Navigate / search

Mugabe Ashangiliwa AU:Yajue Mambo Muhimu Aliyoongea

4882206-3x2-940x627

Tarehe 29 January mwenyekiti wa Umoja wa Africa,Robert Mugabe alihutubia umoja katika kikao cha 26 cha AU  mbele ya hadhira ya viongozi wa Africa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Kimoon.Nilipoisikiliza hotuba yake hiyo(ilitarajiwa kutumia dakika 10 lakini alitumia takribani dakika 54) alizungumza mambo mbalimbali lakini katika hayo mengi,nimechagua machache kuyaandika hapa kwa ufupi sana:

1) Akizungumza mara tu baada ya Mwakilishi wa Palsetina alimkumbusha Ban Kimoon kuwa anakaribia kustaafu wakati hajapata ufumbuzi wa mgogoro wa Palestina.

2) Alimkumbusha Ban Kimoon kuwa nchi za Africa zimekuwa zikihimiza mabadiliko ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa na uwakilishi wa Afrika lakini kilio chao hakisikilizwi na kumkumbusha kuwa wataendelea kupigania haki hiyo.Na alikumbusha kuwa kama Umoja wa Mataifa unataka kuendelea ni lazima kuwe na haki sawa katika nguvu ya uwakilishi.

3) Alikumbusha kuwa Afrika katika mkutano wa Swaziland kuwa afrika iliazimia kuwa na wawakilishi wawili katika baraza la Usalama la Umoja wa Taifa ili kuwakilisha nchi 54 za Africa.

4) Alimshukuru Ban Kimoon kwa kuisaidia Africa katika mambo mbalimbali kama wakati wa kukabiliana na Ebola,Njaa na vita dhidi ya Ugaidi.Ila alionyesha kuwa aliweza kufanya hivyo kwa sababu hatokei bara la Amerika au la Ulaya.

5) Hotuba yake sawasawa na agenda ya mwaka ya AU ilijikita sana kwenye kuhimiza amani na mapatano akitaja changamoto chache za uongozi na siasa na pia kuzipongeza nchi zilizofanikiwa kubadilishana madaraka baada ya mgogoro kama vile Jamhuri ya Afrika ya Kati na Burkina Fasso pia.

6)Alielezea pia maamuzi yao ya kuweza kukamilisha bajeti yao kwa asilimia mia moja baada ya miaka mitano;ikiwemo 25% kwa ajili ya usalama na ulinzi na 75% kwa ajili ya miradi mbalimbali na kuwahimiza nchi ziendelee kulipa ada zao kwa wakati.

7)Alieleza pia kushuka kwa bei ya bidhaa nyingi zinazozalishwa Afrika imeleta changamoto katika kukabiliana na umaskini na kuongeza ukosefu wa ajira na kuhimiza kuwa uundwaji wa Viwanda inabidi uwe wa kasi ili kukabiliana na changamoto hizi.

8) Mahusiano kati ya Africa na China na India na China(AFRO-INDIA and AFRO-CHINA) ameilezea kuwa ni muhimu pia katika kuongeza wigo wa kibiashara.

9)Alikumbushia kuwa Saharawi inatakiwa iachwe huru kwani kuendelea kuifanya koloni la Moroco ni kuruhusu historia ya ukoloni kujirudia na pia Palestina ipewe uhuru wao.

10)Alieleza pa hata baada ya uhuru wazungu wameendelea kuitawala Afrika kupitia njia mbalimbali kama vile NGO’s zilizojazana Afrika.Alituhumu pia kuna wengine wanajihusisha na ugaidi,wengine ni wapelelezi ili kusaidia kuondoa baadhi ya Viongozi wa Afrika Madarakani.

(120129) -- ADDIS ABABA, Jan. 29, 2012 (Xinhua) -- Photo taken on Jan. 29, 2012 shows the site of the 18th African Union (AU) Summit in Addis Ababa, capital of Ethiopia. The 18th African Union (AU) summit opened on Sunday in the Ethiopian capital of Addis Ababa, as African leaders gathered with the theme of "Boosting Intra-African Trade." (Xinhua/Ding Haitao) (lr)

11)Alimtuhumu pia Barack Obama Kutokuwa na msaada kwa waafrika kwani wabdo watu weusi wameendelea kuuwawa marekani na pia maeneo mengi wanayoishi watu weusi bado elimu ni duni sana ukilinganisha na maeneo ya Wazungu.

12)Alioeleza pia jinsi Nigeria walivyolataa kulipia ada yao kutokana na misimamo tofauti juu ya Biafra na walipoamua kulipa deni lao lilikuwa kubwa sana kliasi cha dola/paundi miloni 7 na walitaka pesa hizo ziende kusaidia mafunzo ya wapigania uhuru wa Zimbabwe.Alieleza kwa ufupi pia juhudi ya Hashim Mbita na Tanzania katika kusaidia uhuru wa Zimbabwe.

13)Alimtaka Ban Ki moon kupeleka Umoja wa Mataifa ujumbe wa mwisho kuwa Waafrika wanataka usawa katika baraza la Usalama.

14)Alisema pia Makao makuu ya Umoja wa Mataifa yako mahali pasipo sahihi;alilinganisha uwingi wa watu china(1.3biioni),India(1.2Bil) na Bara la Afrika ni 1 Bilioni hivyo kama kwa kigezo cha uwingi Makao Makuu yanatakiwa yawe kati ya nchi hizo.

15)Alieleza Jakaya Kikwete kuwa alimueleza kuwa kuna mzungu wa ulaya alimwambia Chama cha mapinduzi kimekuwa madarakani kwa muda mrefu hivyo kinapaswa kuondoka,akasema waambie wakae kimya.

16)Alisisitiza kuhakikisha kuwa vijana wa Afrika wanafundishwa na kuambiwa kuhusu historia yao na wajivunie kuwa Waafrika.

17)Na alimtakia kila la kheri mwenyekiti mpya Idris Derby Rais wa CHAD na kumhakikishia kuwa ataendelea kumsaidia angali bado yuko hai hadi atakapoitwa kuungana na wengine na kuouundoka duniani.

18)Alimaliza kwa kushukuru kwa Lugha mbalimbali ikiwemo na kutumia neno la Kiswahili-“Ahsante Sana”

Endelea kutembelea www.JoelNanauka.Com

Leave a comment

name*

email* (not published)

website