Navigate / search

Jinsi ya Kujiongezea Thamani Na Kujitofautisha

render of a man with magnifying glass and the text value

Hivi umeshawahi kujiuliza ni jambo gani haswaa unalohitaji kulifanya ili ufanikiwe?Mara nyingi mafanikio yanapotajwa,basi kila mtu huwa anawaza na kufikiria kwa namna tofauti.Ni vyema kujua kuwa ingwa ziko kanuni nyingi za mafanikio ila kuna kitu kimoja ambacho ni lazima uamue mara tu unapoamua kuanza safari ya mafanikio.Kila ambaye unamuona amefanikiwa katika maisha yake kwenye chochote kile ambacho anakifanya sasa,basi ni lazima alizingatia hili tokea mwanzoni sana.
Na wewe leo nataka ulifahamu jambo hili na uamue kuanza kuliishi katika maisha yako kwa bidii zote-Chagua unachotaka kukifanya na ukifanye kwa ubora wa hali ya juu sana kuliko kawaida.
Hii ndio hatua ya kwanza kabisa unayohiitaji katika maisha yako.Ni lazima kwanza uamue jambo ambalo unataka kulifanya kwenye maisha yako.Labda nikuulize jambo.Hivi wewe unataka kuwa nani hapo baadaye?Swali hili linaweza kuonekana kuwa ni rahisi sana ila ukweli ni kuwa ni gumu sana kwa watu wengi.Kuna watu wengi sana wako bize na maisha yao ila hawajui haswaa wanaelekea wapi.Na kwa sababu hiyo huwa wanajikuta kila mwaka wako palepale na hakuna mabadiliko yoyote yale ambayo wanayapata katika maisha yao.
Hebu tulia kidogo kabla haujaendelea kusoma makala hii na ujiulize-Kama ukiendelea kuishi uanvyoishi sasa na ukiendelea kufanya unachofanya kwa sasa utafika unakotaka kwenda?Kama jibu lako ni hapana basi ujue ni wakati wa kubadilisha mwelekeo na kama jibu lako ni ndio basi endelea hivyohivyo.Watu wengi sana inapofikia kujiuliza swali hili,ni aidha huwa hawataki kabisa kujiuliza ama huwa wanajipa majibu ya uongo.Sijajua wewe uko kundi gani,ila ningetamani sana ujiulize maswali haya na upate majibu yake leo bila kuchelewa.
Baada ya kuamua jambo ambalo unalitafuta katika maisha yako,hatua inayofuata ni kuamua kulifanya jambo hilo kwa ubora wa zaidi ya kawaida.Kumbuka kuwa kwa chochote ambacho utakuwa umeamua kukifanya katika maisha yako basi kuna watu wengine wengi wanafanya kama kitu hicho hicho ambacho unakifanya.Swali kubwa kwako ni kuwa-Ni kwa nini wewe ulipwe zaidi?au kwa nini watu waache wengine na waje kwako wewe?
Duniani kote hakuna mtu ambaye anapenda vitu vya kawaida ama vitu vya wastani.kila mtu huwa anapenda vitu vya tofauti sana.Hata wewe ukinunua nguo ama chochote kile unapenda kiwe tofauti.Hii inamaanisha kadiri kitu kinavyokuwa tofauti ndivyo ambavyo na wewe utazidi kupandisha thamani yako.
Njia nzuri ya kuhakikisha kuwa katika chochote ambacho uanfanya kinavutia watu wengi zaidi na kinavutia thamani kubwa zaidi ni kuhakikisha kuwa unafanya kwa ubora ulipitiliza.Yaani kila mtu ajue kuwa wewe uko juu kwa ubora wa kile unachokifanya kuliko mtu mwingine.Ukienda sehemu zenye maduka,unaweza kukuta kuna maduka mengi sana yanauza bidhaa zinafanana ila kuna mmoja anauza zaidi ya wengine kwa sababu kuna kitu cha utofauti na wale wengine.Vivyo hivyo ili na wewe uvutie watu wengi na thamani kubwa zaidi,basi itakubidi ufanye kwa ubora sana.
Kuanzia leo amua kufanya kwa ubora uliopitiliza kiasi ambacho kila mtu atajua kuwa wewe ndio mtu sahihikila wakati inapohitajika bidhaa/huduma unayotoa hata kama kuna wengine wanafanya kama wewe.
Amua kuwa bora kuliko kawaida na utapata matokeo yasiyo ya kawaida.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website