Navigate / search

Jinsi ya Kuhakikisha unafanya kitu sahihi kwa wakati sahihi(Law of Timing)

Kwenye maisha yako ni lazima ujifunze kusoma nyakati na majira ya kufanya mambo na kuchukua maamuzi muhimu yanayoweza kukupa mwelekeo mpya wa maisha yako.Watu wengi sana wamekwama kwa sababu wamechelewa kuchukua hatua au wamejikuta wamefanya kitu sahihi kwa muda usio sahihi na matokeo yake hawajapata matokeo ambayo walikuwa wanayatarajia katika maisha yao.

Kwenye mafanikio kuna kitu kinaitwa kanuni ya kujua muda sahihi wa kufanya jambo(Law of Timing).Hii inaeleza kuwa kushindwa kutambua muda sahihi katika maisha nyako wa kufanya jambo Fulani kunaweza kukufanya ushindwe kupiga hatua katika maisha yako kwa muda mrefu bila kwenda unakotaka.Inawezekana wewe ni mmoja wa wale watu ambao kila wakati umekuta unajilaumu kwa kushindwa kupiga hatua kwa wakati na unapochukua maamuzi unakuta umeshachelewa  na hayakupatii matokeo ambayo ulikuwa uanyatarajia.

Mwaka 1976  nchini marekani kulikuwa na mazingira mabaya sana ya kisiasa,hasa baada ya skendo ya rushwa ya watwergate na kushidnwa kwa vita ya Vietman.Katika hsiia za wananchi kulikuwa na msukumo wa kutokuwaamini wanasiasa waliokuwa wanaongoza nchi kwa wakati huo na kulikuwa kuna kelele kila kona kupata mtu ambaye mpya kabisa katika mfumo.

Baada ya kuona mazingira yalivyo na muda ulivykuwa unasukuma hitaji la mtu wa aina Fulani,Jimmy Carter ambaye hadi wakati hup alikuwa hajawahi kushika wadhifa mkubwa wa kitaifa ukiacha kuwa gavana na mjumbe wa congress wa Georgia aliamua kujitosa kugombea kuwa Rais wa marekani.Kwa kuwa alikuwa hajawa maarufu katika siasa za kitaifa,vyombo vya habari na wachambuzi wa mambo ya kisiasa hawakumpa nafasi kabisa na alionekana kama msindikizaji.Ambacho hawakujua ni kuwa ingawa alikuwa hana nguvu za kisiasa lakini alikuwa anawakilisha hitaji la wakati(Kupata mtu ambaye sio sehemu ya mfumo wa serikali ya wakati huo).Kwa mshangao wa wengi Carter aliendelea kupata umaarufu wa kisiasa na tarehe 20 January,1977 aliapishwa rasmi kama Rais wa 39 wa marekani.

Ni jambo gani lilimpa mafanikio Carter?Haikuwa uzoefu ama uwezo wake binafsi tu bali aliweza kujua majira na wakati sahihi wa kufanya jambo sahihi.Kuna  majira sahihi ya wewe kuacha kazi na kuanza biashara yako,kuna majoira sahihi yaw ewe kuanza kilimo,kuna majira sahihi ya wewe kubadilisha kazi unayofanya kwa sasa,kuna majira sahih ya wewe kuingia kwenye mahusiano n.k

Tatizo la watu wengi ni kufanya mambo nje ya majira sahihi na matokeo yake huwa wanajikuta wanafeli kila wakati.Ningependa nikushirikishe njia moja muhimu ya kujua majira yako sahihi ya kufany a jambo Fulani katika maisha yako.

Kila wakati jua kuwa moyo wako uan nguvu sana ya kukushauri kuliko mazingir ayanayokuzunguka.Kopsa kubwa ambalo watu wengi sana wanalifanya wanapotaka kufanya maamuzi muhimu kwenye maisha yao ni kusikiliza zaidi watu wa nje,kuendeshwa na hisia ama kufanya maamuzi kwa presha ya mazingira yaliyopo.Kila wakati ambapo utataka kufanya maamuzi lazima usikilize sauti ya ndani sana ya moyo wako ambayo mara nyingi ni rahisi kuidharau na kuipuuzia.

Hivi haijawahi kukutokea wakati fulani ukasikia moyo umesita kufanya kitu fulani ama kwenda mahali fulani,lakini kwa kuwa kwa nje hakukuwa na dalili yoyote mbaya ukapuuzia na baada ya kuchukua hatua kinyume na ulivyokuwa unashauriwa ukakutana na majanga?Siku zote kumbuka kuwa unayo hisia ya kusoma mazingira ndani yako.Hii ndio maana usikubali hata siku moja kufanya maamuzi kwa presha za watu,kwani utakapokuwa unajutia maamuzi hayo hao wanaokupa presha hata mmoja hatakuwepo kukusaidia.Watu wengi sana leo wanajilaumu kwa kuchukua maamuzi ambayo waliyafanya sio  kwa kupenda bali kwa sababu ya msukumo wa watu.

Hats siku moja usifanye maamuzi muhimu katika maisha yako kwa kusukumwa na watu wanaokuzunguka.Ukiona unasita kufanya jambo moyoni,hata kama hakuna kitu dhahiri cha hatari kinaonekana wakati huo na kila mtu anaona ni jambo sahihi,usikubali.Ukiona kuna maamuzi unataka kuyafanya na moyoni una amani timilifu lakini mazingira hayasapoti wala watu hawasapoti,usiogope kuchukua hatua.Mara nyingi Mungu huzungumza na maisha yetu kupitia viashiria vya ndani ambavyo wengine wanaweza wasivihisi kwa wakati huo.

Siku zote kumbuka kuwa mafanikio yako  hayatokani na uwezo wako wa kufanya mambo sahihi,kuwa na watu sahihi na kuwa na uwezo tu-Bali kufanya jambo kwa wakati sahihi kutakusaidia kuepuka makosa mengi na kukosa fursa nyingi katika maisha yako.

Sifa mojawapo ya watu waliofanikiwa ni utayari wao wa kuona wengine nao wanafanikiwa,naomba ushare ujumbe huu ili uwasidie wengine pia.Inawezekana kuna mtu maisha yake yatabadilika kwa kusoma ujumbe huu leo na wewe utakuwa umetumika kumsaidia.

Usisahau kuagiza kitabu chakio cha TIMIZA MALENGO YAKO(Mbinu 60 zinazotumiwa na watu waliofanikiwa) ili kikupe maarifa zaidi ya kuelekea katika mafanikio yako.

See You At The Top

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website