Navigate / search

Mambo 3 Ya Kujikumbusha Kila Siku Kama Unataka Kushinda Changamoto

Kila siku unakutana na watu na mazingira ambayo yatakuwa yanatishia sana mafanikio yako aktika kutimiza malengo uliyonayo kwenye maisha.Hii sio wewe tu peke yako,kila mtu ambaye anataka kufanikiwa katika  maisha huwa anakutana sana na hali hii.Kuna changamoto ambazo kila siku zitakuwa kama zinakuambia kuwa hauwezi tena kuendelea mbele hatua moja zaidi.Nimejifunza kuna mambo 3 ya kujikumbusha kila siku kama kweli unataka kubakia kwenye mstari:

Moja,ni lazima ujikumbushe kuwa una uwezo wa kufanikiwa katika kile unachofanya.Moja ya kitu ambacho watu na changamoto hufanya katika maisha yako ni kuanza kukufanya ujione kuwa hauwezi na kupoteza ujasiri ulionao kwenye maisha yako.Kila wakati ni lazima ujikumbushe kuwa hakuna mtu au hali inayoweza kukuzuia kufanikiwa katika kile uanchokitaka isipokuwa wewe mwenyewe.Usikubali hata siku moja kuamini kuwa kuna mtu ambaye ana uwezo na mamlaka ya kukuzuia kufanikiwa.

Jambo la pili la kujikumbusha ni kuwa kila ambaye alifanikiwa hakuzaliwa hivyo.Kila mtu aliyefika juu leo basi kuna siku alikuwa chini sana,kila aliye tajiri leo hakuanzia hapo,kuna wakati alikuwa chini sana.Hii inamaanisha kuwa hata wewe bila kujali leo uko katika kiwango gani cha maisha ama kile uanchokitafuta basi unaweza kutoka hapo ulipo na ukaenda kwenye kiwango cha juu zaidi katika maisha yako.

Usiubali kuamini kuwa kwa sababu ya hali yako yab leo basi hautaweza kufikia viwango vya juu sana,sio kweli.Siku zote usisahau kanuni ya “Cause and effect”-Kama ukifanya yale ambayo wengine wanafanya na wakawa vile walivyo basi na wewe pia unaweza kupata matokeo ambayo wengine wameyapata pia.Kuwa kwako chini leo haimaanishi siku zote utakuwa hivyohivyo.

Jambo la tatu la kujikumbusha ni kuwa maisha yako ni matokeo ya mawazo yako.Kuna kanuni inaitwa “The Law of Dominant Thought”.Hii inasema kuwa mawazo ambayo yanachukua nafasi kubwa kwenye maisha yako basi hujikuta ndio uankuwa uhalisia wa maisha yako.Hii inamaanisha kuwa usikubakuli hata dakika moja kuruhusu mawazo kushindwa na yanayokuambia hauwezi kwenye maisha yako.Kila wakati jitahidi kuwa mtu ambaye unawaza uankokwenda zaidi kuliko ulikotoka,kila wakati jitahidi kuwaza namna ya kutatua tatizo na sio kutafuta mtu wa kumlaumu.

Kumbuka kuwa hakuna namna unaweza ukawaza mawazo ya kushindwa halafu ikatokea uwe mshindi.Kila uanchowaza ndicho ambacho unakipata kwenye maisha yako.Kuanzia leo uwe makini na kile unachowaza kwenye maisha yako.Waza ushindi,waza utakavyotatua changamoto,waza utakavyosonga mbele n.k

Leo,jikumbushe mambo haya matatu na uyaishi kwa uafasaha.

See You At The Top

@JoelNanauka

 

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website