Navigate / search

Kanuni Ya Parkison:Ili Ufanikiwe Lazima Uikiuke

Breaking_technique

Kwenye kujifunza kuelekea mafanikio,nimekuwa nakutana na kanuni nyingi sana ambazo unatakiwa uzifuate.Ila kwa mara ya kwanza siku moja nilikutana na kanuni ambayo nilikuwa natakiwa kuivunja.Kanuni hii inaitwa “Parskison’s law” iliyotungwa na mwandishi mwingireza C. Northcote Parkison ambaye aliitumia kuelezea kwa nini wengine hufanikiwa kifedha na wengine hufeli.

Kanuni hii inasema bila kujali mtu anaingiza pesa kiasi gani,atajikuta matumizi yake yanaongezeka kwa kasi kiwango ambacho pesa anahitaji kutumia pesa yote anayopata ama hata kuhitaji kukopa Zaidi ili atomize mahitaji yake.Kanuni hii inaeleza kuwa watu wengi wanapata kipato/mshahara mkubwa Zaidi kulinganisha na kipato/mshahara wao wa kwanza kabisa,lakini cha ajabu ni kuwa kila siku inaonekana kuwa pesa wanazopata haziwatoshi kabisa.

Kutokana na kanuni hii mafanikio yako ya kifedha yataanza kutokea pale ambapo utaamua kwa makusudi kuivunja/kuikiuka kanuni hii.Hii ina maanisha kuamua kwa makusudi kuwa hautakuwa tayari kuongeza matumizi yako kwa kiwango ambacho utakosa hata pesa ya kusave ama kwa kiwango Zaidi ya kipato chako.

Hivyo basi,ili kufanikiwa kuikiuka kanuni hii unatakiwa kutumia mfumo unaitwa “wedge”,ambayo humaanisha ni kufanya matumizi yako yawe chini ya kiasi cha mapato yako na kisha kuamua kuwekeza(invest) ama kuhifadhi(save) kiwango cha ziada kinachobaki.Kama utafanya hivi kwa muda mrefu hapo ndipo utakapoanza kujiondoa katika duara la umaskini.

Njia nzuri ya kukusaidia kuikiuka kanuni hii kwa faida yako ni kuorodhesha matumizi yako yote uliyonayo kwa mwezi,na kisha kuamua ni matumizi gani unaweza kuyapunguza ama kuyaondoa kabisa.Kumbuka kuwa,ili kufikia malengo yako lazima ufanye “sacrifice”(ujitoe kupita kawaida) na ukubali kukosa baadhi ya vitu kwa muda ili upate unavyotaka.

Endelea Kutembelea www.JoelNanauka.Com Kujifunza Zaidi,na kama ujumbe huu umekuwa na manufaa zaidi,unaweza kushare na rafiki zako.Pia unayo fursa ya kujiunga na mtandao wa washindi ili kujifunza zaidi kupitia watsapp group bila gharama yoyote;Tuma neno “NDOTO YANGU”,Ikifuatiwa na jina lako kwenda namba 0655 720 197.

Ili kupata Makala za kila wiki za kujifunza jinsi ya kuifikia ndoto Yako,tafadhali nenda kwenye website yangu na chini upande wa kulia kwenye “weekly newsletter” andika email yako pale kisha itume.
Ndoto Yako Inawezekana,

See You At The Top.

Comments

FIDELIS NDOGHWE
Reply

Nimefurahi Kwa SOMO nzuri sana unalotoa Mr Joel Nanauka

nanauka
Reply

Karibu sana Fidelis.

FIDELIS NDOGHWE
Reply

SOMO zuri sana

Ramadhani ngwali
Reply

Somo ni zuri sana…. Nabalikiwa sana

Leave a comment

name*

email* (not published)

website