Navigate / search

Je Unaiamini Ndoto Yako Kiasi Gani?

nicks-visiting-his-old-school-in-aus_inside-32ax87mk45ubk8u1iwog7e

Baada ya miaka 50 ya kufanya mafunzo kwa watu elfu ishirini na kufuatilia maendeleo yao katika maisha yao yote,Elmer Letterman alipoulizwa kuhusu kitu kimoja kinachoweza kumfanikisha mtu alisema bila kusita  akasema “intensity of purpose”(Nguvu ya kusudi/Lengo).Hii inamanisha ni uwezo wako wa kuamini kuwa hakuna kitu kinaweza kukuzuia kufikia malengo yako uliyojiwekea,inamaanisha uko tayari kulipa gharama yoyote ilimradi umefanikisha malengo yako.Kuna watu wengi sana ambao nimekutana nao katika maisha yao wana akili,wana fursa,wanafahamiana na watu muhimu,wana elimu n.k lakini kwa sababu tu wamekosa kuwa na malengo thabiti basi wameshindwa kabisa kufikia mafanikio ambayo wengine wanaoonekana kama hawana fursa na uwezo kama wao wamezipata.

Hivi haujawahi kukutana na watu wanaoonekana kuwa wanaakili sana,wanajua mambo mengi na wanafursa ya kufanikiwa lakini kila siku wako palepale,wamedumaa na hawapigi hatua za mafanikio?Siku moja nilisikia mtu mmoja akisema –“There is nothing so annoying like seeing the dumber person than you is more successful than you”-Hakuna kitu kinakera kama unakutana na mtu ambaye anaonekana kama hana akili sana kama wewe lakini amefanikiwa kuliko wewe.

Dunia haiendeshwi kwa fikra zako,dunia inaendeshwa kwa kanuni.Kama vile ambavyo mtu yoyote akipanda juu ya ghorofa na akajiachia ataanguka na nguvu ya uvutano(gravity) haitajali kama ni mtoto,mzungu,maskini ama tajiri-Ndivyo kanuni za mafanikio zilivyo,huwa hazibagui wala hazichagui yeyote ambaye atazizingatia basi anakuwa na fursa ya kufanikiwa.Hivi haujawahi kukutana na watu ambao darasani walikuwa wanaonekana wa kawaida lakini kwenye maisha wamefanikiwa kuliko waliokuwa vipanga?Hivi haujawahi kuwaona watu waliozaliwa familia za kimaskini wamekuwa matajiri kuliko watoto waliozaliwa kwenye familia za kitajiri-Inawezekana na inatokea kila siku.

Elmer alivujisha siri ambayo kila mtu anatakiwa kuijua kama anataka kufanikiwa.Ili uweze kutimiza malengo ya maisha yako ni lazima uwe na “intensity of purpose” ambayo huwa inaonekana kwa kuamini bila shaka kuwa kila lengo ulilonalo katika maisha yako litafanikiwa.Kuna watu wengi sana wana ndoto na wana malengo lakini hawajafikia kiwango cha kuamini kuwa ndoto zao zinawezekana.Ni lazima nguvu inayokusukuma kuamini kuwa utafanikiwa iwe kubwa kuliko nguvu inayokuambia kuwa utafeli.Utajua kama umefikia katika hatua hii pale ambapo kila wakati utakuwa unawaza malengo yako na unatamani kujifunza kila siku kuhusiana na malengo uliyonayo.Kama wewe inaweza kupita siku nzima hauwazi kuhusiana na malengo yako basi ujue bado haujafikia kiwango cha watu wanaofanikiwa.

Kitu kimojawapo kinachowakwamisha watu kukosa msukumo wa nguvu kuelekea katika mafanikio yao ni ile hali ya kujiona kuwa hawastahili kabisa kufanikiwa kwa viwango fulani.Kuna watu wengi sana ambao kwa mdomo watakuambia kuwa wanaamini watafanikiwa ila mioyoni mwao huwa hawaamini kabisa.Na hii ni rahisi kuijua kwa kuangalia aina ya hatua wanazozichukua.Hata wewe unaweza kujichunguza kuanzia leo-Hebu angalia aina ya hatua unazozichukua,zinaendana na ndoto na malengo makubwa unayosema unayo katika maisha yako?

Mara nyingi sana nimewafundisha watu kuwa wanaweza kufanikiwa kwa viwango vya juu sana lakini kila wakati nimekutana na kikwazo cha kuwafanya waamini wanaweza kufanikiwa.Ili ufanikiwe katika malengo yako ni lazima kiwango cha kuamini uwezo wako wa mafanikio kiwe kikubwa kuliko kiwango cha kuamini uwezekano wa kufeli kwako.Na jambo la ajabu katika hili ni kuwa,hakuna mtu anaweza kuamini kwa niaba yako na pia hata kama ulimwengu mzima utaamini kuwa unaweza kama wewe mwenyewe hautaamini basi hautafanikiwa kabisa.

Kitu kingine kinachowakwamisha watu kutofikia hatua ya kuwa na “intensity of purpose” ni ile hali ya kufikiri kuwa kuna watu maalumu(special) ndio wanaoweza kufikia viwango fulani vya mafanikio.Ukweli wa mambo ni kuwa hakuna watu maalumu ila kuna watu wenye ufahamu maalumu unaowafanya waishi tofauti na wengine na hiyo ndiyo huwafanya wapate matokeo tofauti na watu wengine.Watu wengi sana huwa hawaamini kuwa nao wana fursa iliyo sawa na kila mtu mwingine aliyeko duniani.Hupenda kuamini kuwa kuna watu waliopangiwa kufanikiwa na sio wao,na kwa sababu ya imani hii huwa wanaendelea kudumaa palepale walipo kila siku.

Kanuni ya kichocheo na matokeo(Law of Cause and Effects) inasema kwa kila matokeo unayoyaona basi huwa kuna kichocheo/chanzo kilichosababisha matokeo hayo.Hivyo basi kama unataka kupata matokeo fulani kwenye maisha, unachotakiwa kufanya ni kutafuta nini kilifanyika ili matokeo unayoyaona yatokee.Hivyo basi ili kufanikiwa kama wengine walivyofanikiwa ni lazima ufanye yale waliyofanya.Kitu kimoja wapo unachotakiwa kufanya kuanzia leo ni kujenga Imani ndani yako kuwa mafanikio unayotaka kuyapata yanawezekana na kuwa na msukumo wa kila siku kufuatilia mipango yako.Usikubali jambo lolote likuaminishe kuwa hautaweza kufanikiwa,usikubali mtu yoyote yule akuambie kuwa hautaweza kufanikiwa.Yeyote atakayejaribu kukumabia kuwa hautafanikiwa ujue mtu huyo ni MUONGO.Amua kuamini sauti ya ndani yako inayokupa hamasa ya kusonga mbele na usikubali kuamini sauti yoyote ya nje yako ianyosema hautaweza.

Usikubali siku ya leo iishe na haujafanya jambo lolote lile kuhusiana na ndoto yako ama malengo yako ya mwaka huu.Kumbuka na wewe pia unayo nafasi ya kufanikiwa kama wengine na kuitimiza ndoto yako.

Kumbuka kuwa ndoto yako Inawezekana.Share ujumbe huu ili wengine nao wajifunze.

Endelea kutembelea www.JoelNanauka.Com  | www.Mentorship.co.tz ili kujifunza zaidi.

See You At The Top.

©JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website