Navigate / search

Jinsi Che Guevara alivyopita Dar kuelekea DRC

images

Akiwa ametokea Cuba,Che Guevara alikuja na timu ya wapiganaji 120 wote wakiwa weusi wakielekea Congo kupitia Kigoma kumsaidia Kabila aliyekuwa amejiimarisha eneo la mashariki mwa kongo jimbo la Katanga,wakati huo Che Guevara alikuwa na umri wa miaka 35.Alielekea Kigoma na Kisha kuvuka ziwa Tanganyika 24,April msituni walikokuwa wapiganaji wa kabila.

Baada ya Miezi Saba Che Guevara aliamua kuondoka Congo kwa madai kuwa Jeshi la kabila halikuwa na nidhamu,walikuwa waoga na maofisa ndio walikuwa wa kwanza kukimbia wakishambuliwa na watu wao wakijeruhiwa huwaacha bila kuwasaidia.

Pia Laurent Kabila aliyekuwa na miaka 26 wakati huo alikuwa anatumia muda wake mwingi Kigoma na Dar Es Salaam,akiwa mlevi na anayependa wanawake zaidi.

Akasema….“Kabila is a man that Lacks Revolutionary Seriousness”

HIVYO MWEZI NOVEMBER ALIWAONGOZA WAPIGANAJI WAKE KUPITIA KIGOMA,DAR ES SALAAM KURUDI CUBA!!

Leave a comment

name*

email* (not published)

website