Navigate / search

Jambo Moja Unalohitaji Kubadilisha Lengo Kuwa Uhalisia

Kila Taifa huwa kuna kitu kinaitwa maono ya Taifa,kila kampuni huwa ina kitu kinaitwa mpango mkakati wa kampuni(strategic plan),hii inamaanisha kuwa hata wewe kama mtu binafsi unatakiwa kuwa na mpango mkakati wa maisha yako.
Mpango mkakati ni nini?-Ni muongozo unaoonyesha maisha yako ya baadaye na mikakati ambayo utaitumia kuweza kufanikisha malengo uliyonayo.Kati ya changamoto ambayo watut wengi sana wanayo katika maisha yao ni kukosa mipango thabiti yua kuwasaidia kutoka hapo walipo kwenda kule wanakotaka.Unachotakiwa kujua ni kuwa hakuna kitu chochote cha maana katika maisha yako ambacho kitatokea kwa bahati mbaya.Ni lazima kuwe na mpango maalumu wa kukifanya kitokee.
Kwa mfano watu wengi sana wanaweza kuwa na malengo makubwa katika maisha yao ila wengi pia huwa hawana mikakati yoyote ya kuweza kutekeleza mikakati hiyo.Kuwa na shauku ya kufanikiwa katika eneo fulani la maisha yako ni jambo moja,ila kuwa na mpango wa namna ya kufanikiwa ni jambo la pili na la muhimu sana katika maisha yako.
Kwa mfano,kama una malengo yoyote yale ya kufanikiwa kifedha ni jambo zuri sana;ila swali loa muhimu ni kuwa:Umeweka mikakati gani kuweza kufanikiwa katika malengo uliyonayo.Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa pembeni ya kila lengo ambaklo unalo kwenye maisha yako unajiuliza,hivi nina mkakati gani wa kutimiza lengo hili?
Kwa mfano unasema;nataka kutengeneza milioni 10 kila mwezi kuanzia itakapofika mwezi wa sita mwaka 2017.Hadi hapa ni hatua nzuri.Sasa hatua inayofuata ni kujiuliza,ninafanyaje ili kuitengeneza hiyo pesa itakapofika huo muda?Kwa mfano uanweza kusema kuwa utaongeza mauzo,utaongeza idadi ya wateja,utatafuta kazi ya ziada n.k
Malengo yoyote ambayo hayana mkikakati basi ujue yatachelewa sana kufanikiwa.Jichunguze usije kuwa mmoja wa wale watu ambao huwa wanaweka malengo mazuri ila huwa hawana mpango mkakati wowote wa kuweza kuwasaidia kutimiza malengo yao.
Leo nataka ufanye zoezi la muhimu kwa kila lengo ulilonalo kujaribu kujiuliza kama una mikakati ya maana ya kufanikisha lengo hilo.Najua katika wengi watakaosoma hii ni wachache sana ndio watafanya hili zozezi,nah ii ndio inakuambia kuwa kutakuwa na wachache sana ambao wataweza kufanikiwa kufika katika kilele cha mafanikio.Je wewe utakuwa tayari leo kuungana na hao wachache ambao watafika kileleni.
Kumbuka kuwa kadiri ambavyo unakuwa na mipango ambayo ni dhahiri sana katika kufikia malengo yako,ndivyo ambavyo na wewe utapata hamasa na uhakika zaidi kuwa malengo yako yatatimia bila shaka.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website