Navigate / search

JINSI NG’OMBE MMOJA ALIVYOMFANYA VICTORIA AWE MILIONEA

OK Dollars dollar

Victoria kisyombe ana shahada ya kwanza ya mambo ya mifugo na pia shahada ya uzamili katika eneo hilohilo pia aliyoipata chuo kikuu cha Einbur,Uingereza.Maisha yake yalikuwa mazuri hadi pale alipofiwa na mume wake na kubakia majane an watoto watatu wa kuwatunza.Kutokana na mila hakuruhusiwa kurithi kitu chochote ambacho walikuwa nacho wakati mume wake akiwa hai hivyo alinyang’anywa kila kitu.Baada ya hapo Victoria alijikuta amebakiwa na ng’ombe mmoja tu aliyekuwa anaitwa Sero.Akiwa na watoto watatu wa kuwatunza Victoria aliamua kumtumia ng’ombe huyu kuendesha maisha yake na kuwahudumia watoto wake.

Alianza kuuza maziwa kwa watu mbalimbali na pesa ambayo aliipata basi aliitumia kuitunza familia na kuendeshea maisha yake.
Kupitia mauzo ya kila siku ya maziwa aliweza kupata pesa za kutunza familia yake lakini pia aliweza kuhifadhi kiasi fulani(savings) ambacho baada ya kuwa kimekua akakitumia kama mtaji wake wa kwanza.Victoria ametambuliwa na ulimwengu kwa jinsi alivyojitoa kubadilisha maisha ya akina mama wa Tanzania.

Taasisi yake ya SELFINA (Sero Lease and Finance Limited) imetambuliwa mara kadhaa kimataifa na kupewa tuzo ya taasisi bora ya ujasiriamali unaonufaisha jamii wa kanda kwa mwaka 2010(Regional Social Entrepreneur of the Year for Africa in 2010) lakini pia ametambuliwa na Benki ya Dunia na World Economic Forum.Kampuni ya Victoria imekuwa msaada mkubwa sana kuwatoa akina mama katika umasikini na takribani akina mama 220,000 wamefaidika na huduma zake.

Wakati akihojiwa na mtandano wa Lioness of Africa,Victoria anasema-“kama naweza kubadilisha maisha ya mtu mmoja hilo linatosha kuleta tofauti kwa sababu nyuma ya mtu huyo mmoja kuna familia,nyuma ya famillia kuna jamii nzima na nyuma ya jamii kuna Taifa la Tanzania”

Maisha ya Victoria yamejaa mafunzo makubwa sana kwa mtu yoyote yule ambaye anataka kufanikiwa kufikia kilele cha ndoto yake:

Kwanza ni kuwa hata baada ya kunyang’anywa kila kitu na kutokea kwa kifo cha mume wake cha ghafla,Victoria hakukata tamaa na kuona kama ndio mwisho wa maisha umefika.Kufiwa na mume,kunyang’anywa kila kitu na kisha kubakiwa na watoto watatu wa kuwatunza kunaweza kumfanya mtu yeyote yule achanganyikiwe katika maisha yake.Lakini pamoja na kujikuta katika hali ya kukatisha tamaa ambayo inaonyesha kama hakuna njia tena ya kufanikiwa,Victoria alikataa kukata tamaa na akaamua kuamini kwamba anaweza kufanikiwa tena katika maisha yake.Kila mmoja wetu huwa anaweza kupitia mazingira kama haya katika maisha yake.

Kuna nyakati ambazo mambo yanaweza kutokea hadi ukafikiria kuwa haitawezekana tena kuinuka ama kufikia malengo uliyojiwekea,unachotakiwa kufanya ni kukataa kukata tamaa katika maisha yako.Bila kujali leo uko katika hali gani ama siku ukikutana na hali hiyo huko mbeleni,amua kuanzaia leo kuwa-Hakuna chochote kile ambacho kitakukatisha tamaa katika maisha yako.

