Navigate / search

Jinsi Kanuni Ya Equal Odds Inavyowasaidia Watu Kufanikiwa

Moja ya kanuni muhimu sana katika suala la mafanikio ni kanuni inaitwa “The Rule of equal Odds” ambayo iligunduliwa na mwanasaikolojia maarufu ambaye aliwasoma harvad anayeitwa Keith Simonton.Kanuni hii inasema kuwa chapisho lolote la mwanasayansi ambalo huwa analitoa lina uwezekano wa kufanikiwa sawasawa na chapisho lingine lolote la mwanasayansi mwingine (The average publication of anuy particular scientist does not have any statistically different chance of having more impact than any opther scientist average publication).Kwa maneno mengine hauwezi kujua ni kitu gani ambacho ukikifanya kitakuletea matokeo ambayo unayatarajia.
Hii inamaanisha kuwa yeyote yule ambaye unamuona amefanikiwa katika eneo fulani la maisha yake ni kwa sababu alitumia kanuni hii.Kinachotokea ni kuwa,watu wengi sana huwa tunafahamu habari zao kupitia yale ambayo wamefanikiwa tu na huwa hatujui walijaribu mara ngapi kufanya kitu kama hicho bila kufanikiwa wakati hatuwaoni na hatujui kabisa.Hii ndio maana wanasema “Success is the game of numbers”(Kadiri unavyojaribu mara nyingi ndivyo unavyoongeza uwezekano wako wa kufanikiwa).
Kila aliyefanikiwa kufika juu sana katika maisha yake atakuambia kuwa alishawahi kujaribu kufanya mambo mengi sana na katika hayo kuna jambo moja ambalo alipoligusa ndio likawa ufunguo wa mafanikio yake hadi sasa.Changamoto kubwa ambayo huwafanya watu wasifike wanakotaka ni kwa sababu huwa wanajaribu mara moja na wakishaona wamekwama basi hukata tamaa kabisa na hawaendelei kufanya tena.Kuna mambo kadhaa ya kujua kuhusiana na kanuni ya “Equal Odds”:
Moja ni kuwa kadiri unavyojaribu mara nyingi ndivyo unavyozidi kupata uzoefu wa kile unachokifanya na unazidi kuongeza uwezekano wa kufanikiwa katika kitu hicho.Uzoefu wa kitu unachotaka kukifanya katika maisha yako ni jambo la muhimu sana,hata hivyo uzoefu ambao unaweza kukusaidia sio ule ambao unaambiwa bali ni ule ambao unajifunza kwa kufanya.Kadiri unavyofanya ndivyo utakavyogundua njia bora na rahisi zaidi ya kufanya kwa mara nyingine ili uweze kupata matokeo mazuri.Wewe mwenyewe utakuwa ni shahidi kuwa unapojaribu kufanya kitu fulani kwa mara nyingine basi unajikuta unafanya kwa urahisi zaidi kuliko ilivyokuwa awali.Kumbuka kuwa unapofeli haimaanishi kuwa hauwezi,bali inamaanisha kuwa haujafanya kwa njian sahihi na kama ukijua njia sahihin basi utafanikiwa kama wengine.Leo jaribu kufikiria na kama kulikuwa na kitu ambacho ulikuwa umekiacha kwa sababu ulikuwa umefeli-Ni wakati wa kutumia uzoefu wako kuanza upya kwa namna bora zaidi.
Mbili ni kuwa hakuna mtu anayefanikiwa kwa kufanya mara moja tu.Hili ni jambo la msingi sana la kulifahamu kuhisiana na maisha yako.Tunaishi katika ulimwengu ambao watu wengi sana wameaminishwa kuwa kila kitu kinapatikana haraka-Hii ndio maana kila mtu anayefanya biashara huwa anajikita katika kuonyesha kuwa anaweza kufanya kwa haraka zaidi.Falsafa hii imefanya watu watake kila kitu kwa haraka ikiwemo mafanikio na kutimiza malengo wanayoyataka.Kumbuka kuwa kuna mambo ambayo utayapata kwa haraka ila kuna mambo mengi pia ambayo hautayapata kwa haraka kama unavyotaka.Kanuni ya Equal Odds inakutaka kuwa mtu ambaye utakuwa tayari kujaribu mambo mengi na mara nyingi iwezekanavyo bila kuchoka.Mafanikio yako yamefichwa katika utayari na uwezo wako wa kujaribu mara nyingi kuliko kawaida bila kuchoka na bila kujali kuwa matokeo yanachelewa ama la.
Ukitaka kufaidika na kanuni hii basi ni lazima uamue kuanza kuitumia leo na uanze kuitumia bila kuchoka ili ikupe matokeo ambayo unayataka.Ukianza kuitumia mapema ndivyo utakavyojiongezea uwezekano wako wa mafanikio mapema pia.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website