Navigate / search

Mambo 3 Ya Kuyafanya Kila Siku Asubuhi Ili Uwe Na Siku Ya Mafanikio

Jinsi ambavyo huwa unaianza asubuhi yako huwa inapelekea namna ambavyo utafanikiwa katika siku hiyo ama la.Kama wewe ni mtu ambaye unaianza siku yako vibaya basi uanweza kujikuta unaharibu kila hatua ambayo inafuata ndani ya siku hiyo.

Moja ya kitu cha muhimu sana ni kujua kwa ufasaha ni mambo gani unatakiwa kuanza nayo ili siku yako iwe na mafanikio makubwa.Kuna mambo matatu ambayo leo ningetaka uyazingatie unapoanza siku yako ili uifanye siku yako iwe ya mafanikio:

Jambo la kwanza kabisa ni lazima upate muda wa kutafakari kuhusu mipango na malengo yako ya maisha.Unaweza kutumia muda huu pia kusali na pia kutulia kwa dakika chache ili kupata picha halisi ya mwelekeo wa maisha yako.Ni lazima ujiulize na upate majibu kama uko kwenye mstari sahihi ama la.Ni lazima ujiulize kama uanfanya unayotaka ama ni maisha yanakuendesha tu,ni lazima ujiulize kama unaenda kufanya kitu ambacho unakipenda ama la,ni lazima ujiulize kama kuna tabia unatakiwa kuziacha ama la n.k tumia muda huu vizuri kutafakari kuhsuu maisha yako na upate majibu yanayotakiwa.

 

 

Muda huu wa kutafakari pia utautumia kupitia malengo ambayo umejiwekea kwenye kuyafanya  kwa siku hiyo.Yapitie moja moja na uhakikishe kuwa umeyapanga kwa mpangilio ambao unatakiwa.

Jambo la pili hakikisha unapata kitu cha kukutia hamasa ili kuanza siku hiyo.Inaweza kuwa kusikiliza kitu fulani ama kusoma makala fulani ambayo itakupa hamasa na maarifa mapya ya kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza.Kumbuka kuwa kila siku unahitjai kuwa na nguvu ya ziada kukabiliana na vikwazo vitakavyoibuka.Moja ya kitu cha msingi sana kwenye maisha yako ni kuhakikisha kuwa unaanza siku ukiwa umejaa nguvu tele.Hii itawezekana tu kama utaamua kuanza siku yako kwa kusoma ama kusikiliza kitu ambacho kitakupa hamasa ya hali ya juu sana.

 

 

 

Jambo la tatu ni kuhakikisha kuwa unaanza moja kwa moja kufanya kitu ambacho kwako ni kipaumbele.Watu wengi sana huwa wanapoteza masaa ya kwanza ya siku yao kwa kufanya mambo yasiyo ya umuhimu na kusoma vitu ambavyo sio vya umuhimu.Ili wewe ufanikiwe kufanya mambo mengi kwa muda mfupi ni lazima uamue kuwa siku inapoanza,bila kuchelewa unaingia kwenye kufanya kile ambacho umekusudia.

 

 

 

Ukianza siku yako kwa kupoteza muda,basi utajikuta siku nzima unapoteza muda wako bila sababu za msingi na utaanza kuona kama hauna hamasa.Ukianza siku yako kwa kufanya yale uliyojipangia utaanza kupata hamasa na msukumo wa kufanya bila kuchelewa.Achana na kupiga stori,achana na kupoteza muda kwenye mtandao,anza ulichokiweka kuwa kipaumbele chako mara moja.Hakikisha inapofika nusu ya siku yako,unakuwa umemaliza mambo yote muhimu sana unayotakiwa kuyafanya kwa siku husika.

See You At The Top

@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website