Navigate / search

Kufukuzwa kwa Mzee Hassan Nassor Moyo:Usaliti,Ujasiri,msimamo ?

_MG_1071

Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM aliyepata kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwaziri, Mzee Hassan Nassor Moyo alifukuzwa uanachama wa chama cha mapinduzi ambacho yeye ni mmoja wa waasisi wake, akiwa mwanachama namba 7.

Mzee Moyo (81) ni miongoni mwa viongozi waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tu baada ya Muungano, aliteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Kufukuzwa kumetokana na madai kuwa amekwenda kinyume na maadili ya chama pamoja na matamshi yasiyokubaliana na sera za chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa CCM mkoa wa Magharibi, Unguja, Aziza Iddi Mapuri, matamshi mbalimbali ya Moyo aliyokuwa akiyatoa katika mikutano ya hadhara inayofanywa na Chama cha Wananchi (CUF) inaonesha kwamba amekisaliti chama akiwa mzee wa kupigiwa mfano katika CCM.

Katika taarifa hiyo, imetoa mfano kuwa Aprili 30, 2014 katika mkutano wa CUF uliofanyika Kibandamaiti ambapo Katibu wa CUF, Seif Sharif Hamad alimsimamisha Mzee Moyo ambaye alisema serikali tatu ndiyo msimamo wa Wazanzibari wote.

Aidha, katika mkutano uliofanyika Tibirinzi huko Pemba Februari 9, 2014 Mzee Moyo alijitambulisha kuwa ni mwenyekiti wa maridhiano kutoka CCM ilhali si kweli, kwani Chama cha Mapinduzi hakimtambui kiongozi huyo.

Katika taarifa hiyo imesema CCM baada ya kutafakari kwa kina imebaini kiongozi huyo amekuwa akiongoza upotoshaji wa hali ya juu na hafai kuendelea kuwa mwanachama wa chama hicho tawala nchini.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, Mzee Moyo wakati akihutubia kongamano la CUF hapo katika ukumbi wa taasisi ya Kiswahili na lugha za kigeni, alibeza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema kwamba mkataba wa Muungano wa Aprili 22 haujulikani uliopo na wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba walikuwa hawajui wanachokifanya.

“Kutokana na matukio yote hayo na matamko anayoyatoa Mzee Moyo amepoteza sifa za kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi ambaye ni mfano wa kutegemewa wa wazee na vijana,” alisema.

Mzee Moyo baada ya Kufukuzwa alisema:

“Mimi sijutii kufukuzwa katika Chama Cha Mapinduzi kwa sababu sikuzaliwa kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi milele……natofautiana na CCM katika mambo mbali mbali ikiwemo suala la muundo wa muungano,’’ alisema.

Katika siku za hivi karibuni Mzee Moyo katika majukwaa ya CUF amekuwa akitamka bayana kwamba muungano wa serikali mbili umepitwa na wakati na Zanzibar ipo haja ya kuwa na mamlaka kamili.

Mbali ya uwaziri wa Katiba na Sheria katika Serikali ya awamu ya kwanza, nyadhifa nyingine alizotumikia Mzee Moyo katika serikali ya Muungano ni pamoja na mbunge kwa muda mrefu na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Hii si mara ya kwanza kwa Mzee Moyo kuleta kauli zenye utata kwani hata mwaka 1968 aliwahi kutoa tamko la kutaka chama cha ASP kivunjwe kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake vizuri na inasemekana alifukuzwa na wanachama wenye hasira waliokuwa mkutanoni na kuambiwa kuwa kama atataka kurudu ten abasi arudi na Karume.Kama kinavyoonyesha kipande cha barua ya Siri hapa chini.

11178347_10152693040751493_9052646565799401952_n

Ila swali kubwa linabaki:Alichofanya unakitafsirije:Ujasiri,Usaliti ama msimamo?

Leave a comment

name*

email* (not published)

website