Navigate / search

Mambo 3 Ya Kukusaidia Kushinda Dhahabu maishani

337DF77900000578-0-image-a-53_1461496953407

Akiwa amebakiza maili 23 kabla ya kumaliza katika mstari wa mwisho,Jemima Sumgong alianguka na akajigonga kichwa chake chini na akapata maumivu makalim sana.Umbali uliokuwa umebakia ulikuwa ni mdogo sana kuweza kuleta tofauti yoyote kwa wakati huo.Wenzake ilionekana kama wanaongeza nguvu Zaidi na kumuacha kwa umbali mkubwa Zaidi,lakini hata hivyo Jemima aliamua kuinuka huku akiugulia maumivu na akaendelea na mbio kuwafukuza wenzake waliotangulia.

Unajua kilchotokea?Mwisho wa mbio zile Jemima alifanikiwa kumaliza kwa muda wa masaa2 dakika 22 na sekunde 58 akimshinda bingwa mtetezi wa mwaka uliopita (2015) Tufa na akajichukulia medali ya dhahabu katika mashindano ya mbio ndefu ya London.

Kuna mambo makubwa matatu Jemima anatufundisha:
Moja ni kuwa haijalishi mara ngapi umeanguka chini/Umefeli ukielekea katika kutimiza ndoto yako;kitu cha muhimu ni kuwa unatakiwa uwe na nguvu za kuinuka tena na kuanza upya kila unapojikuta umeanguka chini.Kwa tafsiri rahisi kuanguka chini/kufeli mara moja haimaanishi ndio hauwezi kuendelea mbele tena bali inamaanisha ukiwa na nguvu za kuinuka bado una fursa ya kutimiza ndoto yako.Inawezekana umeshawahi kuanzisha biashara ikafilisika,ulishawahi kufeli shuleni kwako,ulishawahi kuwa na pesa nyingi sana na sasa hauna au unaugua sana na ni kama hakuna dalili ya kupona.Unatakiwa kujua kuwa unayo nafasi ya kuinuka na kuanza tena,usikubali kukata tamaa na kukosa matumaini ya kuendelea bado fursa unayo.

Pili ni kuwa aliamua kudharau maumivu aliyokuwa anayapata kwa sababu ya lengo kubwa alilokuwa nalo.Jemima anasema kuwa alikuwa anasikia maumivu makali sana kichwani baada ya kuanguka lakini ilibidi afanye uamuzi;aidha kuugulia maumivu ama kuendelea kukimbia ili atomize ndoto yake kupta medali ya dhahabu.Tunapoendelea kufuatilia ndoto zetu kuna nyakati tuatasikia maumivu makali sana pengine ya uchovu wa mwili kwa kufanya kazi kwa bidii,maumivu ya kukataliwa ama ya kudharauliwa.Jambo la msingi ni kutambua kuwa mafanikio huja baada ya sisi kuamua kuwa maumivu tunayoyasikia hayatatuzuia kufikia ndoto yetu.Bila kujali leo uko chini kwa kiwango gani,dhamiria kuwa hakuna aina yoyote ya maumivu itakayokusababisha kuacha kuendelea mbele.

Tatu Jemima aliendelea kushindana bila kujali wenzake wamemuacha umbali gani.Baada ya kuanguka,wenzake waliendelea kukimbia na waklimuacha mbali sana lakini hakukata tamaa na hatimaye alishinda.Inawezekana katika maisha yak oleo unajaribu kujilinganisha na watu mbalimbali uliomaliza nao shule,ulioanza nao kazi,marafiki zako n.kUkijaribu kutathmini uanona kama vile hakuna namna unawezxa kufanikiwa kama wao.Siri ni kuwa,usikate tamaa kwa kuangalia wako mbali kiasi gani,endelea kufanya jambo sahihi na kwa bidii na wewe utafikia kilele cha ndoto yakeo.Usikubali kukatishwa tamaa na mafanikio ya watu wengine bali uwe mtu unayetiwa hamasa na mafanikio ya watu wengine ili uweze kuyafikia na wewe.

Leo kwa mara nyinginep;kumbuka kuwa maisha yako ni kama mbio ndefu za marathoni,zinahitaji uvumilivu,zinahitaji kutokata tamaa na zinahitaji kuvumilia maumivu yatokanayo na magumu unayokutana nayo njiani.
Endelea Kutembelea www.JoelNanauka.Com Kujifunza Zaidi,na kama ujumbe huu umekuwa na manufaa zaidi,unaweza kushare na rafiki zako.Pia unayo fursa ya kujiunga na mtandao wa washindi ili kujifunza zaidi kupitia watsapp group bila gharama yoyote;Tuma neno “NDOTO YANGU”,Ikifuatiwa na jina lako kwenda namba 0655 720 197.

Ili kupata Makala za kila wiki za kujifunza jinsi ya kuifikia ndoto Yako,tafadhali nenda kwenye website yangu na chini upande wa kulia kwenye “weekly newsletter” andika email yako pale kisha itume.
Ndoto Yako Inawezekana,

See You At The Top.

Comments

David derick
Reply

masomo ni mazuri yanajenga

nanauka
Reply

Nashukuru kwa mrejesho David

amiri shillingi
Reply

Thanks bro, you are well done, plse join me on whatsap(0718700916) or weekly email to get more crucial alert from you.

nanauka
Reply

To join watsapp group send your full name and the word “ndoto Yangu” to 0655 720 197 and to receive weekly newsletters subscribe to the website below.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website