Navigate / search

Jinsi ya Kupata Kila Unachotaka Maishani

6_mohammed

Taasisi ya afya ya nchini Scotland ilifanya utafiti kwa miaka kumi(10) na kugundua kuwa watu wanaokufa kwa sababu ya magonjwa ya moyo jumatatu asubuhi ni wengi kwa silimia ishirini(20%) ukilinganisha na siku nyingine za wiki.

Pamoja na kuwa na sabbu nyingi sana kwa jambo hili,ila sababu mojawapo ni kuwa jumatatu asubuhi ni siku mbaya ya wiki kwa watu wengi sana duniani.Watu wengi huamka na kujikuta wanalazimika kwenda kufanya kazi ambazo hawazipendi,sio ndoto zao na kama wangepewa fursa ya kufanya kitu kingine basi wangeacha kazi hizo.

Wengi wanagundua wanalazimika kurudi katika ofisi zilezile wanazozichukia,watakutana na watu walewale ambao wasingependa kuwaona na wataendelea kulipwa mshahara kiasi kilekile ambacho wanaona ni chini ya kiwango chao na huku wakikumbuka madeni wanayotakiwa kulipa na majukumu ya kifedha yanayowakabili.Katika hali kama hizi wengi huanza siku ya jumatatu asubuhi kwa majonzi na kukosa furaha na mawazo huwa mengi hadi wanapata msongo na kupelekea matatizo ya moyo.

Jambo la kutambua ni kuwa hali yako haitabadilika hadi ufanye mambo haya mawili(2):

1)Amua kuamini kwamba inawezekana kubadilisha hali yako ya sasa.

Watu wengi ukiwauliza kwa nini wanaendelea na hali ambazo hawazipendi watakuambia ni kwa sababu hawana fursa nyingine yoyote ama hawana pesa.Lakini nilichokuja kugundua ni kuwa wengi bado hawajakata shauri kwa dhati ndani ya mioyo yao kuwa wanataka mabadiliko ya kweli;wengi ukiongea nao ni kama vile wamekubaliana na hali hiyo na wameamini kuwa hawana cha kufanya.Ukiamini hivyo basi hali yako haitabadilika.

Law of attraction(kanuni ya kuvuta vitu) inasema unavutia kwako watu,rasilimali na fursa zile ambazo unaziamini na unaziwaza ndani yako kila wakati.Kuanzia leo usiamini katika kutokuwezekana,panga mikakati yako,amua kubadilisha usichokipenda na anza kuchukua hatua.

2)Chukua hatua ya mabadiliko bila kujali utafeli mara ngapi

Unatafuta kazi,usiapply mara mbili tu usipopata unakata tamaa.Unatafuta mkopo,usiende benki moja tu au kwa mtu mmoja tu eti akikataa basi unasema haiwezekanim,umefeli mara moja unasema sitafaulu tena wakati jack ma alifeli chuo mara tatu na leo ni bilonea.Jaribu mara nyingi uwezavyo ili kujitengenezea uwezekano mkubwa Zaidi.

Watu wanaofanikiwa ni wale ambao kila wakiambiwa haiwezekani wanatafuta njia nyingine ya kufanya iwezekane.Umeshawahi kumuona mwanaume amempenda mwanamke kwa dhati?Hata akiambiwa NO mara kumi atatafuta mbinu nyingine.Mara ataleta mau,mara zawadi ya simu,mara atajenga urafiki na rafiki wa karibu wa huyo mdada,mara atatuma meseji kutwa mara saba…Ili mradi tu apate namna ya kukubaliwa.Upendo wa kweli hauruhusu kukataliwa mara moja kukukoshe mke.

Kwenye kufanikisha ndoto zako ni vivyo hivyo;usikubali kukataliwa kwako mara moja kukukoseshe kutimiza ndoto yako uipendayo.
NDOTO YAKO INAWEZEKANA,LEO JARIBU TENA KILE KILICHOSHINDIKANA HUKO NYUMA.

See You At The Top.

Endelea kutembelea ukurasa wangu wa facebook kujifunza zaidi

Comments

Iddy Malinda
Reply

kaka unatoa elimu

Leave a comment

name*

email* (not published)

website