Navigate / search

Mambo 2 ya kuyajua ili Usikate Tamaa Maishani

bullying_alamy_2402756b

Katika hatua zetu za kuelekea katika kilele cha mafanikio yetu na kutimiza ndoto zetu huwa tunakutana na mambo mengi sana ya kukatisha tamaa(setbacks).Wakati mwingine kuna mambo ambayo yakitokea katika maisha yako ni kama vile yanaashiria huwezi tena kufanikiwa na kutimiza malengo yako uliyojiwekea.Kwa ufupi unaingiwa na hali ya KUKATA TAMAA kusiko kwa kawaida.

Ukiwa katika hali hii huwa unatamani uwe karibu na watu wanaokutia moyo na wanakufanya ujisikie kuhurumiwa kila wAkati(Sympathizers).Ingawa hali hii itakufanya ujisikie vizuri ukweli ni kuwa inakuharibu zaidi.Kadiri unavyochukua muda mrefu kujikung’uta mavumbi na kuamua kusonga mbele mara baada ya kukutana na hali ya kukatisha tamaa ndivyo utakavyochukua muda mrefu kufikia malengo yako.

Wale wanaotimiza malengo yao maishani huwa na fikra kubwa za aina mbili kuhusiana na mambo ya kukatisha tamaa yanapowatokea:

1.Maisha yangu huwa si matokeo ya yale yanayotokea(stimuli) bali ni matokeo ya ninavyochukulia yanayotokea(response).Katika stadi za maisha ya kila siku,inaonekana kuwa changamoto tunazopitia husababisha asilimia 10 tu ya vile tulivyo,asilimia 90 iliyobaki husababishawa na mwitikio/hatua tunazoamua kuchukua baada ya changamoto kutokea.Kama mtu akikuambia hauna thamani-Hilo ni tukio lakini je mwitikio wako utakuwaje?Mwingine atapuuzia atasema hayo ni maoni yake,mwingine ataumia na kujifungia chumbani na kuanza kulia na baada ya hapo hata mavazi yake yatakuwa yanaendana na mtu asiyejithamini.Hii ndio maana watu wawili wanaweza kupitia changamoto moja inayofanana lakini wakatapa matokeo tofauti.
Kuanzia leo amua kuwa mwitikio wako(response) uwe ni ule unaokupa nguvu Zaidi na sio kukudhoofisha.

2. Fikra ya pili ni kuwa sina mtu wa kumlaumu katika hili,NAWAJIBIKA.Watu ambao kila wanapopata changamoto kazi yao ni kuwalaumu watu wengine au mazingira huwa hawafiki mbali.Wengine watalaumu wazazi wao,wengine shule walizosoma,wengine mabosi wao kazini,wengine mishahara midogo n.k
Cha kushangaza ni kuwa watu wawili kutoka familia moja utakuta mmoja anafanikiwa mwingine anashindwa,watu wawili kutoka ofisi moja mmoja anapandishwa mshahara kila mwaka mwingine hapandishwi,watu wawili waliosoma darasa moja mmoja amekuwa mkurugenzi mwingine bado hana kazi.

Suala kubwa si kuendelea kulaumu au kulalamikam;Tambua kuwa wajibu wa kubadilisha maisha yako uko mikononi mwako.Jifunze wenzako walifanya nini wakafanikiwa nawe ujue utafanyaje ili ufanikiwe.
AMUA KUBADILISHA MWELEKEO WA MAISHA YAKO LEO.

Kumbuka,

Naamini Katika Ndoto Zako,
Naamini katika Uwezo Wako,
Naamini katika Hatima Yako,

Tukutane Kwenye Kilele cha Mafanikio Yako.

Comments

Sonelo
Reply

Thanks a lot Bro:Joel for that strong message!

Mike
Reply

Good message brother Joel

Leave a comment

name*

email* (not published)

website