Navigate / search

Jinsi ya Kutumia muda wako vizuri ili Ufanikiwe

IMG_1948

Kati ya vitu ambavyo unatakiwa kuvithamini sana maishani mwako ni matumizi ya muda wako.Watu wanofika mbali ni wale wanaotambua kuwa kupoteza muda wao ni zaidi ya kupoteza pesa zao;kupoteza muda wao ni kupoteza hatima yao(future).Kiufupi ni kuwa kila mtu unayempa muda wako ni sawa na kumpa sehemu ya maisha yako.

Unapotumia muda wako kufanya jambo fulani ni kusema kuwa jambo hilo umelipa sehemu ya maisha yako.Je,thamani ya maisha yako inalingana na kitu/jambo/mtu unayempa muda wako?.

Hivi unajua kama unatumia masaa 2 kuangalia movie/tamthilia/muziki kwa siku,masaa hayo ukijumlisha ni sawa na siku 30 kwa mwaka mzima.Maana yake umetumia mwezi mzima kutumbulia macho waigizaji wanaoingiza pesa kukutumia wewe.Ingekuwaje ungetumia muda huo kufanya kozi za mtandaoni ama kusoma kitabu?Kumbuka kuwa “You have no right to entertain yourself unless you have achieved something”..ENTERTAINMENT SHOULD BE A REWARD FOR YOUR ACHIEVEMENT.

Sifa kubwa ya watu wanaofika mbali ni kuwa wanakuwa “wakatili” kwa muda wao;hawako tayari kupoteza muda wao kwa mambo yasiyochangia katika hatima(destiny) yao.Wanakuwa wajasiri kusema hapana kwa mambo ambayo wanaona kabisa hawako tayari kuyafanya ama kutumia muda wao kwa hayo.
Kinyume chake watu wanaokwama ni wale ambao wanatumia muda wao hovyo;wako tayari kughairisha mambo yao muhimu ili wawaridhishe wengine,wako tayari kuvumilia kupotezewa muda na wengine.Hata ukiwapigia simu asubuhi hii ukawaambia wakusindikize mahali,watakublai.Kiufupi hawajui thamani ya muda wao na hawana ratiba ya siku yao.

Fanya maamuzi thabiti ya kuwa “mkatili” kwa muda wako kuanzia leo.Kama unataka kufika mbali Maishani,Thamini muda wako Zaidi ya unavyothamini Pesa Zako.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website