Navigate / search

Makosa Manne ya Kiuongozi ya Kuyaepuka ili Ufanikiwe Zaidi!

r22

Mara nyingi inasemekana kwamba, makosa yanatupa nafasi kubwa ya kujifunza, Japokuwa sio vizuri kufanya makosa mwanzoni. Katika makala hii, tunaangalia makosa manne ya kiuongozi yanayofanywa sana na watu ambayo pindi utakapoyajua na kujifunza namna ya kuyaepuka, utakuwa umejiokoa mwenyewe katika matatizo mengi kama kiongozi.

1. Kushindwa kufafanua malengo

Watu wanapokosa malengo yanayoeleweka, huwa wanajichanganya sana. Hawawezi kufanikiwa kama hawaelewi ni kitu gani wanachokifanyia kazi au kazi yao inataka nini? Pia hawawezi kuweka vipaumbele vya kazi zao sawasawa. Hii inaonyesha kazi zao pia huwa zinaishia vibaya.

2. Kushindwa kutoa taarifa ya utendaji wako

Sara anafanya kazi vizuri kama muwakilishi wa mauzo, lakini anapojibu simu za wateja huwa anajibu katika namna isiyofaa. Bosi wake anajua hili lakini anasubiri wakati wa Sara kutoa taarifa ya utendaji wake ili amwambie ni wapo huwa anakosea. Kwa bahati mbaya kama hautamtaarifu Sara kwamba kuna uwezekano wa kutokea tatizo, ataendelea kuwakosea wateja. Kutokana na taarifa ya watendaji 1400 waliopigiwa kura na makampuni ya Ben Blanchard, kushindwa kutoa taarifa ya utendaji wako ni kosa kubwa ambalo viongozi wengi wanafanya. Unaposhindwa kutoa taarifa ya utendaji kwa watu wako unawazuia nafasi ya kuboresha utendaji wao.

3. Kudhani kwamba uko sawa!

Mtego mkubwa ambao huwa unawanasa viongozi, ni kudhani kwamba maamuzi yao au njia yao siku zote ni sahihi. “Mara nyingi, viongozi wanafikiri kwamba kwa sababu wana cheo au wadhifa juu ya wengine, basi wao ni wenye mawazo mazuri” alisema Mitchell Levy, mwandishi wa kitabu cha “Creating Thought Leaders Tweet” na mtendaji mkuu wa THiNKaha. “Wanadhani kwamba chochote wanachokisema kitafanyika kwasababu tu ni wao wamesema hivyo, hata kama wao wanafanya kinyume na hivyo”.

Kosa lingine ambalo huwa wanafanya ni kutokuwasikiliza watu wanaofanya nao kazi pamoja, timu. Ndugu Duggan Cooley, raisi na mtandaji mkuu wa Muungano wa njia za Pasco, alisema, viongozi wakati mwingine wanakazana kufanikisha kazi zao, wanasahau kusikiliza maoni ya watu. Hii inaweza kupelekea tatizo kubwa la mawasiliano ndani ya shirika. Kusuluhisha mambo kama haya, mwandishi wa vitabu, Levy, anasisitiza viongozi wawe wanarudi nyuma na kuruhusu wengine watafute, watatue na waanzishe mawazo, ushirikishwaji huu ufanyike kote ndani miongoni mwa wafanyakazi na nje kujumuhisha wadau na wateja. “Unahitaji kuunga mkono tabia hii, na kuruhusu watu unaofanya nao kazi pamoja, wajivunie ushiriki wao” alisema.

4. Kushindwa kugawa kazi/majukumu

Baadhi ya wasimamizi hawagawi majukumu, kwasababu wanahisi hakuna mtu mbali na wao ambaye anaweza kufanya kazi vizuri. Hii inaweza kuleta matatizo makubwa kadiri vikwazo vinapozidi kujitokeza na kadiri wanavyozidi kuchanganyikiwa na kuudhiwa. Kugawa kazi sio jambo rahisi na inaweza kuwa vigumu kuamini timu yako au mtu fulani katika timu yako anaweza akafanya hiyo kazi vizuri. Lakini mpaka utakapojua kugawa kazi, hautapata muda wa kulenga mambo makubwa ambayo viongozi na wasimamizi wengi wanalenga. Kubwa zaidi, utashindwa kuwaimarisha na kuwaendeleza watu. Viongozi wanatamani mambo yafanyike katika namna fulani wanaoijua wao wanadhani wao pekee ndio wanaoweza kufanya hivyo.

Pamoja na ratiba nzuri na mikakati mirefu, mabosi wasioweza kugawa kazi au majukumu watapotea haraka katika kuhakikisha kazi inafanyika. “Jambo la muhimu kama kiongozi, unaloweza kufanya ni kujijua mwenyewe na aina yako ya kipekee ya kiuongozi, inayokutaofautisha na wengine” raisi Cooley, aliliambia gazeti la BusinessNewsDaily.”Kama unazidiwa, hebu jiulize mwenyewe maswali, Je, ni kwa sababu umeshindwa kugawa majukumu? Je, umeshirikisha wengine? Je ulitakiwa uwashirikishe wengine ili kufanikisha jambo hilo lakini haujafanya hivyo?!

Leave a comment

name*

email* (not published)

website