Navigate / search

Maamuzi 3 yatakayobadilisha Maisha Yako

Make-a-Decision-770x300

Eleanor Rooselvelt aliwahi kusema”I am who I am today because of the decisions I made yesterday-Maisha ninayoishi na vile nilivyo leo ni matokeo ya maamuzi niliyoyafanya jana) Namna pekee ya kubadilisha mwelekeo wa maisha yako ni kufanya maamuzi maishani mwako.Ni lazima UAMUE ili UPIGE HATUA.Watu ambao ni waoga kufanya maamuzi katika maisha yao siku zote wamekuwa ni watu wanaodumaa na hawasogei hatua mbele Zaidi.Kuna maamuzi ya aina tatu ambayo ni muhimu kuyafanya leo.

Ni kweli hauna pesa za kufanya biashara kwa sasa,lakini uje ukiendelea kukaa hivyo na kusubiri pesa zitakuja?Ni kweli umeumizwa katika mahusiano yako yaliyopita lakini je ukiendelea kulia maisha yatabadilika?Ni kweli umefeli katika elimu yako,lakini je ukiendelea kuwaza kufeli kwako maisha yatabadilika?Ni kweli wazazi wako wamshindwa kukusaidia lakini je ukiendelea kuwalaumu na kuwanung’unikia maisha yako yatakuwa bora?
Maisha huwa hayabadiliki kwa kuendelea kuangalia hali uliyonayo bila kufanya maamuzi ya kukupeleka mbele Zaidi.Kuna maamuzi mawiil lazima uyafanye leo:

1)Amua kubadilisha mawazo yako

Mawazo ndio chanzo cha mafanikio,usiruhusu mawazo yanayokukosesha furaha,mawazo yanayokufanya usikie maumivu au mawazo yanayokukumbusha kufeli kwako.Nguvu hiyohiyo unayoitumia kuwaza mawazo ya kushindwa,anza kuitumia kuwaza mawazo ya kushinda.Jiambei kila wakati;mimi ni mshindi.

2)Amua kuchukua hatua leo.

Hakuna kitu huwa kinabadilika chenyewe,unahitaji kuchukua hatua ya kubadilisha hali yako.Kazi haitakufuata,zifuate ziliko.Watu wengi huwa wanajipa majibu ya hapana kabla hawajajaribu,usijaribu kuhitimisha kuwa haiwezekani wakati bado hauajajaribu hata kidogo.Ukianza kuchukua hatua utashangaa mambo yatakavyobadilika maishani mwako,sio ngumu kama unavyofikiria.

3)Amua kutokata tamaa.

Kutokata tamaa ni matokeo ya maamuzi ambayo lazima uyafanye maishani mwako.Jiapize kuwa bila kujali nini kitatokea katika maisha yako,bila kujali hali zinazokuzunguka hivi leo,bila kujali wengine watasema nini juu yako,hautakata tamaa kabisa maishani mwako katika kufukuzia ndoto yako.
Maamuzi haya matatu yatakufanya upate mwelekeo mwingine mpya wa maisha yako katika kuitimiza ndoto yako.NDOTO YAKO INAWEZEKANA,KATAA KUKATA TAMAA.

Naamini katika Ndoto yako,
Naamini katika uwezo wako,
Naamini katika Hatima Yako.
SEE YOU AT THE TOP
Tembelea (www.joelNanauka.com) Kujifunza Zaidi.

Comments

Sonelo
Reply

Nimeipata hiyo message nashukuru sana mwalimu!

nanauka
Reply

Karibu tuendelee kujifunza

Aloyce
Reply

Sawa sawa sitarud nyuma ! Asante kwa ujumbe mzuri.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website