Navigate / search

Kitabu “The Millionaire Next Door”-Mambo 9 yanayopelekea watu Kuwa mamilionea

millionaire_1890954b

Nimewahi Kusoma vitabu vingi sana vinavyohusiana na mambo ya Fedha na Utajiri lakini naweza kusema kitabu cha The Millionaire Next Door kilichoandikwa na Thomas Stanley(Phd) na William Danko(Phd) ni kati aya vitabu bora kabisa ambavyo nimewahi kuvisoma.Nadhani tofauti kubwa inatokana na ukweli kuwa waaandishi hawajaandika tu mawazo yao ama uzoefu wao bali kitabu chao kimetokana na utafiti wa Kisayansi.

Pamoja na Mambo mengi waliyoyazungumza ningependa nikushirikishe mambo 9 kwa ufupi sana ambayo nadhani yatakusaidia pia:(Kumbuka kuwa mamilionea tunawaowazungumzia hapa ni wa dola za kimarekani na utajiri tunaozungumza ni “wealth” na sio “rich”-Wealth ni kipimo cha unaweza kukaa muda gani bila kufanya kazi na ukaendelea kuishi maisha unayoishi sasa bila kupungikiwa)

1) FAMILIA ZA WATU MATAJIRI ZINA BAJETI

Nilishangaa sana niliposoma jambo hili.Fikra za wengi ni kuwa unapokuwa na pesa nyingi basi hauhitaji bajeti ya fedha zako,cha ajabu wakichogundua ni kuwa familia ambazo zilikuwa zinaangukia katika kundi la matajiri zilikuwa zina bajeti ambayo ilishirikisha mume na mke.
Familia za matajiri zinaweza kusema zinatumia kiasi gani kununua nguo kwa mwaka,chakula,nyumba n.k kwa upande mwingine familia ambazo si za matajiri huwa hazina bajeti kabisa za matumizi yao na hakuna mfumo wa kufuatilia nani ametumia nini katika familia.

2)MAMILIONEA WANAISHI CHINI KIDOGO YA KIPATO CHAO

Ili uweze kukusanya utajiri ni lazima mapato yako yazidi matumizi yako,katika utafiti wao waligundua kuwa mamilionea wengi wanaishi chini Kidogo ya Kipato chao.kwa maneno mengine wanajitahidi kwa kila wananchoingiza waweze kuwa na akiba ya kuwekeza.Wanaoendelea kuwa chini ni wale ambao kila wanachoingiza wanakula na hakuna wanachobakiza.

3) MAMILIONEA HAWAENDESHWI NA HADHI(STATUS)

Kitabu kimeeleza kitu cha kushangaza kuwa mamilionea wengi hawaendeshwi na maisha ya kupenda kuonekana na hadhi ya juu inayoambatana na matumizi makubwa ya pesa kwa ajili ya vitu vinavyoonekana kama vile nguo ama magari.Cha Kushangaza mamilionea takribani 25% walikutwa hawajabadilisha magari yao kwa miaka kadhaa lakini wale wasio mamilionea huwa wanabadilisha magari takribani kila mwaka.

4) MAMILIONEA HUJIKITA KUJENGA TABIA ZA KUWAWEZESHA WATOTO WAO KUWA MAMILIONEA

Tofauti kubwa ya mamilionea na wengine ni kuwa wao huwa wanawajenga watoto wao kupata tabia(characters) za kuwasaidia kuwa mamilionea na sio kuwapatia pesa.Huwa wanawajenga kifikra kama vile kuwajengea uvumilivu,uaminifu,kufanya kazi kwa bidii n.k wakati wazazi wasiokuwa mamailionea kazi yao ni kutoa misaada ya kifedha kwa watoto wao hadi wanakuwa wakubwa matokeo yake watoto wanashindwa kujenga tabia zinazofaa, na utafiti unaonyesha kuwa watoto hawa hugeuka kuwa wakopaji sana wakiwa watu wazima lakini mamilionea wao huwajengea tabia za kupata utajiri watoto wao ilili kuweza kutengeneza utajiri wao wenyewe.

5) WATOTO WAO WANASOMA MASOMO GANI

Mamilionea wengi walionekana wanapenda watoto wao wasome masomo ambayo hata ajira ispokuwepo wataweza kujiajiri.Kwa marekani watoto wengi wa mamilionea wanasoma sheria na uhasibu.Ingawa mamilionea hawa hawawapatii watoto wao pesa za kufuja za matumizi lakini wako tayari kutoa gharama yoyote ili watoto wao wasome vyuo vikuu bora Zaidi.

6) LAZIMA KWA WANANDOA WOTE(Home Team) MJIFUNZE KUISHI CHINI YA MAPATO YENU

Wameeleza kuwa katika utafiti wao kama watu mko katika ndoa lazima wote wawili muwe tayari kuishi chni ya kiwango cha kipato chenu na sio vinginevyo.Ikitokea mmoja hayuko tayari basi inakuwa ni jambo gumu kulifanikisha.

