Navigate / search

Jambo la Kwanza Unalotakiwa Kulifanya Ili Ufanikiwe

soldiers

Mwaka 1519 Kapteni wa kikosi cha wapiganaji 500 wa Hispania na meli 11, Hernán Cortés alitua na vikosi vyake katika mji wa Veracruz nchini mexico ili kupigana vita.Akijua fika kabisa kuwa vita ile itakuwa ngumu sana na itahitajika kujitoa kafara ili waweze kushinda,kapteni Cortes alifanya uamuzi wa kipekee sana.Aliamuru ghafla meli zote zilizowaleta wanajeshi wake eneo la vita zichomwe moto na isisalie hata moja.

Wakati moshi unaofuka na meli zinaungua akawaita wanajeshi wake na kuwaambia;Mnaona meli zinavyoungua?Maana yake ni kuwa hatuna option ya kurudi nyuma tuna machaguo mawili tu;Tushinde vita ama tuwe tayari kuuwawa na adui zetu ila hakuna fursa ya kukimbia tukishindwa(We have got no option for retreat,we only have to win or to die in battle field).Matokeo Yako walishinda vita ile.

Falsafa ya namna hii ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku.Wanajeshi walipogundua kuwa hakuna njia nyingine ya kufanikiwa isipokuwa kushinda vita ile,walitumia kila mbinu na kila nguvu waliyonayo ili kushinda.Hiki ndicho kinachotokea mtu anapoamua kufanya jambo Fulani maishani mwake bila kuweka upenyo wa aina yeyote wa kuachia njiani.
Mtu anayeanza biashara yake akiwa ameshachoma “meli” zote za kuajiriwa ataweka nguvu kubwa tofauti na mtu ambaye bado ameegesha meli ya upenyo wa kurudi kwenye ajira mambo yakishindikana,mtu ambaye ameamua kuishi na mwenzi wake na amechoma meli zote za kuachana atafanya juhudi kubwa zaidi ya kutengeneza upatanisho kuliko yule mwenye meli nyingi zinazomsubiri kama mahusiano yake yatafeli.

Kila wakati unapotengeneza fursa ya mahali pa kukimbilia jambo fulani linaposhindikana maishani mwako, kiufupi akili yako itakuwa standby kukimbilia huko na haitafanya juhudi za kutumia ubunifu na nguvu zote ili kushinda changamoto inayokukabili kwa wakati huo.Kuna mambo matatu ya msingi unatakiwa kuyafanya:

Kwanza,kwa kila jambo lenye thamani kwako,usijaribu kutengeneza upenyo wa kukimbilia (escape root) unapoanza kufanya.Hii ni kwa sababu,ubongo wako umeumbwa kutamani kufanya mambo marahisi kila siku na kukimbia mambo magumu.Mara utakapojiwekewa njia rahisi kama alternative,uwe na uhakika hautaweza kufanikiwa katika kile unachofanya kwani kila wakati akili yako itarelax kwa kujua kuna njia mbadala.

Pili,kwa kila jambo muhimu unaloamua kulifanya maishani mwako na kweli unatamani kufanikiwa kwa kiwango cha juu,jiulize-Hivi nimeshazichoma meli zangu?Kama bado ni bora uanze kufanya hivyo mara moja leo.Kama unaamua kufanya jambo la muhimu maishani mwako,usikubali kutengeneza fursa za visingizio vya kushindwa.

Tatu,Kila wakati unapokutana na changamoto maishani mwako katika kuelekea mafanikio yako,usitumie muda wako kutafuta njia za KUZIKIMBIA bali tafuta njia ya KUZITATUA.Usiruhusu akili yako iwe inafanya kazi kutafuta njia mbadala za kukimbia changamoto bali iwe inatafuta njia mbalimbali za kutatua changamoto hizo kila siku.

Watu ambao kila wakati huwa na visingizio vya kwa nini walishindwa kufanikisha jambo fulani maishani mwao,huwa ni watu ambao hawafiki mbali katika safari ya mafanikio yao maishani.

Endelea Kutembelea www.JoelNanauka.Com Kujifunza Zaidi,na kama ujumbe huu umekuwa na manufaa zaidi,unaweza kushare na rafiki zako.Pia unayo fursa ya kujiunga na mtandao wa washindi ili kujifunza zaidi kupitia watsapp group bila gharama yoyote;Tuma neno “NDOTO YANGU”,Ikifuatiwa na jina lako kwenda namba 0655 720 197.

Ili kupata Makala za kila wiki za kujifunza jinsi ya kuifikia ndoto Yako,tafadhali nenda kwenye website yangu na chini upande wa kulia kwenye “weekly newsletter” andika email yako pale kisha itume.
Ndoto Yako Inawezekana,
See You At The Top.

Comments

Sonelo
Reply

Nimeuelewa sana huo ujumbe pastor, thanks a lot!

jacqueline mwasha
Reply

Mungu akubariki pastor ujumbe zako zinanisaidia sana,tena mnoo kila siku zadidi kupambana bila kukata tamaa na kuyumba au kuridi nyuma.zinanifundisha sana barikiwa mnoo.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website