Navigate / search

Jinsi Ya Kuongeza Fursa Za Mafanikio Kila Siku

1483155_1217358591626817_9018011250599828966_n

Mojawapo ya kitu kikubwa sana nilichojifunza kuhusiana na fursa za mafanikio maishani ni kitu ninachokiita(referability index),ule uwezo wako wa kuaminiwa hadi kiwango cha kupendekezwa na mtu mwingine.Ukweli ni kuwa fursa si kitu kilichoko hewani bali fursa zipo katika mikono na mitandao ya watu wengine unaowafahamu na wengine usiowafahamu.

Mara nyingi watu huulizwa kama wanaweza kutafuta mtu wa kufanya kitu Fulani(wanataja sifa),ukweli ni kuwa kazi hii huwa ngumu sana hasa kwa kuzingatia kuwa kila unayempendekeza anabeba jina lako,na akiboronga nawe utaonekana haufai ila akifanya vizuri nawe utaonekana unafaa.Hii ndio sababu watu wengi hata makazini wakiambiwa kuna fursa, huogopa moja kwa moja kupendekeza mtu kwani inaathiri katika sifa yao pia(reputation).

Hivi haujawahi kusikia watu wanatafuta MC wa harusi na mtu anatajwa kisha kila mtu anasema,”huyo hapana kabisa”,au fundi gari anasifika kwa wizi wa vifaa na kila anayetaka kupeleka gari kwake anaambiwa sifa zake mbaya,ama mfanyabishara ukishamtumia pesa ni msumbufu kupindukia au mtu ni mchonganishi kwa wafanyaki wenzake?

Lakini pamoja na hayo yote,wapo watu wengi ambao hata wewe ukiambiwa uwapendekeze,huwezi kuwaza mara mbili mbli kwani ni watu unawaamini sana katika maisha yako.Leo ningependa uzifahamu sifa mbili za kujijengea maishani ili uwe mtu ambaye jina lako litakuwa la kuaminika na kutajwa haraka kila fursa inayokuhusu inapotokea.

1)Uwe Mkweli na Mwaminifu

Hakuna kitu cha hatari kama kukosa uaminifu katika majukumu unayopewa,na hasa katika eneo la pesa.Kama wewe ni mtu ambaye huwezi kuaminiwa katika eneo hili safari yako ya kuelekea mafanikio itakuwa ngumu sana.Kama kila wakati unajiunga na wenzako kutafuta mbinu za kuiibia ofisi pesa kupitia udanganyifu wa aina mbalimbali au unatapeli watu kwa kutumia bidhaa unazouza ama unakopa na kulipa ni hadi usumbue waliokukopesha basi uwe na uhakika hakuna atakayetaja jina lako fursa kubwa itakapokuja.

Unatakiwa uzoee kusema ukweli kuliko uongo;usidanganye umechelewa kwenye foleni wakati unajua ulichelewa kutoka nyumbani-wengine wanaokuuliza wanakuona ila hawatakuambia kamwe kuwa wanakuona ila hawatakutaja jina lako kwenye fursa nyingine.Ni bora kuwa mkweli na mwaminifu kuliko kuwa muongo na ukaziba fursa zako za mbeleni.

2)Kila unachofanya fanya kwa ubora wa hali ya juu.

Bila kujali kama unalipwa ama haulipwi,bila kujali kama unalipwa kiwango kidogo na kile unachotarajia ama la.Cha muhimu ni kuwa kama umeamua kufanya jambo lolote maishani mwako basi lifanye kwa bidii zote bila ulegevu na ulifanye kwa ubora.

Kanuni itakayokusaidia maishani ni kujiuliza swali hili:Kama ningeambiwa napewa pesa kiwango cha juu kabisa ninachotaka kwa masharti ya kuifanya kazi hii,je ningeifanya hivi nilivyofanya?Kama jibu ni hapana basi ujue unazuia fursa zako zinazofuata.Usifanye jambo kwa kunagalia kile unachopata leo bali kwa kuangalia ni fursa gani uanweza kuzifungua kesho.

Bila kujali kwa leo uko katika nafasi gani na unafanya shughuli gani,fanya jambo ambalo utaongeza uwezo wako wa kuaminiwa na kutajwa kwa jina lako katika fursa zinazokuja mbele yako.Kamilisha kazi ya watu uliyopewa,peleka bidhaa ambayo ilishalipiwa,usichelewe appointment makusudi ukasingizia foleni,pancha ma kuuguliwa,ahidi mambo ambayo uan niaya dhati kuafanya na si kufurahisha watu kisha haufanyi.

Kumbuka kuwa SIFA MBAYA husambaa kwa kasi sana Kuliko SIFA NZURI,Hivyo ziepuke kabisa ili kuifikia ndoto yako.

Endelea Kuitembelea Ukurasa wangu wa Facebook ili Kujifunza Zaidi.

Ndoto Yako Inawezekana,

See You At The Top.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website