Navigate / search

Intuition-Mbinu Ya Kukusaidia Kufanya Maamuzi Sahihi Kila Wakati

Umeshawahi kufanya uamuzi fulani katika maisha yako halafu baadaye ukajilaumu sana?Je,katika maamuzi ambayo umeshawahi kujilaumu kuna wakati wowote ambapo ulipata mashaka ya kufanya maamuzi hayo na ukasita ila kwa sababu ya mazingira ya nje ambayo yalioonekana kuwa ni mazuri,ama presha kutoka kwa watu ukaamua kuchukua maamuzi tofauti na moyo wako unavyotaka?
Siku zote kumbuka kuwa wewe kama mwanadamu unapata hisia zaidi ya zile ambazo huwa zinatokana na kusikia,kuona,kuhisi na kunusa.Moyo wako una uwezo wa kupata hisia za mambo tofautitofauti na ni lazima uwe na uwezo wa kuzijua hisia hizo na kuzitafsiri ili ufaidike na kazi ambayo inakufanyia.
Kitaalamu hii huwa inaitwa “Intuition”-Yaani kuweza kupata hisia za jambo kutokea ndani yako ambazo mara nyingine zinaweza zisiwe zinakubaliana na mazingir aya nje yako.Wakati mazingira ya nje yanaonyesha kuwa kila kitu kipo sawa ndani yako unaweza kukuta kuwa moyo wako unakukatalia kabisa.Kitu cha pekee kuhusiana na hali hii ni kuwa,wakati inawezekana kila mtu asiwe na uwezo wa kuhisi unachohisi,wewe peke yako ndio utakuwa unapata hisia hizi.Ni lazima ufike kiwango ambacho utaweza kujifunza kusikiliza hisia hizi na kuzifanyia kazi.
Kuna watu ambao tangu siku ya kwanza wanaingia kwenye mahusiano moyo wao ulikuwa unawaambia wasichukue hatua,lakini kwa sababu kwa nje hakukuwa na ushahidi wowote wa ubaya wa huyo mtu wakaamua kutoutii moyo wao kwa sababu hawana ushahidi wa nje.Baada ya muda mfupi wamegundua kuwa kuna mambo mabaya sana ambayo yametokea ambayo kama wangeusikiliza moyo wao,basi leo wasingekuwa wanajutia tena.
Kuna watu walishawahi kupewa dili kubwa la biashara na kwa nje lilionekana zuri sana ila kwa ndani moyo wao ulikuwa unasita kuwekeza pesa zao.Ila kutokana na presha ya marafiki na uchu wa kupata faida kubwa,wakaamua kuingiza pesa zao na leo wanajutia uamuzi wao.
Kuna mtu ambaye alipata kazi nzuri sana kuliko aliyokuwa anafanya,lakini moyo wake ulikuwa unasita sana na alikuwa anasema hivyo kila wakati.Hata hivyo kwa sababu ya kutamani mshahara mkubwa akaamua tu kwenda kwenye kazi mpya.Kilichotokea ni kuwa alijikuta anafaukuzwa kwenye kazi yake mpya baada ya muda mfupi.
Kitu cha muhimu sana kuhusu intuition ni kuwa si lazima ikupe ushahidi wa kile unachohisi ila itakuja na hisia za nguvu sana na utajua kabisa hapa moyo wangu umekataa.Nimeshawahi kusikia watu ambao walighairisha safari zao na baada ya safari kuanza basi walilokuwa wasafiri nalo likapata ajali.
Anza kujifunza kuusikiliza moyo wako kila ambapo unakukataza kufanya jambo fulani,sio kwa uoga bali unapata hisia za nguvu kuwa mambo hayatakuwa sawa.Ukianza kuusikiliza mara ya kwanza utashangaa kesho yake iankuwa rahisi sana kusikiliza na utajiepusha na makosa mengi sana katika maisha yako.
Anza Leo na Utaona Faida Yake.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website