7) MAMILIONEA WANATUMIA MUDA MWINGI KUFIKIRI NA KUPANGA KUHUSU KESHO YAO

Iligundulika kuwa mamilionea wengi huwa wanatumia muda mrefu kwa kila siku na kila wiki kufikiri na kupanga juu ya kesho yao katiaka eneo la fedha na uwekezaji.Hata hivyo wengi wasio mamilionea huwa hawatumii muda wao kabisa kujipanga kuhusu kesho wataongezaje kipato ama namna wanavyoweza kuongeza uwekezaji wao(wako tayari wakeshe kwenye TV lakini hawana muda kupanga mipango ya kujiinua kiuchumi).Mamilionea huwa wana malengo yaliyo dhahiri sana kuhusu mbeleni wanataka wafanikiwe katika mambo gani na kwa kiwango gani pia.

8) KINACHOWASUKUMA KUFANIKIWA NI UHURU WA KIFEDHA

Mamilionea wengi kinachowatia hamasa kufanya mambo yao kwa bidii ni ili kupata uhuru wa kifedha maishani.Hata hivyo wale wasio mamilionea kinachowasukuma kufanya mambo yao ni ili waweze kulipia gharama za maisha zinazowakabili.Je wewe unafanya unachofanya kwa lengo lipi?

9) MAMILIONEA WANATENDA WANACHOSEMA

Mamilionea huweka vipaumbele na mipango yao na kuiishi kila wakati lakini wasio mamilione huweka mipango na hwana nidhamu ya kuishi kwenye mipango hiyo.

Kiufupi ni kuwa ukichunguza maisha ya mamiliionea matendo yao yanendana na maneno na mipango yao lakini wanaohindwa kuwa mamilionea huwa hawafikii malengo hayo.

Kitabu hiki ni kizuri sana kwa mtu anayependa kujifunza matokeo ya tafiti kina namba nyingi zilizotumika na majedwali amabayo yanasaidi pia kuweza kuelewa kwa kiwango kikubwa.Ni vizuri kutambua kuwa wengi wanaoonekana wana pesa huwa ni”riches” ila sio “wealth” hii ndio maana wengi wakiacha wanachofanya (boking,football etc) hurudi kuwa maskini wa kawaida.Ni vizuri tujipange kuwa wealth ili tueache urithi kwa watoto wetu pia.

Nakutakia Mafanikio Makubwa Ya Kifedha Mwaka Huu.

Comments

Manase Mlonganile
Reply

Asante Mheshimiwa Nanauka.

Nawexa kupata wapi hiki kitabu kwa hapa mjini?

Ubarikiwe.

nanauka
Reply

Tembelea duka la Scholastica pale M.city

Manase Mlonganile
Reply

Asante

John Nu
Reply

Aisee! Yaani nimesoma hizo point nimepata kitu cha tofauti ubarikiwe sana mtumishi
Itabidi nikitafute hicho kitabu

nanauka
Reply

Nafurahi kama imeklusaidia.Ni kizuri sana kitafute.

Abdiel Elisha
Reply

Nakuelewa sana mtu wa Mungu.
Joel Nanauka…kazi yako ni kubwa sana!

nanauka
Reply

Nashukuru kusikia inakusaidia,naamini ndoto yako lazima itatimia.

Abdiel Elisha
Reply

Najifunza vingi kwako mkuu..
Mungu akupe maisha marefu..

Venance
Reply

Nimefatilia point za hii mada zimenipa jambo kubwa sana asante sana kwa ushauri wa bute. Na naweza pata nafasi ya kuwepo kwenye group la whatsapp maana nilituma sms lakini sikupata majibu yoyote.

nanauka
Reply

karibu sana,naomba utume tena nambari yako na jina lako kwenye namba 0743 86 85 07

Emmanuel Msemakweli
Reply

Kazi nzuri sana kiongozi. Unatusaidia wengi sana.!
Barikiwa.

juma issa
Reply

thnx mh mbunge

oliver charles mpandula
Reply

Nashukuru saaana mkuu ubarikiwe

nanauka
Reply

Amina Oliver,NASHUKURU SANA

oliver charles mpandula
Reply

Maisha ni mtego ukikosea utanasa.

Moses Mkemwa
Reply

Asante sana kwa somo zuri.Hakika tunahitaji elimu hii kwa ustawi endelevu wa maisha yetu hapa duniani.Mungu akubariki sana brother Joel.

nanauka
Reply

Amina Moses,nashukuru kwa kutembelea website.Tuendelee kujifunza.

oliver charles mpandula
Reply

Tegemeo langu ni Mungu dhamira yangu ndio ndoto yangu

oliver charles mpandula
Reply

Workhard is a most powerfully in success

GERVAS
Reply

NIMEKUWA MFUATILIAJI WA MADA ZAKO HONGERA,HICHO KITABU CHA MILIONEA NEXT DOOR KWA TULIOPO MIKOANI UNAWEZA KUNITUMIA NIKITUMA PESA?

nanauka
Reply

naomba uwasiliane na mratibu wa mentroship Programme,Daudi Mwalilino 0655 720 197 atakupa maelekezo ya jinsi ya kukipata.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website