Navigate / search

Kama Haben Girma ameweza,Nawe Utaweza

Mwaka 2015 kuna habari kubwa sana ya kusisimua ilitolewa kuhusu dada mmoja anayeitwa Haben Girma.Kilichofanya habari hii iwe kubwa ni kwamba dada huyu alikuwa ni mtu wa kwanza ambaye ni kiziwi na kipofu kuweza kumaliza masomo ya sheria katoka chuo kikuu bora kabisa nchini marekani cha Harvard.
Haben alizaliwa nchini marekani baada ya wazazi wake ambao ni watu kutoka nchini Eritrea kukimbilia marekani kama wakimbizi.Katika familia yake sio tu yeye alizaliwa katika hali hiyo ya kuwa kipofu na kiziwi,lakini pia kaka yake.
Katika hali ya kawaida alikuwa Haben alikuwa na kila sababu ya kujihurumia na kutafuta kuhurumiwa pia katika maisha yake,lakini alikataa na akaamua kuisishi ndoto yake ya kuja kuwa wakili.Umeshawahi kufikiria watu walikuwa wanasemaje alipokuwa anawaambia kuwa anataka kuwa mwanasheria na wakili katika maisha yake?
Kutokana na maisha yake na mafanikio yake,kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika kuelekea ndoto zetu:
Moja ni kuwa lazima tuamue kuziamini ndoto zaidi ya vile tunavyoamini katika kutokuwa na uwezo wa kuzitimiza.Mara nyingi sana tuanapokuwa tunataka kuakmilisha jambo fulani katika maisha yetu,kitu cha kwanza ambacho hutujia ni kuangalia jinsi ambavyo tuan udhaifu,ambavyo hatuna pesa,ambavyo hatujasoma ama historia zetu.Na kwa sababu hii watu wengi sana wamejikuta wakiwa wanashinda kuchukua hatua zinazotakiwa kwa wao kuweza kusonga mbele.Leo hebu angalia kama wewe pia ni mmoja wa wale ambao kila wakati wamekuwa wanatumia visingizio vya udhaifu na mapungufu waliyonayo kushindwa kabisa kuendelea mbele katika maisha yao.
Haben alikuwa na haki kabisa ya kutumia ulemavu wake kama kisingizio cha kuwa ombaomba ama kushindwa,lakini aliamua kuwa tofauti.Hii ni kusema kuwa hakuna udhaifu wowote ulio nje yetu unaoweza kutuzuia kama ndani yaetu tutakuwa tumeamua kufukuzia ndoto zetu.Ni lazima uamua kuwa bila kujali una udhaifu gani,ama una mapungufu gani-Huu sio wakati wa kusema mimi siwezi kwa sababu fulani fulani,bali huu ni wakati wa kuamini kuwa chochote unachotaka kianwezekana.
Hebu fikiria hivi kama angeamua kutoa visingizio kuna mtu angeweza kumlaumu kweli?Kwa hali aliyonayo kila mtu angemwelewa.Hata wewe unaweza kuwa na visingizio ambavyo kila mtu anaweza kukuelewa lakini kama kweli unataka kufikia malengo yako ni lazima uamua kuishi tofuati sana na usiwe mtu wa visingizio.
Jambo la pili ni kuwa Haben,hakuataka kusubiri kuhurumiwa na mtu yeyote yule aliamini kuwa anao wajibu yeye mwenyewe.W atu wengi sana hata sasa wameshindwa kufikia malengo yao kwa sabau huamini kuwa kuna mtu mahali fulani anawajibika na maisha yao.Na ahii huwasababishia kila wakati wawe watu wa kulamumu na kutafuta mtu wa kumsema kuwa ndio sababu ya kushindwa kwao.
Haben hakulaumu Mungu,hakulaumu wazazi,wala hakulaumu mtu yoyote yule.Pia heben hakusubiri mtu wa kumsaidia.Aliamua kuchukua hatua mara moja bila kujali nani ni sababu ya yeye kuwa vile alivyokuwa.
Huu ndio moyo unaotakiwa kuwa nao pia;Usikubali kushindwa kuendelea mbele kwa sababu ya kuamini kuwa kuna mtu ambaye amesababisha wewe uwe vile ulivyo sasa,usikubali kuamini kuwa bosi wako,wazazi,mume wako,mke wako,mwanasiasa fulani au mtu yoyote yule eti ndio amekuwa sababu ya wewe kuwa hivyo ulivyo leo na kwamba hauan uwezo kabisa wa kufanikiwa kwa sababu hiyo.HAPANA.
Usisubiri kuhurumiwa na mtu yoyote.Fanya kama vile Heben alifanya,chukua hatua ta ujasiir na anza kuiishi ndoto yako.Anza kufuatilia malengo uliyojiwekea kwa kasi sana.Usijifungie tu ndani ukisubiri kuhurumiwa,usiwe tu mtu wa kulaumu wengine-Unao uwezo wa kubadilisha maisha yako ukiamua.
Kama Haben ameweza,naamini na wewe utaweza pia.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website