Navigate / search

Jinsi Nchi za Magharibi zinavyoweza kumuweka Rais wanayemtaka

Ouattara-Gbagbo

Mwaka 2011 Alassane Outara mchumi aliyewahi kuwa mkurugenzi msaidizi wa IMF(International Monetary Fund) alitambuliwa rasmi na jumuiya za kimataifa,Umoja wa Mataifa,Umoja wa ulaya na Ufaransa kwa upekee kuwa ndie Rais halali wa Ivory Coast.

Si mara ya kwanza kwa Outara kushika nafasi ya juu nchini Ivory Coast kwani mwaka 1990-1993 aliwahi kuwa waziri mkuu wa Ivory Coast kwa matakwa ya IMF;agizo likiwa ni kuwa anatakiwa awe kwenye nafasi hiyo ili kuleta mabadiliko ya uchumi.Katikati machafuko ya mwaka 2011 Outara alitambuliwa kuwa Rais wa Ivory Coast.Tuangalie jinsi ufaransa walivyoamua nani awe rais wa Ivory Coast na Kwa nini hawakumtaka Bagbo kabisaMoja ya kitu cha kufahamu ni kuwa Ufaransa wana mkataba maalumu na nchi 14 za afrika ambazo wameshawahi kuzitawala zinazotaka pamoja na mambo mengine tenda zote za serikali(public procurement) wapewe wafaransa.Hii inajumuisha kununua kokoa yote wanayozalisha bila kujali kama kuna mahali pengine wanaweza kupata bei nzuri.Mkataba huu uliongezewa nguvu na kuingizwa kipengele cha mafuta wakati Outara akiwa IMF.

Baada ya ugunduzi wa mafuta nchini Ivory Coast,iligundulika futi za ujazo takribani trilioni 50 ambazo nyingi ziko katika kina kirefu.Katika kuangalia namna ya kuchimba;ufaransa wakamkumbusha Bagbo kuwa hawezi kutoa tenda hiyo kwa mwingine yoyote isipokuwa wafaransa.

Rais bagbo aliuita huo ni upuuzi na akatafuta wadau wa bei nzuri makampuni ya china,Rusia na Brazil.Kitendo hichi kiliwakera sana wafaransa na Ikumbukwe kuwa rais wao alishawahi kusema–“Bila makoloni yao ya Afrika,Uchumi wa Ufaransa hauwezi kudumu”-(Chiraq).Pia wafaransa walikereeka zaidi baada ya Rais Bagbo kuongoza kampeni ya kuuza kokoa ya wakulima wa Ivory Coast katika masoko ya dunia kwenye bei nzuri kinyume na mkataba wa wafaransa.

Wafaransa walitafuta kisingizio na waliomba kibali maalumu cha kufanya kazi ya kuleta amani hasa kaskazini mwa Ivory Coast kulikokuwa na machafuko(na ndiko walijaa wafuasi wengi wa Outara).Kibali hiki walikitumia wakati wa machafuko ya uchaguzi kuyapiga majeshi ya serikali hasa katika maeneo strategic na kumdhoofisha Bagbo.Ushahidi wa video ulionyesha jinsi wafaransa walivyokuwa wanaendesha vita usiku dhidi ya serikali ya Bagbo na mchana wanasema ni waasi ndio waiofanya mashambulizi.Vikosi vya Ufaransa chini ya mwamvuli wa UN viliongoza mashambulizi hadi Ikulu ambako Bagbo aikamatwa na kupelekwa mahakama ya uhalifu wa kivita.

Mchunguzi wa kifaransa aliyehatarisha maisha yake;alifichua siri jinsi ambavyo Raia wawili wa Beraluz ambao walikuwa ni marubani wa serikali walivyotumika kwa makusudi kulipua kambi ya ufaransa na kuua wanajeshi tisa ili kupata kisingizio cha kuendesha mashambulizi makali kwa majeshi ya serikali.

Ingawa ni kweli tume ya uchaguzi ilimtangaza Outara mshindi kwa 54%,kwa mujibu wa katiba ni mahakama ya katiba ndiyo yenye mamlaka ya mwisho kutangaza mshindi(nayo ilimtangaza Bagbo mshindi kwa 51%).

Televisheni ya Taifa wakati matangazo yanaendelea ilionyesha jinsi kura nyingi zilivyochakachuliwa hasa maeneo ya kaskazini kwa kuwa na wapiga kura wengi kuliko waliojiandikisha,haya yote jumuiya ya kimataifa iliyapuuzia.Majeshi ya Bukina Faso wakati huo yakiamrishwa na Rais aliyepinduliwa Blaise Compaore yaliingia Ivory Coast kumsaidia Outara(Ikumbukwe kuwa Outara aliwahi kuwa na Uraia wa Bukina Faso na Mzazi wake mmoja ni wa Bukina Faso-na Rais Compaore ndiye alifanikisha kumuua Thomas Sankara ambaye alikuwa hatakiwi na Ufaransa).

Kuna video ilienea sana mtandaoni ikionyesha wazee wawili wanapigwa na kuchomwa moto,hii ilikuwa baada ya kijiji chao kugundulika kuwa walimpigia kura Bagbo.Msimamo ulikuwa hata kama Bagbo atapata kura moja basi kijiji kizima kinachomwa moto.

Pamoja na haya yote bado jumuiya ya kimataifa haijataka kumuwajibisha Outara,na kuthibitisha hilo; mwaka 2012 Ivory Coast na ufaransa walisaini makubaliano mengine na kuendelea kubakiza wanajeshi 1600 ndani ya Ivory Coast.Vifo vya watu 3000 na wakimbizi milioni 2 sio hoja tena kwa ufaransa kwani walichokitaka wamekipata.Familia zilizopotoza ndugu kwa kuchomwa moto na watoto waliobaki yatima kwa wazazi wao kuwawa na wafuasi wa Bagbo sio hoja tena ya wafaransa,walichotaka wamekipata.

Tangu kuondoka kwa Bagbo madarakani ushawishi wa china nchini Ivory Coast(Biashara kati yao ilitoka paundi milioni 50 mwaka 2002 hadi paundi milioni 500 mwaka 2009),umepungua kwa kasi na makampuni ya mafutaya Ufaransa ikiweo TOTAL yameendelea kupewa haki inayolingana na mkataba ambao Bagbo alikuwa anaupinga na kununua kokoa kwa bei ya chini bila kujali kuna wanunuzi wa bei ya juu.Ukweli ni kuwa njia Rais ya kupendwa na kusaidiwa kushika dola na nchi za Magharibi ni kuwa kibaraka wao.

Yako mambo mengi wanayofanya viongozi wa afrika kwa matakwa ya mataifa ya Magharibi.Ukijaribu kuwa kama Lumumba,Thomas Sankara,Sekoe Toure ama Laurent Bagbo wanamtumia mtu ndani ya nchi yako mwenyewe.Ila naamini kuna kizazi kipya kitainuka kuiweka Afrika kuwa na Uhuru wa kwelikweli.Kuelekea uchaguzi mkuu Tanzania 2010,tunamchagua Bagbo ama Outara..Kazi kwetu.

Hii ndiyo Afrika,Hii ndiyo Dunia…Tunahitaji mapinduzi.

 

Joel Arthur Nanauka

 

Comments

mondu andrew
Reply

Kwa tamaa za waafrika in ngumu kupata maendeleo ya kweli mwanamapinduzi yeyote afrika lazima auwawe ,fikra za kweli zinazimwa

Leave a comment

name*

email* (not published)

website