moja ya kitua ambacho alikuwa anatakiwa kukabiliana nacho kila wakati ni manyanyaso kutoka kwa wateja ambao walikuwa ni wabaguzi kwa sababu ya kuona kwamba yeye si mmarekani kwa kuzaliwa,hata hivyo alijitahidi kuvumilia huku akifukuzia malengo aliyonayo kwenye maisha yake.

Anasema kila alipokuwa ananyanyaswa na wateja wabaguzi waliokuwa wanakuja katika duka ndivyo ambavyo alikuwa anazidi kupata hamasa ya kufanya kazi zaidi kwa bidii na kufukia malengo ambayo anayo kwenye maisha yake.Siku  moja alifanya maamuzi kuwa ni lazima afanye kazi kaw bidii ili siku moja aje kuwa na uhuru wa kifedha.Anasema kwa sababu alikuwa hata ana akaunti ya kupeleka fedha,aliamua kuwa kila wakati atakuwa anaweka fedha ambayo anaipata kwenye bahasha yake na baadaye mwisho wa mwaka aliamaua kuitumia kama ndio mtaji wake wa kwanza.Leo hii ana utajiri wa zaidi ya milioni 100 na shida zote zilizokuwa zinamkabili zimeshaisha.

Maisha yake yanatoa mafunzo kadhaa kwa kila ambaye anatafuta mafanikio kwenye maisha yake.Jambo la kwanza ni kuanza pale ulipo kwa kile ulichonacho na vile unavyoweza.Usikubali kuendelea kusubiria wakati kuna ambacho uanweza kufanya kwa sasa kwa kile ulichonacho.Ingawa alikuwa na ndoto kubwa sana za maisha yake,alikubali kujishughulisha na jambo dogo ambalo lingemsaidia kumsogeza kwenye hatua inayofuata ya maisha yake.Usikubali kuzuiwa kupiga hatua kufuata unachokiamini kwa sababu haujapata kikubwa unachotaka,anza na kidogo unachoweza kwa sasa.

Jambo la pili la kuliangalia hapa ni kuwa,hakuruhusu watu waliokuwa wanamdharau kwa kuwa sio mmarekani kumfanya akate tamaa,bali aliifanya kuwa ni motisha kwenye maisha yake na kuelekea kwenye ndoto yake kubwa.Kila kitu na kila mtu ambaye anakuambia ama kukuonyesha wewe si kitu ama hautasonga mbele,tumia hiyo kama motisha ya kukusaidia kusonga mbele zaidi na sio kukukatisha tamaa ya kusogea.

Jambo la tatu na la mwisho ni jinsi ambavyo aliweza kujiwekea nidhamu ya kuweka kidogokidogo hadi kufikia lengo alilokuwa nalo.Nawe usidharau kile kidogo ambacho unacho mkononi kwa sasa,unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa kwa kila kidogo ulichonacho uanweka kidogokidogo hadi kufikia kiwango kikubwa uanchokitaka.Kila kinachopita katika mikono yako ni mbegu unayotakiwa kuikuza ili izae na kuwa kubwa zaidi.Usidharau mshahara ulionao leo,usidharau faida unayopata leo,usidharau kidogo unachopata,tafuta namna ya kukitumia na kukizalisha ili kikusaidie baadaye kutimiza malengo yako.

See You At The Top

#TIMIZAMALENGOYAKO

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website