Navigate / search

Jinsi Ya Kujenga Ujasiri Kwenye Kila Unalofanya

Uwezo wako wa kujiamini na kuwa jasiri kufanya kile ambacho unataka ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa unafanikiwa katika malengo uliyonayo.Kuna watu wengi sana ambao wamepoteza fursa kubwa sana katika maisha kwa sababu walikosa ujasiri,
kuna watu ambao walishindwa kujielezea ili wapate wanachotaka kwa kukosa ujasiri,kuna watu ambao wameshindwa kuanza kufanya kitu wanachokitamani kwa kukosa ujasiri,kuna watu ambao wamefeli usahili wa kazi kwa kukosa ujasiri,kuna watu wameogopa kufanya maamuzi muhimu kwenye maisha yao na matokeo yake wamedumaa mahali pamoja na wanaishi kwa “stress” za hali ya juu kwa sababu ya kukosa ujasiri wa kufanya maamuzi.

Sifa mojawapo ya watu ambao wanafika mbali sana ni wajasiri katika yale ambayo wamekusudia kuyafanya.Huwa wanapoamua kufanya kitu wanachukua hatua bila kuogopa.Kuna watu wengi sana kwa kukosa ujasiri wamejikuta wamekubali kujiingiza
katika “Commitments” ambazo  hawakuwa tayari kuzitekeleza ila kwa sababu ya hofu na uoga wakajiingiza.Kuna watu ambao wamesema ndiyo katika mambo ambayo walikuwa wanatamani kusema hapana na baadaye wakajikuta katika matatizo makubwa sana.Leo nataka ufahamu mambo kadhaa kuhusu hofu katika maisha yako:

Kwanza ni kujua kuwa kila mtu unayemuona ni jasiri katika jambo fulani kwenye maisha yake,kuna siku aliwahi kupata hofu ya jambo hilo.Kila unayemuona leo anasimama mbele za watu na anaongea kwa ujasiri kuna siku alikuwa muoga na alipoitwa mbele za watu pengine alitokwa na jasho jingi kwa uoga.Kila unayemuona huwa akitaka kitu haogopi kupiga simu kwa mtu yeyote ama kujaribu kitu chochote kuna siku aliwahi kuwa muoga.Hii inamaansiha kuwa ujasiri unajengwa na wewe mwenyewe na hauwezi kujitokeza wenyewe tu.Hivyo kama kuna mambo katika maisha yako ambayo umekuwa ni muoga basi kuanzia leo unatakiwa kufahamu kuwa na wewe unaweza kuwa jasiri kama hawa wengine walivyoweza kuwa majasiri.

Hatua ya pili ni kuchambua na kujua kila eneo la maisha yako ambalo unakosa ujasiri na sababu nyuma yake.Kila mtu ni jasiri katika jambo fulani na pia anakosa ujasiri katika jambo lingine.Mwingine ni jasiri wa kuongea na watu ila sio jasiri wa kusimamia kile kitu ambacho anakiamini;mtu akitokea kidogo tu basi huwa anayumbishwa kirahisi sana.Kwa sasa nataka ujiulize-“Hivi mimi sina ujasiri katika mambo gani”.Kumbuka kuwa kila kukosa ujasiri huwa kunajengwa na kitu fulani,unatakiwa ujiulize na ujue kitu ambacho kimekukosesha ujasiri katika eneo husika.Kuna wengine wamekosa ujasiri kwa sababu wazazi wao waliwaambia wao si kitu,kuna wengine walikosa ujasiri kwa sababu walimu wao waliawaambia hawataweza,kuna wengine bosi wao aliwaambia hawatafika mbali na hawako “Smart”-Maneno kama haya yanatosha kabisa kumfanya mtu aanze kutokujiamini katika maisha yake.

Wakati mwingine kukosa ujasiri katika jambo fulani hutokana na kufeli huko nyuma.Kuna watu hawana ujasiri wa biashara kwa sababu walijaribu huko nyuma na wakafeli hivyo hawataki tena,kuna watu walikuwa na mahusiano na wakaumizwa hivyo hawataki tena kujaribu-Je wewe umekosa ujasiri kwa sababu gani?

Hatua ya tatu ni kutengeneza mkakati wa kuanza kujenga ujasiri katika maeneo hayo.Wakati mwingine itatakiwa utafute mtu ambaye ni jasiri katika lile eneo ambalo wewe sio jasiri ili akusaidie kukufundisha mbinu kadhaa,wakati mwingine itatakiwa uongeze maarifa kupitia vitabu ama kusikiliza watu mbalimbali ili wakupe maarifa ya kukujengea ujasiri zaidi n.k. Lakini njia nyingine nzuri ya kupata ujasiri kwenye kile kitu ambacho huwa unakiogopa ni kuanza kukifanya.Mark Twain aliwahi kusema “fanya kile kitu unachokiogopa na hofu itakufa yenyewe”.Usijidanganye kufikiria kuwa kile ambacho hauna ujasiri wa kukifanya kwa sasa kitaondoka tu chenyewe,ni lazima ufanye juhudi kujenga huo ujasiri.

Hatua ya nne ni kujenga ufahamu wako kwa kujiambia maneno(self-talk).Documentary ya Human Brains inasema kuwa kwa kila dakika kila mtu huwa anajiambia maneno 300 hadi 1000.Kikosi maalumu cha kijeshi cha marekani cha majini(NAVY SEALS) huwa wanatumia sana mbinu hii ili kujenga ujasiri wa wanajeshi wao.Pata muda wa kujiambia maneno ili kujenga ujasiri wako-Wakati unaanza itakuwa kama vile haina matokeo,lakini kadiri unavyoendelea kuongea ndivyo utakavyogundua kuwa inakuletea ujasiri zaidi-Pata muda ujiambie-“Mimi ni bora-I am the best”,”Sitaishia njiani”,”Tatizo hili nitalikabili”,”Nitainuka tena”-Kadiri unavyozidi kujiambia ndivyo kadiri utakavyokuwa unazidi kuwa jasiri.

Anza kuchukua hatua hizi leo na utaanza kuona matokeo.

See You At The Top

@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website