Navigate / search

Kanuni Ya Solid Ground Itakusaidia Kuvuta Fursa Kubwa

Siku Moja wakati nasoma kitabu cha kanuni 21 za Uongozi kilichoandikwa na John C. Maxwell nilkikutana na kanuni mojwapo muhimu sana kwa kiongozi inaitwa “The Law of Solid Ground”.Na moja ya kitu ambacho alieleza kuhusiana na kanuni hii alisema kuwa “Mtu yoyote yule hawezi kufanikiwa sana katika maisha yake na kufikia MALENGO Makubwa kama wakati pekee ambao anafanya mambo ya muhimu ni pale tu ambapo huwa anajisikia kufanya hivyo,na kama hajisikii basi huwa hafanyi chochote”
Hii ni tabia amabyo inaweza kuwatoautisha watu wengi sana katika maisha,hasa kati ya wake ambao wanafanikiwa na wale ambao hawafanikiwi.Tofauti ya kuwa mtu mkuu na kuwa mtu wa kawaida ni kwamba wale wanaokuwa ni wakuu huwa wanafanya mambo muhimu sana kwenye maisha yao hata kama hawajisikii kufanya ila wale wengine huwa hawafanyi hadi wapate hisia za kufanya hivyo.
Nidhamu yako ya kufanya mambo bila kutegemea hisia zako ni moja ya kitu muhimu zaidi unachokihitaji ili kufikia kilele cha mafanikio.Kama wewe ni aina ya watu ambao huwa unafanya mambo pale tu ambapo unajisikia vizuri na baada ya hapo haufanyi tena hadi ujisikie vizuri basi utakuwa mtu ambaye haufiki sana mbali katika maisha yako.Kanuni ya Solid Ground inakutaka uwe mtu ambaye unaweza kuaminiwa na watu wengine kwa kusimamia mambo muhimu ya maisha yako.Na leo ningependa tuone mambo mawili ya muhimu kuhusiana na kanuni hii:
Moja ni kuwa ni lazima uwe mtu ambaye unasimamia ahadi zako unazotoa kila wakati.Kwa maneno mengine usikubali kuwa mtu ambaye unasema na hausimamii kitu ambacho umekisema.Hata wakati mmoja usiwe mtu ambaye unasema kitu ambacho haumaanishi kukifanya katika maisha yako.Kabla haujatoa ahadi yoyote ilekatika maisha yako jitahidi sana kupima dhamira na uwezo wako wa kuitekeleza.Kabla haujachukua hatua yoyote ile kukubali kufanya kitu toka kwa mtu,jikague kama kweli umedhamiria kufanya.Gharama ya kukataa kufanya kitu na kutokueleweka ni ndogo sana ukilinganisha na gharama ya kukubali na kutokufanya.Watu wakianza kusema kuwa wewe ni mtu ambaye hauaminiki katika ahadi zako,hii itakuathiri sana katika kutimiza malengo uliyonayo.Kumbuka kuwa sifa zako mbaya huwa zinaenea kwa kasi zadi kuliko sifa zako nzuri.
Sifa ya kuwa mtu ambaye huwezi kuaminika ni mbaya zaidi kuliko sifa nyingine yoyote ile ambayo uanweza kuwa nayo katika maisha yako.Mtu akisikia hauaminiki na wala hausimamii ahadi unazotoa,inamaanisha kuwa hatakuwa tayari kufanya jambo lolote lile na wewe wala hatakuwa tayari kukusema mbele ya watu wakati fursa fulani inapotokea.
Mbili ni muhimu sana kuwa mkweli.Ni jambo lisilopingika kuwa ukweli una gharama kubwa,lakini pia ni jambo lisilopingika kuwa upongo una gharama kubwa sana kuliko ukweli.Kati ya sifa zinazoongoza kwa kukimbiza watu muhimu kwenye maisha ya watu wengi ni tabia ya kutokuwa wakweli.Watu wakigundua kuwa wewe sio mtu mkweli katika kila unachosema basi kila wakati hawatakuamini na hawatakuchukilia kama mtu makini wa kufanya nao kazi.
Inawezekana tabia ya kusema uongo imeshachukua nafasi kubwa sana katika maisha yako kwa sasa na unaweza kukumbuka ni mara ngapi kwa sababu ya tabia hii umepoteza watu muhimu sana ama umepoteza fursa.Kama wewe unajua kuwa uansumbuliwa bado na tabia hii-Ni vizuri kuanzia leo,kila wakati uanpojigundua kuwa umesema uongo na ukigundua-Jiambie kuwa “Sitaki kusema tena Uongo”.Kila utakaposema hivi utaanza kujijengea kuwa kama moja ya “value” yako na utashangaa wakati mwingine ukitaka kusema tu uongo unakumbuka na utaanza kupata ujasiri wa kusimamia ukweli.
Kumbuka kuwa kanuni ya Solid Ground ndio huwafanya watu wavutie watu muhimu kwenye maisha yao ama wawafukuze.Kuanzia leo zingatia hatua hizi mbili kama sehemu ya kuanza kujenga uwezo wako wa kutembea katika kanuni hii.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website