Navigate / search

Kanuni Mbili Muhimu Za Mafanikio

Siku moja baada ya mtu mmoja kuwa amesoma Makala yangu kwenye gazeti mojawapo ninaloandikia alinipigia simu ili kunieleza jinsi Makala ile ilivyokuwa imemgusa moyo wako.Hata hivyo baada ya kutumia dakika chache kunieleza jinsi ambavyo imemsaidia akaanza kushusha malalamiko jinsi ambavyo yeye amekuwa akifanya kile kitu ambacho nilikiandika kwa muda mrefu sana bila kupata matokeo ya kuridhisha katika maisha yake.Nilipojaribu kumuuliza amekuwa akifanya hivyo kwa muda gani,nilishangaa sana kugundua kuwa alifanya hivyo kwa miezi mitatu tu na tayari ameshaanza kuchoka kwa sababu haoni matokeo.

Hili ni jambo linalowatokea watu wengi sana katika maisha yao,kila wanapoanza kufanya jambo fulani basi huwa wanatamani kupata matokeo ya harka,na kwa namna yoyote ile matokeo ambayo waliyatarajia yakichelewa basi huwa ni watu wa kukata tamaa na huanza kuacha kile walichokuwa wanakifanya.Kila mtunisha misuli unayemuona ukijaribu kumuhoji kuhusu safari yake hadi akafanikiwa kutunisha misuli atakuambia kuwa ilimchukua muda mrefu sana kujenga huo mwili alionao.

Sasa kuna watu wanatamani kuwa na misuli mikubwa namna hiyo ila wakienda Gym siku wiki moja tu na wasipoona matokeo waliyokuwa wanayatarajia basi huanza kukata tamaa.Mafanikio ya kweli siku zote kumbuka ni matokeo ya kufanya kitu kwa muda mrefu unatakiwa hadi umepata matokeo ambayo ulikuwa unayatarajia.Hivyo bila kujali umeanza kutumia kanuni gani na kufuatilia kufanya jambo lipi kwa vitendo,usikubali kukatyishwa tamnaa eti kwa sababu hauoni matokeo kwa haraka kama ambavyo ulitarajia hapop mwanzoni.

Vilevile jambo lingine la kuzingatia ni kuwa,hakuna kanuni moja inayotosha kukuletea mafanikio.Ili ufikie katika kilele cha juu cha malengo uliyojiwekea basi ni lazima utumie kanuni mbalimbali ambazo ukizichanganya zitakupa matokeo ambayo yanakusudiwa.Kufikia mafanikio ni kama vile mfumo wa mwili wako unavyoendeshwa-Unahitaji mfumo wa hewa,maji,chakula,damu n.k-Ndivyo ilivyo na kwenye mafanikio yako pia,utahitaji kuwa na kanuni mbalimbali amabzo ukiozijumlisha ndio zitakupa matokeo makubwa.Usiwe aina ile ya watu ambao wao wanajau kanuni moja tu na wanashikilia hivyo bila kujua kuwa wanahitaji kanuni mbalimbali ili kukamilisha uwezo wao wa kufanikiwa.

 

Leo ningependa  kukushirikisha kanuni 2 ambazo ni lazima uzizingatie kwa muda mrefu na kwa umoja wake bila kukata tamaa hadi uone matokeo uanyoyatafuta:

Kanuni ya kwanza ni kujifunza kwa wale ambao tayari wameshafanikiwa.Kwenye eneo la mafanikio huwa tunasema,mafanikio yanaacha alama.Hii inamaanisha kila aliyefanikiwa kuna njia ambayo alipita ambayo ukiifuatilia kwa umakini utagundua kuwa kuna mambo mengi ya kujifunza yanayoweza kukusaidia kuepuka makossa waliyofanya wengine ama kujua namna bora ambayo waliifanya ili kupata matokeo waliyonayo.

Kanuni hii inamaanisha kuwa mafanikio ni matokeo ya kanuni ya kichocheo na matokeo ambayo inasema kuwa –kwa kila matokeo unayoyaona lazima kuna kichocheo fulani,hivyo kama unataka kupata matokeo ya namna hiyo uanchotakiwa kufanya ni kutafuta kichocheo nawe ukifanye iili upate matokeo.Hii ndio maana kati ya maswali muhimu unayotakiwa kujiuliza kwa kila aliyefanikiwa ni kuwa alifanya nini kupata matokeo aliyonayo.Mafanikio huwa hayachagui sura,kabila wala rangi-Ukifanya yale ambayo wengine wanafanya utapata matokeo ambayo wengine wamepata.

