Navigate / search

Jinsi Waliofanikiwa Wanavyotumia Maneno Kutimiza Malengo

Kwenye tamthilia ya “The Brains” inasema kila mwanadamu wa kawaida huwa anajisemea maneno 300 hadi 1000 kwa dakika moja.Haya ni yale maneno ambay huwa anayasema ndani kwa ndani bila nje kusikika.Maneno haya huwa yanaitwa “Self-Talk” yaani kujisemesha wewe mwenyewe.Katika tafiti mbali mbali zimeonyesha kuwa kial self-Talk ambayo unajifanyia huwa ina uwezo wa kukufanya ufanikiwe kama inakuwa
nzuri ama ina uwezo wa kukufanya ufeli kama inakuwa mbaya.Hivi umeshawahi kujikuta unasema maneno ndani kwa ndani na hadi yanakuletea hisia fulani kwenye maisha yako?
Mara nyingi sana watu wamejikuta wakijisemea maneno ambayo yamewafanya kuendelea kujiona kuwa ni wadhaifu na watu wasioweza chochote kwenye maisha yao kwa sababu ndani yao huwa wanajiambia-“Mimi siwezi”,”Mimi si kitu chochote” n.k Kadiri ambavyo huwa unajiambia maneno ya namna hii basi ndivyo utakavyoedelea kujiona kuwa ni mtu ambaye hauwezi chochote katika maisha yako.
Unachotakiwa kujua ni kuwa hata kama kila mtu aatakuambia unaweza ila kama wewe mwenyewe ndani kwa ndani unajiambia hauwezi basi ujue utabakia ukiwa hauwezi kwelikweli.Hii ndio maani ni muhimu sana kuzingatia kile unachoendelea kujisemesha ndani ya moyo wako hata kama kila mtu huku kwa njue hasikii chochote kile.Hebu jiulize,unapokuwa umebaki peke yako na hauzungumzi na mtu yoyote yule huwa unajisemea maneno gani ndani yako?Kuna njia kadhaa za kuhakikisha kuwa kila wakati kile unachojisemesha kinafanan na kile kitu ambacho unakitaka kwenye maisha yako:
Njia ya kwanza ni kuhakikisha kuwa kila wazo ambalo linakujia kwenye akili yako ambalo haliendani na kile ambacho wewe unakitataka katika maisha yako,unafanya bidii mara moja kubadilisha mwelekeo wa mawazo yako.Hiki si kitu kirahisi ila kinawezekana.Uzuri ni kuwa kila ambapo utaanza kuwaza kinyume na kile unachokiamini ni lazima utajua tu-Unachotakiwa kufanya kila unapoanza kuwaza habari ya kujiona kuwa wewe ni wa kushindwa,kujiona kuwa wewe si mtu muhimu ama jambo baya litatokea basi hapo hapo unatakiwa kujilazimisha kubadilisha mwelekeo wa mawazo yako.Ili kufanikiwa kufanya hili uanweza kuonge kitu fulani kwa sauti,kuimba ama kuanza kusoma.
Hili ni jambo la muhimu sana kulifanya kwani kama hautakuwa mtu ambaye unatawala mawazo yako na unajiruhusu kila wakati kuwaza viut ambavyo vinakufanya ujione kuwa wewe ni mtu ambaye unashindwa kila saa ama wewe ni mtu ambaye hauna uwezo-Mawazo haya huwa yatajitafsiri katika tabia zako,mwenendo wakon na maneno yako ya nje pia.Kitu cha msingi ni kuhakikisha kuwa kila kujisemesha ambako sio sahihi katika maisha yako unakudhibiti haraka sana bila kuchelewa.
Jambo la pili ni kujisemesha kila siku kuhusiana na kule ambako unataka kwenda na vile ambayo unataka vitokee katika maisha yako.Siku zote kumbuka kuwa maneno unayojisemea mwenyewe huwa yana nguvu sana kuliko yale ambayo watu wanakuambia.Watu walifanikiwa wakiwemo washindi wakubwa katika mashindano ya olimpiki duniani huwa wanatumia muda mwingi sana kujisemesha maneno ambayo huwasaidia kujenga ujasiri na kujiamini ili kufanikiwa katika mashindano ambayo wanashindana.
Kuanzia leo jitahidi kila wakati uwe unajisemesha kuhusiana na maisha yako na yale ambayo unataka yatokee bila kuchoka.Jiambie-“Mimi ni bora”,”Hata katika changamoto hii nitashinda pia”,”Sitabakia kuwa chini katika maisha yangu”,”Mimi ni mshindi”,”Sitakufa maskini”
Usiruhusu kuanzia leo kuwa mtu ambaye kila wakati unaruhusu kujisemesha kwa maneno ya ndani mabaya ambayo hukufanya ushindwe kujiamini na kusonga mbele katika maisha.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website