Navigate / search

Mambo 2 Ya Kufanya Ili kuifanya Ndoto Yako Kuwa Kweli

528926652_154

Ili kuvuka kutoka hatua moja ya maisha yako na kuingia katika hatua nyingine kubwa katika maisha ,jambo moja wapo unalohitaji kuwa nalo ni utayari wa kujaribu kufanya.Nimeshawahi kukutana na watu wengi sana ambao kila siku wana mawazo mapya tena ni mawazo mazuri sana ila tatizo lao ni kuwa huwa hawachukui hatua kabisa.

Pengine hata wewe unaposoma ujumbe huu leo,una mawazo mengi sana tena makubwa na ambayo yakifanikiwa basi utabadilisha maisha yako kwa kiwango kikubwa sana.Jambo la Kujiuliza ni kwa nini watu wengi huwa hawafanikiwi katika kutekeleza mawazo yao.Kuna sababu 2 ambazo ukiweza kuzikabili basi wewe hautakuwa mmoja wa wanaoshindwa kuchukua hatua.

1) Kujipa majibu kabla hawajafanya

Nimekutana na watu wengi sana ambao mawazo yao yanahitaji msaada wa mtu,kampuni au taasisi Fulani ili waweze kufanikiwa.Cha ajabu nikiwauliza kwa nini hawajachukua hatua huwa wanasema “najua hatakubali nikimwambia”.Usikubali kujiambia Hapana kabla haujajaribu(Never Say No to Yourself before You have tried it”.

Ili ufanikiwe maishani,usiwe mtu wa kujipa jibu la hapana kabla haujajaribu.Utashangaa sana mambo mengi na watu wengi ambao unadhani watakuambia hapana siku ukija kuwashirikisha wanakubali ama wanakuunganisha mahali sahihi pa kukusaidia kufanikiwa.Leo,chukua hatua kuelekea katika kufanyia kazi mipango yako.Mpigie simu unayehitaji akusaidie,nenda ofisini kwake,andika email etc.Chukua hatua bila woga nawe utashangaa.Mambo mengine ni kama milango inayofunguka yenyewe(Automatic Doors),haifunguki hadi uisogelee.

2) Anza na Kidogo ulichonacho

Mara nyingi tunajifariji kuwa tutaanza kesho tutakapokuwa na vitu tunavyovihitaji.Ila cha kushangaza ni kuwa hata kesho ikifika tunajikuta tunasubiria kesho nyingine.Ukweli ni kuwa watu wanaosubiria kesho kukamilisha jambo Fulani huwa hawafanikiwi kwa sababu kesho huwa haifiki(Tommorow never comes).

Badala ya kusubiria kesho ifike utakapokuwa umekamilisha kila unachotaka nakushauri anza na hatua iliyo katika uwezo wako kwa leo wakati unaendelea kutumaini kuifikia hatua ambayo iko juu ya uwezo wako kwa kesho.

Kuna kanuni katika kuelekea mafanikio inaitwa”the law of compound effect”,kanuni ya mkusanyiko wa mambo mengi unayofanya ili kutimiza jambo Fulani.Mfano rahisi ni pale unapoamua kuvunja ukuta kwa kutumia nyundo yako.Unaweza ukapiga sana hadi nyundo ya mia mbili ndio ukuta ukaanguka.Lakini swali ni je?Ni nguvu ya nyundo ya mia mbili ndio iliyoangusha ukuta?

HAPANA.Ukuta umeanguka sio kwa nyundo moja ya mwisho bali kwa mkusanyiko wa kila pigo la nyundo ulilopiga hata kama ilikuwa hainyoshi dalili yoyote ile.

Katika safari ya Mafanikio ndio vivyo hivyo,kila uanchofanya kuelekea mwelekeo wa ndoto yako Kina Faida.Siku inakuja ambapo utashangaa ghafla”ukuta umeanguka”-Umepata kile unachotaka.

Leo,unapoanza siku yako orodhesha mambo ambayo unatakiwa kuyafanya katika kuchukua hatua ya kuelekea mafanikio yako.Je unaweza kushare na mimi mipango hiyo ili nikukumbushe itakapofika jioni?

Endelea Kutembelea ukurasa wangu wa facebook kujifunza zaidi na tuma neno “NDOTO YANGU” na jina lako kwenda 0655 720 197 ili uunganishwe katika mafunzo kwa njia ya Watsapp bila gharama yoyote.

Ndoto Yako Inawezekana,

See You At The Top.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website