Navigate / search

Kashfa Ya Nkandla:Jinsi Upinzani Unavyoweza Kusimamia Uwajibikaji

EFF-Parliament

Ripoti ya Thuli madonsela kiongozi wa taasisi ya kutunza na kutetea mali za umma(Public Protector) aliandika ripoti kuhusu kashfa ya uboreshaji wa makazi ya nyumba binafsi ya Rais Zuma.Katika ripoti hiyo iliyokuwa na kurasa 400 ilieleza kuwa Rais Zuma amekiuka katiba kwa kuisababishia serikali hasara katika uboreshwaji wa makazi yake kwa kujenga vitu ambavyo havikuhusiana na masuala ya usalama kama ilivyokusudiwa kama vile uzio wa zizi la ng’ombe,bwawa la kuogelea,ukumbi wa sinema n.k.Gharama ya matengenezo ilikisiwa kuwa ni randi milioni 27 lakini hadi rtipoti inatolewa ilikisiwa imeshatumika randi milioni 206.

Ripoti ilibaini kuwa gharama iliyotumika katika marekebisho na matengenezo ya nyumba ya Zuma ni mara nane ya gharama ya kununua nyumba gharama zilizotumika kununua nyumba mbili za Nelson Mandela na ni Zaidi ya amra 1,000 iliyotumika kwa rais mtangulizi wa Mandela bwana FW De Clerk.Ripoti ilimtaka bwana Zuma Kulipa pesa zote zilizotumika kwa vitu visivyohusiana na mambo ya usalama kiasi cha takribani.Hata hivyo ripoti iliyotolewa na kamati ya uchunguzi ya serikali ilitoa tamko kuwa Zuma hajafanya kosa na marekebisho yoteb yalikuwa yamefuata kanuni na taratibu.

Hapo ndipo sarakasi zilipoanza;uzalendo ukishindana na kutetea chama na kumtetea kiongozi wa chama na serikali.Kwanza chama tawala kilionyesha kutoridhishwa na ripoti hiyo na kuanza kumshambulia public protector.Rais Zuma kwa kutumia mazoea ya kawaida,akatamka kuwa hatalipa hizo pesa.
Nguvu ya vyama vya upinzani ndipo ilipoingia na kwa mara ya kwanza ikasababisha kuwe na umoja wa ghafla kati ya Democratic Alliance(DA),Congress of the People(COPE) na Economioc Freedom Fighters(EFF) cha Bwa.Julius Malema mshirika wa karibu sana wa zamani wa Rais Zuma.Mwendelezo wa sakata hili ulitoa mafunzo yafuatayo:

Moja ni kuwa vyama vya upinzani viliamua kutumia mahakama ya kikatiba kutafuta haki yao kwa kufungua kesi dhidi ya Zuma ya Kumtaka kulipa pesa sawasawa na ripoti ilivyokuwa inasema.Jambo zuri ni kuwa mahakama baada ya kupitia kesi hiyo ilifanya maamuzi na kusema kuwa Zuma amevunja katiba na kushindwa kusimamia kiapo chake cha ofisi ya Rais hivyo anatakiwa alipe.Hii inamaanisha kuwa upinzani usichoke kutumia vyombo rasmi vya sharia bila kujali huko nyuma kama vilionewa ama la.

Pili,ni vita iliyokuwepo ndani ya bunge pale wapinzani walipoamua kupeleka hoja ya kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Jacob Zuma.Nilipata bahati ya kuangalia Jinsi Mmusi Maimane,Kiongozi wa DA alivyowasilisha hotuba yake na pia Julius Malema ili kushawishi wabunge wa ANC wawaunge mkono kumwangusha Zuma.Ingawa waliongea kwa uchungu na kuonyesha jinsi Zuma ameshindwa kutetea kiapo chake na amevunja katiba ya nchi bado wabunge wa chama tawala cha ANC walipiga kura ya kuwa na imani naye.Hivyo ndivyo “namba” zilivyoshinda katika kutetea mvunja katiba.Kwa kutoridhsishwa na hilo,wapinzani waliamua kutoka nje ya bunge na wasiendelee na bunge.

Tatu,kulikuwa na vita kubwa sana ndani ya bunge hasa baada ya EFF kuleta hoja kuwa hawana Imani na spika wa bunge,Baleke Mbete kwa kuwa tangu mwanzoni ripoti ya Nkandla ilipoletwa bungeni alionekana kumtetea na kumsaifisha Zuma .Hivyo walimtaka akae pembeni apishe mjadala uendelee.Baleka alipinga na aling’ang’ania kwenye kiti bila kujali hoja za upinzani.Hapa ndipo utaona jinsi gani spika wa bunge anavyoweza kuwa kikwazo katika kulisaidia bunge kutimiza wajibu wake wa kuisimamia serikali.

Ingawa hoja ya kumtoa zuma ilipingwa na ushindi ulipatakana upande wake,ila angalau hukumu ya kumtaka alipe pesa za wananchi ilitolewa na atatakiwa kufanya hivyo.Ingawa wabunge wa ANC walitumia sana uwingi wao kumtetea Zuma,walizidiwa sana kwa hoja na walio wachache.Bila upinzani kuweka nguvu kubwa katika suala la Nkadla,pesa za wananchi zingepotea na kusingekuwa na uwajibikaji.

Hii inatufundisha kuwa kama upinzani ukiwa imara katika kusimamia masuala ya uwajibikaji katika serikali,bila kujali idadi ya wabunge ilionao inawezekana kabisa kuleta tofauti katika nchi.

Kiufupi ni kuwa Upinzani imara unatakiwa usimamie masuala muhimu ya kutetea wananchi bila kuchoka na kuhakikisha kuwa inaiwajibisha serikali ili kuhakikisha haki za wananchi zinatetewa.Zitafutwe ripoti mbalimbali zifanyiwe kazi na zifuatiliwe hadi mabadiliko yaonekane bila kuishia njiani.

Joel Nanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website