Navigate / search

Makosa 4 yaliyofanywa na viongozi wa kwanza wa Nchi za Afrika

images

Afrika kama bara linatofautiana kwa utamaduni kati ya nchi moja hadi nyingine.ila nchi hizo zinafanana sana kwa historia na matukio ya kisiasa tangu zilipopata uhuru wao.Tangu Nchi ya Ghana ilipotangaziwa uhuru wake ni kama wimbi la kutaka mapinduzi Afrika liiliibuka.Kuanzia Julius Nyerere aliyeacha Ualimu na kuingia kwenye siasa,Robert Mugabe aliyeacha kazi ghana na kurudi zimbabwe ama aliyekuwa mfanyakazi wa posta Patrice Lumumba aliyeamua kujiingiza kwenye siasa.Ukifuatilia historia zao kuna mambo kadhaa ambayo ni funzo kwetu katika kizazi chetu,kwanzani kwamba nchi nyingi baada ya kupata uhuru zilijikita katika kujenga nguvu ya “founding fathers” kuliko kujenga taasisi zenye nguvu.Matokeo yake serikali iliendeshwa kawa kutegemea mtu mmoja.Athari kubwa ya hili ilikuwa ni pale walipoondoka madarakni wale waliochukua nafasi zao ilikuwa ngumu sana kuendesha nchi kwani hawakuwa na “commanding power” kama  ilivyokuwa kwa waasisi;na kwa kuwa taasisi zilikuwa dhaifu sana ambazo ndizo zilitakiwa ziwasaidie kuendesha serikali walishindwa kabisa kuendesha serikali hizo.Hii itakueleza kwa nini marais wa pili wa nchi nyingi zaz afrika wameingia katika rekodi ya kupinduliwa ama kuwa viongozi wabaya sana wa nchi zao.

Pili katika kizazi cha kwanza cha viongozi wa Afrika kulikuwa na watu abao walikuwa tayari kutumika kudhoofisha juhudi za dhati za viongozi wazalendo.Kuibuka kwa Patrice Lumunba Jamhuri ya demokrasia ya Kongo lilikuwa tishio kubwa kwa utawala wa kikoloni wa kibelgiji na mataifa ya magharibi.Hotuba yake siku ya uhuru wa Kongo ilikuwa kali ilyoeleza jinsi wabelgiji walivyoteseka chini ya utawala wa ukoloni na kueleza kuwa ukoloni umepatika kwa damu na sio kwa kupenda kwa wabelgiji.Hotuba hii iliyofanywa mbele ya rais wa ubelgiji na viongoiz wa jumuiya ya kimataifa ilikuwa ni mwanzo wa azimio la kumuua Lumumba.Ili kufanikisha hilo  walitumiwa wakongo wenzake,Moise Tshombe wa jimbo la Katanga na Kanali Mobutu aliyekuja kuwa Rais baadaye.Kule Burkina  Faso(The Land of Upright Men) baada ya tumaini jipya kuinuka kijana wa miaka 32 Thomas Sankara na kuindoa nchi yake katika utegemezi wa chakula,kuvunja rekodi ya chanjo kwa wananchi wake,kupunguza manunuzi ya magari ya kifahari kwa viongozi wa nchi na kuanza kuzalisha nguo nchini mwake badala ya kuagiza alituiwa rafikai yake wa karibu,Blaise Compaore ili kumuua.Hata leo kuna wengi wamekubali kutumika kinyume na viongozi wazalendo wa nchi zao.

Tatu ni kukithiri kwa rushwa na matumizi mabaya katika serikali za kwanza.Kwa sababu hakukuwa na taasisi imara ilikuwa rais sana kwa viongozi wa nchi hizi kufuja pesa na kuwa na amri juu ya rasilimali za nchi zao bila kuwa na “Oversight institutions”.Hii ilipelekea juhudi kubwa waliyokuwa wameifanya kuisia katika mikono ya walafi wachache.Katika nchi za Afrika ni jambo la kawaida kukuta familia tajiri ni zile ambazo zilikuwa katika kizazi cha kwanza cha uongozi,walitumia fursa hiyo kujitajirisha zaidi.Kwenye taasisi zilizoanzishwa kama vile mashirika ya umma nchini Tanzania uchungui unaonyesha kuwa wengi waliokuwa wamekanidhiwa nafasi hizo walikuwa hawana sifa na wafanyakazi walilipwa mishahara minono isiyoendana na uzalishaji wao.Hii ilpelekea serikali kuwa ndio inayoingiza pesa kuyaendesha na iliposhindikana mashirika haya yalikufa.Lakini pia ufisadi mkubwa ulifanywa na viongozi binafsi,wa kizazi kilichofuatia kama vilia mabavyo mobutu alikwapua zaidi ya dola bilioni 5 kutoka katika benki kuu ya kongo na kukodisha ndege ya concorde kumpeleka mtoto wake kwenye harusi Ivory Coast.

Nne,Viongozi wa kwanza hawakuwa tayari kuvumilia kabisa upinzani wa kimawazo.Na kwa sababu hiyo wengi walifanya mambo makubwa mawili.Moja ilikuwa ni kuitumia na kuipa nguvu “detention Act” sheria iliyokuwa inawaruhusu kumkamata mtu na kumswekaa ndani bila ya haki ya kujitetea kwa muda usiojulikana.Hii ndio ilitumika kumshughulikia Oginga Odinga kule Kenya,Ellen Sirlef kule Liberia na wengine wengi.Sheria iliyokuwa inatumiwa na wakoloni ilipendwa sana na watawala wa kawnza kwa kisingizio kuwa kuna wengi walikuwa wanataka kuwapindua na walikuwa wanatumika na wakoloni.Pili waliamua kufuta vyama vya siasa nchini mwao na kubakiza chama kimoja,kuanzia Nyerere wa Tanzania,Kenyatta wa Kenya,Nkrumah wa Ghana na Kaunda wa Zambia.Hii iliminya demokrasia na kutengeza kundi la watu wengi wasioridhika.Matokeo ya kutoruhusu utofauti wa mawao ndio uliopelekea kuibuka kwa vuguvugu nyingi za mapinduzi katka nchi za Afrika kwani kulikuwa hakuna namna rahisi ya ya kushiriki katika michakato ya kisiasa.Hii ndiyo ilipelekea kupinduliwa kwa Kwame Nkrumah akiwa nje ya nchi kwa ziara,Hii ndio ilipelekea jaribio la mapinduzi hapa Tanzania mwaka 1964.Ukweli ni kwamba kadiri unavyowanyima watu uhuru wa kujieleza ndivyo unavyozidi kutengeneza uasi ndani ya nchi yako.

Swali ni je?Makosa haya hayaendelei kuruddiwa na viongozi wa sasa?Niwekee maoni yako hapa chini Tafadhali.

 

Tujifunze kwa waliotangulia.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website