Navigate / search

Je,Kuna Siku Itafika Nawe Utatoa Machozi Kama Alix?

alix-idrache-2

Umeshawahi kufanikiwa katika jambo ambalo ulikuwa unaona kama vile haliwezekani?Ama umeshawahi kuvuka kikwazo ambacho kilikuwa kinaonekana kinatishia mafanikio yako ya kesho?Umeshawahi kuwa katika hali inayoonyesha kuwa hautaweza kuinuka tena lakini ghafla unashangaa umefanikiwa kuvuka kikwazo kilichokuwa kinakukabili?

Gazeti la Bussiness insider la tarehe 26,May 2016 liliripoti habari iliyokuwa inasisimua na yenye mafunzo makubwa sana kuhusu mafanikio katika maisha ya kila siku. Second Lt. Alix Schoelcher Idrache hakuwahi kufikiria kuwa kuna siku ambayo ndoto yake ya kumaliza mafunzo ya kijeshi na kufanikiwa kwa kiwango cha juu itatimia.Picha zilisambaa zikimwonyesha akitokwa na machozi wakati wa sherehe za mahafali ya jeshi ya kwenye kiwanja cha Michie Stadium in West Point siku ya May 21.

Alix Idrache sio tu alifanikiwa kumaliza mafunzo yake bali pia alifanikiwa kuwa mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi kwenye somo la physics na kupata fursa ya kuendeleza taaluma yake katika chuo cha jeshi la anga Fort Rucker, Alabama.
Kwa nini habari ya Alix imevutia hisia za dunia?

Moja ni kwa sababu Alix anatoka katika nchi inayofahamika kwa umaskini wa hali ya juu,HAITI.Kila nchi yake inapotajwa watu hufikiri juu ya umaskini uliokithiri na watu waliokosa matumaini katika maisha yao ya kila siku.Ni wazi kuwa watu wengi hupenda kutufanya tuamini kuwa hatutaweza kufanikiwa kwa sababu ya historia ya nchi tunazotoka,makabila ama hata ni eneo gani la nchi unatokea.

Alix hakukubali historia ya mahali anapotokea iwe ni kikwazo cha yeye kufanikiwa kutimiza ndoto yake.Ni mara ngapi umesikia kuwa watu wa nchi fulani ndio wamefanikiwa Zaidi?ama watu wa mkoa fulani huwa ndio matajiri ama hufanya vizuri katika masomo yao kuliko watu wa eneo unalotokea?Hujawahi kusikia kuwa pengine ukoo wenu watu huwa hawamalizi shule?ama wakiolewa lazima waachwe ama huwa hawafanikiwi kifedha?

Kila siku lazima utakutana na historia ya kukatisha tamaa inayoendana na ile ya Alix,lakini ni uchaguzi wako mwenyewe kuiamini historia unayoambiwa ama kuchagua unachotaka kukiamini na kuiishi ndoto yako kwa mafanikio.
Wakati Alix anahojiwa,alisema baba yake alikuwa siku zote anamwambia kuwa elimu ndio zawadi bora Zaidi anayoweza kumpa na kuwa kama akiamua ataweza kufanikiwa.Ingawa walikuwepo watu wengi sana ambao walikuwa wanamwambia kuwa hawezi,yeye alichagua kuamini maneno ya baba yake kuwa anaweza.Kila siku utakutana na watu wanaokuambia maneno mbalimbali lakini wengi wao watakuambia maneno ya kushindwa na sio kushinda.Uamuzi ni wako,unachagua maneno gani?

Unachagua maneno ya wanaosema haiwezekani kujiajiri Tanzania?Unachagua maneno ya wanaosema haiwezekani kuwa tajiri kwa sababu ya elimu yako ndogo?Kumbuka kuna sauti inayokuambia unaweza,na hiyo ndio unatakiwa kuichagua na sio vinginevyo.

Kila mtu ana HAITI yake,lakini ni wajibu wako kutoka kwenye HAITI yako na kuanza Kuiishi NDOTO YAKO.Nakupa ushauri uwe kama Alix aliyeyashinda mazingira ya kila aina na akaweza kuitimiza ndoto yake bila kujali watu walikuwa wanasema nini.NI ZAMU YAKO SASA.

Natamani kukuona siku moja ukitoa machozi kama ALIX utakapokuwa umefika kwenye KILELE CHA NDOTO YAKO,Sio machozi ya huzuni na maumivu bali machozi ya Furaha.Na siku Hiyo ikifika utaniruhusu nikupe picha niiweke Mtandaoni?

Endelea kutembelea www.JoelNanauka.Com

Ndoto Yako Inawezekana,

See You At The Top.

Comments

chisanyo Charles
Reply

Napata nguvu yakuendelea kukabiliana na changamoto.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website