Navigate / search

Mambo 2 Ya Kufanya Unapopitia Kipindi Kigumu Maishani

index

Gazeti la the daily mail la uingereza siku ya tarehe 10 Mei lilirpoti taarifa iliyovutia hisia za wengi ulimwenguni.katika toleo hilo lilieleza juu ya kisa cha mwananmke mmoja ambaye ana umri wa miaka 72 na mume wake ana umri wa miaka 79 wamefanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza kwa njia ya IVF baada ya kudumu katika ndoa kwa muda wa miaka 46.

Dr.Arnuragi Bishnoi aliyekuwa anamuhudumia mwanamke huyo kwa muda wa miaka miwil mfululizo katika clinic yake,alikiri kuwa ndoto ya mama huyo kupata mtoto ilikuwa kama ni kizungumkuti cha karne na aliendelea kumhudumia ili kumtia moyo tu ila hakuona kama kuna uwezekano wa Bi.Darijinderi Kaur kuweza kupata mtoto katika umri huo kama hakuweza kufanikiwa katika miaka yote hiyo iliyopita tangu alipokuwa kijana.Katika jamii anayotoka Bi.Kaur kutopata mtoto huchukuliwa kama ni laana toka kwa mwenyezi Mungu na hufanya jamii ikutenge.

Mara baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na miaka sabini alipohojiwa alieleza kuwa tangu miaka 46 iliyopita alipokuwa ameolewa aliamini kuwa siku moja atakuja kupata mtoto,hivyo hata baada ya taarifa za kidaktari kuthibitisha kuwa hawezi kupata ujauzito aliamua kuendelea kuamini kuwa kuna siku itawezekana.

Alieleza pia jinsi ambavyo ndugu na marafiki zake wa karibu walimkatisha tamaa na kumwambia ameshakuwa mzee aachane na tumaini la kupata mtoto.Yeye mwenyewe anasema alikataa kukubaliana nao na aliamini kuwa bado inawezekana kuja kupata mtoto katika uzee wake.

Ukiwa kwenye hali kama ya Bi rajun,ya kukaa muda mrefu ndoto yako haijatimia kuna mambo mawili unatakiwa kuyazingatia:

Moja,unatakiwa kuhakikisha kuwa katika mazingira yoyote yale uliyonayo,bado unaendelea kuwa na tumaini la kuifanikisha ndoto yako siku moja.Hakuna kosa kubwa unaloweza kulifanya kama kukubali kuacha kuiamini ndoto yako-Katikati ya mazingira magumu unatakiwa bado uendelee kuiamini na kuikiri ndoto yako.Watu wengi huwa wakipitia mambo magumu maishani mwao na yanayowakatisha tamaa,huwa wanakimbilia kusema,”mi naona niachane na ndoto hii”-HAPANA-Kila aliyefika kilele cha mafanikio aliwahi kupitia kipindi cha kuona mazingira yanayomzunguka si rafiki kumsaidia kufikia ndoto yake,ila kila mmoja aliamua kuendelea kuamini.je,unazungukwa na mazingira ya kukatisha tamaa…endelea kuamini tu utapata “mtoto” unayemtarajia.

Pili,unatakiwa uwe na uwezo wa kukabiliana na wakatisha tamaa.Tafiti huonyesha kuwa mtoto mdogo tangu anapozaliwa hadi anafikisha umri wa miaka 5 huwa anakuwa ameshaambiwa hapana mara 40,000 na ndio mara 5,000.kiufupi ni kuwa tunaishi ulimwengu ambao umejaa wakatisha tamaa na una uadimu wa watu wa kukupa nguvu na kukutia moyo.Watu wa namna hii utakutana nao.Bi Kaur alikuwa anakutana nao kila siku,ndugu zake,jirani zake na hata madaktari waliokuwa wanamuhudumia lakini aliamua kuamini tofauti.
Ukweli ni kuwa hauna uwezo wa kuchagua utakachoambiwa na kukisikia toka kwa watu wengine ila unao uwezo wa kuchagua na kuamua nini unataka kukiamini.Leo unapoanza siku yako,amua kuamini ndoto yako Zaidi kuliko maneno ya wanaokatisha tamaa-Amua kuamini kuwa bila kujali ugumu wa mazingira unaweza bado kuifanikisha ndoto na malengo yaliyo mbele yako.
Wengi walisema Bi Kaur ameshachelewa na amekuwa mzee,wengi watadhani kuwa umeshachelewa,umepoteza muda na haiwezekani tena-La hasha-Ukiamua kuamini INAWEZEKANA.Kama Bi Kaur angeamua kukata tamaa asingefanikiwa kupata mtoto,nawe pia uwe kama Bi Kaur.

Endelea Kutembelea www.JoelNanauka.Com ili kujifunza Zaidi,

Kumbuka kuwa Ndoto Yako Inawezekana.

See You At The Top.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website