Jambo la pili la kujifunza kutoka kwa Victoria ni kuwa aliponyang’anywa vitu na kujikuta katika hali ngumu alijiuliza swali moja tu-“Kuna kitu gani ambacho ninacho leo,kinaweza kunisaidia?”.Alipojikagua akagundaua amebakiza ng’ombe mmoja tu na akaanza kumtumia huyo kuyajenga maisha yake kwa upya.Ndivyo ilivyo,hata katika wakati mgumu sana mtu anaoupitia lazima kuna kitu ambacho anacho anaweza kuanza kukitumia.Mara nyingi kinaweza kuwa ni kitu ambacho unaweza kukidharau kirahisi sana lakini ndicho kilichobeba mafanikio yako.Ni vizuri hata leo hii ujiulize swali la muhimu katika maisha yako-“Hivi kuna kitu gani kwenye maisha yangu ambacho naweza kukitumia kubadilisha maisha yangu?”.

Watu ambao walimnyang’anya kila kitu wakamwachia ng’ombe ambaye wao waliona hana faida yoyote kumbe ndio alikuwa amebeba hatima (destiny) ya Victoria.Kuna watu wengi wakikuangalia wanakuona hauna kitu kabisa kinachoweza kukufanikisha,hata wewe mwenyewe ukijiangalia unaweza kuona kama hauna kitu kinachoweza kukusaidia lakini ukweli ni kuwa kama ukijikagua hapo ulipo leo,kuna kitu unacho ambacho ukiamua kuanza kukitumia kitakupeleka hatua moja mbele,kuna kitu amabcho uanweza kufanya na inawezekana unakidharau ial ndio kimebeba mafanikio yako.Kazi kubwa uliyonayo ni kukitafuta hadi upate jibu.

Jambo la tatu ni kuwa,baada ya kupitia shida zote hizo za kunyang’anywa mali zake na kujikuta akihangaika.Victoria aliamua kuanza kusaidia akina mama na wajane wengine ambao walikuwa wanapitia shida kama ambazo yeye alizipitia.Kwa kupitia shauku ya kusaidia wengine,Victoria amefanikiwa sana katika kampuni yake.Siku zote kumbuka kuwa mafanikio tunayoyatafuta si kwa ajili yetu wenyewe,kama ndoto yako haihusishi kusaidia wengine basi inaweza kuwa kikwazo kwako kufanikiwa.Katika kila lengo ulilonalo,kila wakati jiulize:Nawezaje kutumia mafanikio yangu kuwasadia wengine kufanikiwa?

Jambo la nne ni kuwa Victoria alitumia kipato kupitia ng’ombe wake kujenga biashara kubwa.Bila kujali alikuwa anapata kipato kiasi gani bado aliweza kuhifadhi kiwango fulani cha pesa.Haijalishi unalipwa mshahara mdogo kiasi gani ama unapata faida ndogo kiasi gani katika biashara yako,jitahidi uwe na uwezo wa kutunza kiasi fulani.Kumbuka kuwa chochote unachofanya sasa hivi inatakiwa kuwa ni mbegu ya kitu kikubwa unachotakiwa kukifanya.

Bado najiuliza wale mashemeji zake na mawifi walioshabikia Victoria kunyang’anywa mali wakimuona leo wanasemaje?Kuna hali unaweza kuipitia katika maisha yako na watu wakawa wanachekelea na kusema kuwa hauwezi kuinuka tena na kufanikiwa.Kama hautakata tamaa,basi uwe na uhakika kuna siku watashangaa jinsi utakavyofanikiwa.

Lakini swali kubwa napenda kukuacha nalo ni-Unamjua ng’ombe wako?Umeshaanza kumtumia?

Kumbuka kutembekea www.JoelNanauka.com ili kujifunza zaidi.
Kumbuka kuwa ndoto yako inawezekana.

See You At The Top.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website