Hii inamaanisha usiwe aina ile ya watu ambao wanapotaka kufanya kitu wanarukia tu na kuanza,hapana.Kama unataka kufanikiwa jitahidi kwa kila ambacho unataka kufanya tafuta watu amabo walishafanya kitu kionachofanana na hiko.Waulize maswali walianazje,walikoseea wapi n.k-Hii itakusaidia sana kujiepusha na makosa ambayo watu wengi sana wamekuwa wakiyafanya kwa sababu tu ya kutotaka kujifunza kwa wengine.

Kuna watu wamepoteza mitaji,wamepata hasara katika kilimo n.k kwa sababu tu walishindwa kutenga muda wa kujifunza kwa waliiotangulia ili wapunguze makossa.Watu husema kuwa wenye hekima hujifunza na makossa yao ila wenye hekima zaidi hujifunza kwenye makossa yaw engine.Siku moja nilimsikia askofu David Oyedepo anayemiliki vyuo vikuu vitatu kwa sasa nchini Nigeria akisema kuwa kabla hajaanzisha chuo chake cha kwanza alisoma historia ya takribani vyuo vikubwa thelathini duniani.Usiwe na haraka ya kuanza jambo bila kujifunza,iweke kuwa  ni kanuni yako ya kila wakati na utaona jinsi ambayo utapunguza makossa na kuongeza ufanisi.

Kanuni ya pili ni ile ya kuamua kuwa sasa imetosha(enough is enough).Kila maisha ya mtu huwa yanabadilika siku moja maalumu.Katika siku hii kwa nje atabakia kuwa wa kawaida lakini kwa ndani akili yake itakuwa imeshachukua mtazamo mwingine kabisa.Hii ndio ile siku inaitwa-“Enough is Enough”,IMETOSHA.Bila kufikia hatua hii basi ujue maisha yako yatachelewa sana kubadilika.

Hii ndio ile siku ambayo unaamua kuchukua maamuzi yasiyo ya kawaida si kwa sababu ni marahisi ama yanawafuhisha watu ila kwa sababu ni muhimu katika maisha yako.Hii ndio siku ambayo uanaamua kuwa hautaki kuwa maskini tena na utajihatarisha kufanya yote yanayowezekana ili kubadilisha hali yako ya sasa.

Hii ndio siku ambayo unasema nimeumia sana katika mahusiano haya na sasa inabisi nifanye maamuzi,ndio ile siku ambayo mtu anasema nimeshateseka sana katika kazi hii na sijaona maendeleo ngoja nifanye maamuzi ya kuondoka.Ukweli ni kuwa siku hii inaogopwa na wengi ila ndio iliyobadilisha wengi.Watu wengi sana wameendelea kuwa vile walivyo miaka yote bila mabadiliko kwa sababu hawajawahi kufiak hatu ya kusema imetosha sasa.

Wengi hawapendi kuchukua maamuzi ya namna hii na kuifikia hatua hii kwa sababu wako tayrari kuendelea kuumia pale walipo kuliko kujaribu kupata faraja bila kuwa na uhakiak.Mwanafalsafa mmoja waliwahi kusema kuwa wanadamu ni watu wa ajabu sana kwani wako tayari kuenedelea kuvumilia katika jehanamu wanayoijua kuliko kujaribu kutafuta mbingu wasiyoijua.Hii inamaanisha kuna watu wengi sana wanatamani kubadilika ila kianchowakwamisha ni kujiuliza-Itakuwaje nikichukua hatua nisipofanikiwa?

Inawezekana na wewe ni mmoja wa hawa watu.Kumbuka-Huwezi kubadilisha hali yako ya sasa bila kufikia hatua ya kusema umechoshwa kabisa na hali yako ya sasa.

Je uko tayari leo kusema “Enough is Enough?”-IMETOSHA.

Kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO kimeelezea mbinu 60 ambazo watu waliofanikiwa wanazitumia kufikia kilele cha mafanikio yao.Unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba 0655 720197 na tutakuelekeza kwa wakala wetu katika mkoa uliopo ama kama uko Dar Es Salaam na unahitaji kuletewa hadi pale ulipo uanweza kuwasiliana nasi kupitia 0712 224282

See You At The Top

Leave a comment

name*

email* (not published)

website