Navigate / search

Jinsi ya Kuongeza Ufanisi na Kufanikiwa kwa kila Unachofanya

article-2474991-18F526AB00000578-563_634x432

Kutokana na ukuaji wa teknolojia na mitandao ya kijamii(social media) kuwa mingi,mara nyingi tunajikuta tunashindwa kufanya mambo ya muhimu kwa umakini wote(divertion of focus).Kwa wastani mtu wa kawaida kwa sasa yuko kwenye mitandao ya kijamii isiypongua mitatu na kwa utafiti mdogo watu hutumia kwa wastani hadi masaa matatu kuperuzi mitandao ya kijamii kwa siku.

katika kanuni za ufanisi kuna kanuni inaitwa-“Single undertaking”;Hii maana yake ni kuamua kufanya jambo moja kwa kuweka umakini wako wote hadi unamaliza bila kuacha.Faida yake ni kuwa kadri unapoendelea kufanya unapunguza muda wa wa kulifanya kwa sababu unafaidika na “learning curve”(uzoefu unaoupata kwa kuendelea kufanya bila kukatisha).

Kila unapofanya jambo na kuliachia njiani unaporudi ulifanya unakuwa unatumia nguvu kubwa zaidi na unakuwa umepoteza faida ya learning curve uliyoanza kuipata.Pia tafiti zinaonyesha kuwa itachukua si chini ya dakika 25 kwa ubongo wako kurudia katika hali ya kawaida ya kufanya lile jambo ulilokuwa umeliacha.

Mara nyingi unakuta ni mitandao ya kijamii ndiyo inatulazimisha kukatisha:Ukisikia watsapp imeingia,au favorited twitt ambayo umeweka alarm,wakati mwingine ni mazoea tu ya kushika simu kila wakati bila hata sababu za msingi.

Leo,jaribu kujizuia na anza kujenga tabia ya kufanya jambo moja bila kukatisha.Pia anza kufanya mazoezi ya kutoperuzi mitandao ya jamii bila lengo mahsusi.Kama unahisi umeshakuwa mlevi(addicted) na mitandao ya kijamii,

Leo anza kwa kuamua kukaa lisaa lizima bila kuperuzi ili ufanye jambo la muhimu na kufaidika na kanuni ya SIngle taking.Kama utafanikiwa naomba unitaarrifu na uweke email yako hapa chini nitakutumia zawadi nzuri sana.
Nakutakia Wiki ya Mafanikio….!!!

Comments

Sonelo
Reply

Mungu akubariki mtumishi, kwa ujumbe huu!!!

nanauka
Reply

Ahsante sana,Amina

Maweza Rashid
Reply

Noted

Maweza Rashid
Reply

Inawezekana tu kubadilika kwasababu mambo mengi kadri unavyojizoesha ndivyo tatzo lunavyozd kuongezeka na kutengeneza usugu kwenye ubongo wa mwanadam ,Leo umenipa ukumbusho ulio mwema
Ahsante sana
Ubarikiwe.

nanauka
Reply

Ahsante sana Maweza,Tuendelee Kujifunza ili tutimize ndoto zetu.

Maweza Rashid
Reply

Inawezekana tu kubadilika kwasababu mambo mengi kadri unavyojizoesha ndivyo tatzo linavyozd kuongezeka na kutengeneza usugu kwenye ubongo wa mwanadam ,Leo umenipa ukumbusho ulio mwema
Ahsante sana
Ubarikiwe.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website