Navigate / search

Jinsi Ya Kutumia Mbinu ya Commitment Device Ili Kuishinda Tabia Ya Kughairisha Mambo

Moja ya changamoto kubwa sana ambayo lazima uijengee uwezo wa kuishinda katika maisha yako ni tabia ya kughairisha mambo.Tabia hi imewasababisha watu wengi sana washindwe kufikia kiwango kikubwa cha matokeo ya yale wanayofanya kwa sababu kila wakati wamekuwa wanaghairisha mambo muhimu kwenye maisha yao na matokeo yake wanajikuta wanajirundikia mambo mengi sana na huyafanya kwa presha kubwa wakati muda wa mwisho umeshafika(Deadline).


Je wewe umeshawahi kuathirika na tabia ya kughairisha mambo?Imeshawahi kutokea fulani siku yoyote katika maisha yako uliwahi kughairisha jambo fulani bila sababu za msingi na ukajikuta siku za mwisho umekosa fursa au umefanya kwa pupa na matokeo yake ukafanya vibaya?Kuna watu wengi sana ambao wanafanya kwa tabia hii na wanajikuta wamekosa kazi wanayotaka,wameshindwa kupata tenda wanazotafuta na hata wengine wamepoteza nafasi za kupandishwa cheo kwa sababu tabia ya kughairisha mambo imewaathiri.
Mwandishi mkubwa sana wa vitabu Victor Hugo aliwahi kukutana na changamoto ya kumaliza kitabu chake mwaka 1830.Miezi 12 kabla ya mwaka huu mwandishi huyu aliweka mkataba na wachapishaji kuwa ataweza kuandika kitabu kipya chenye jina la “The Hunchback of Notre Dame”.
Kama ilivyokuwa kawaida ya watu wengi wanapoona kuwa “deadline” iko mbali huwa wanarelax,vivyo hivyo na yeye aliamua kuendelea na kufanya mambo mengine kwa kuamini kuwa miezi 12 ni mingi sana hivyo anaweza kufanya mambo mengine kwanza kisha badaye atarudi kuanza kuandika kitabu chake.Kadiri siku ambavyo zilikuwa zinakwenda ndivyo ambavyo kampuni ya uchapishaji ilivyokuwa inazidi kukasirika kwa tabia ya Hugo kwani alikuwa hajaandika chochote.Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya na siku zinasogea,Kampuni ya uchapishaji ilimtaka Hugo awe amemaliza kitabu ama wasitishe mkataba.

Baada ya mambo kuendelea kuwa magumu ndipo Hugo alipokuja na mkakati aliouita “Commitment Device” ili aweze kukamilisha kazi yake kwa wakati.Kwanza alijiuliza kwa nini huwa anagharisha mambo kila wakati?Na jibu alilopata ni kuwa ni kwa sababu huwa anapenda sana kutembea kama sehemu ya mambo yanayomfurahisha.

Hatua ya pili aliyochukua ni kuchukua nguo zake zote nzuri anazozipenda ambazo huwa anazivaa kwenye matembezi na akazipeleka kwenye mji mwingine tofauti na akaagiza zifungiwe huko na akabaki na nguo moja tu.

Hatua ya tatu akaanza zoezi la kuandika mara moja.Kila wakati alipopata kishawishi cha kuondoka kwenda kutembea kikwazo cha kwanza kilikuwa ni nguo na alikuwa hawezi kuanza kusubiria hadi aagize zifike,hivyo aliendelea kuandika.Baada ya siku chache akawa tayari amepata mzuka mkubwa sana wa kuendelea kuandika na akawa haghairishi tena.

Cha ajabu ni kuwa mkakati huu uliweza kufanya kazi kwani ulimpatia muda wa kusoma na kuandika kila siku na akafanikiwa kuchapisha kazi yake wiki mbili kabla ya siku ya mwisho iliyotakiwa.Mkakati huu ndio unaitwa “Commitment Device
“.Mbinu hii unaweza kuitumia na wewe pia.

Kwanza angalia ni mambo gani ambayo huwa yanakusababisha uwe unagharisha mambo.Pili tengeneza mkakati wa kuyaepuka ama kutokuwa karibu nayo na ujizuie na kila kishawsihi ambacho huwa kinakupelekea kufanya mambo yanayokusababisha kughairisha mambo.

Inawezekana ikakulazimu kuacha kulipia king’amuzi chako kwa muda ili ujenge tabia mpya,inaweza ikawa kuondoka baadhi ya application kwenye simu yako ama inawezekana ikawa ni kuwakimbia baadhi ya watu kwenye maisha yako.Je wewe katika wiki hii utaanza kutumia commitment device gani ili usighairishe mambo?

Ukifanikiwa,naomba unipe taarifa pia.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website