Navigate / search

Mambo 3 ya Kukusaidia Kuvuka Vikwazo Vya Kufikia Ndoto Zako

nick-01

Siku ya Kwanza nilipomuona Nick Vujicic nilijifunza kuwa kinachofanya watu wasifanikiwe si kwa sababu hawana vile ambavyo wengine wanavyo ila ni kwa sababu hawajaweza kutumia vile walivyonavyo kwa kiwango cha juu.Akiwa hana mikono wala miguu,Nick anaishi maisha ya furaha na mafanikio kuliko watu wengi walioko duniani ambao wamekamilika kuwa na viungo vyote walivyonavyo.

Katika udhaifu wake huo,Nick ananishangaza sana kwani anatembea dunia nzima kuwatia watu moyo ili kufikia ndoto zao.Kiuhalisia ilikuwa anatakiwa yeye ndiye atiwe moyo na afarijiwe kutokana na hali yake lakini hali iko tofauti.Ukweli ni kuwa kinachowafanya wengi washindwe katika masiha ni ule mtazamo na tafsiri waliyonayo kutokana na changamoto zinazowakabili.

Kuna mambo 3 ya kuzingatia kutokana na maisha ya Nick:

1)Kuwa na Furaha Maishani ni Uamuzi wako.

Bila kujali hali na matatizo unayopitia,suala la kuamua kuwa na furaha ni uamuzi wako mwenyewe.Wanasaikolojia wanahusisha sana hali yako ya furaha na kiwango cha mafanikio yako.Kiufupi ni kuwa ,furaha hufanya akili yako iongeze ubunifu,unaongeza ufanisi wa kufanya mambo na huvutia watu wengi na fursa nyingi upande wako.Kama Nick anaweza kuwa mwenye furaha katika hali yake,je wewe unashindajwe kuwa na furaha.Usiisubiri furaha ije,jiambie nafsini mwako “bila kujali kinachoendelea katika maisha yangu leo nachagua kufurahi”

2)Ukiamini na Kuamua kufanya jambo unaweza

Kwa hali halisi ya Nick,sikuwahi kufikiri kuwa anaweza kutumia computer ama kuandika,ila nilishangazwa sana nilipoona video yake anaweza yote hayo lakini pia anaweza hata kuogelea(Ajabu).Kitu cha kutambua ni kuwa,ukiamua na kuamini unaweza kufanya kitu Fulani,inawezekana.Unataka kuwa mfanyabiashara,inawezekana.Unalenga kufanya kazi katika kampuni kubwa ya kimataifa,Inawezekana.Unalenga kujenga nyumba au kununua gari mwaka huu,Inawezekana,Unataka kufaulu vizuri masomo yako,Inawezekana.Bila kujali madhaifu yako,Imani yako ya kuwa inawezekana inatosha kukufanya uvuke vikwazo vyote.

3)Mafanikio yanatokana na Unavyojiona

Sehemu nyingi anazoenda Nick,huwa wanamuhurumia na wengine hata kulia kutokana na hali yake.Najiuliza,kuna watu wangapi kwa sababu hawana kiungo kimoja tu wamekata tamaa na wengine wanakaa barabarani tu kuomba msaada,hawaamini kama kuna maisha tena ya mafanikio.Najiuliza wangapi wameachwa kwenye ndoa zao na wamekata tamaa ya kuinuka tena,najiuliza ni wangapi wameumizwa na waliowapenda na kuwaamini na hawaoni tumaini tena.

Najiuliza ni wangapi wametafuta kazi kwa muda mrefu na wamekata tamaa tayari,hivi ni wangapi wanasoma Makala hii leo na wamejaribu kila biashara na kila wazo limefeli na wanaona haiwezekani tena,hivi ni wangapi wanafikiria kuwa kwa sababu waliwahi kufeli mitihani huko nyuma basi hawataweza kufaulu tena?

Nick anatufundisha kuwa;mafanikio yetu yanatokana na tunavyojiona na tunavyotafsiri yale yanayotokea maishani mwtu.
Usikate Tamaa kwa sababu ya Kile ushichonacho,tumia kidogo ulichomacho na utashangazwa na Matokleo yake.

Endelea kutembelea ukurasa wangu wa facebook (Joel Nanauka) Kujifunza Zaidi.

See You At Top.

Comments

jacqueline mwasha
Reply

Sitakata tamaa maishani mwangu,sitachoka kufanya yale ninayotaka kufanya au niliopanga kufanya kwenye maisha yangu,kwa jina la yesu lazima nifikie hatma ya ndoto zangu.
Bro asantee sana hujui ni jinsi gani mm nafaidika na mafundisho yk pastor.barikiwa sanaaaa.????

nanauka
Reply

Amen,Songa Mbele Bila Kuchoka wala Kukata Tamaa

Diana Kazinza
Reply

Ahsante sana kaka Joel.
Hili kwangu ni somo kubwa sana.
Am blessed.
Ubarikiwe sana.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website