Navigate / search

Ili Uwe Messi Kwenye Field Yako Ni Lazima Umpasie Suarez

150308164807-messi-suarez-shake-hands-super-169

Juzi wakati Barcelona imeishinda Celta Vigo kwa magoli 6 kwa 1,dunia nzima ilishangazwa na jinsi lionel Messi alivyopiga penalti.Badala ya kufunga ili afikishe idadi ya magoli 300 na kuweka rekodi mpya,nyota huyu aliamua atimize ndoto ya mchezaji mwenzake Luis Suarez aliyekuwa na magoli mawili ili amsaidie atomize magoli matatu(Hat Trick).Matokeo yake yamekuwa ni nini?Dunia nzima haizungumzi juu ya Hat Trick ya Suarez,inazungumza jinsi Messi alivyokuwa tayari kutimiza ndoto ya mwenzako hata kama ilikuwa ni fursa kwake pia kutimiza ndoto yake.

Mwanafalfasa maarufu Aristotle alisema asilimia tisini na tano(95%) ya yale yanayotokea katika maisha yetu yanatokana na tabia tulizojenga katika maisha yetu.Hii ndio maana ni muhimu sana kuzingatia tabia gani zinatawala sana katika maisha yetu kwa sababu kwa hizo hupelekea kufanikiwa ama kufeli.
Kati ya tabia muhimu unayohitaji kuwa nayo ni ile ya kutokuwa mchoyo wa wenzako kufanikiwa.Hivi karibuni nilishangaa sana baada ya kuzungumza na mtu mmoja anayefanya biashara fulani ya network marketing baada ya kuniambia kuwa biashara hiyo huko Mkoani kwake ilichelewa kujulikana kwa sababu watu wa kwanza kuingia walikuwa hawapendi watu wengi waijue zaidi ili wasipitwe katika mafanikio.

Hiki ni kiwango cha juu sana cha kutokupenda wenzako wasifanikiwe lakini matokeo yake ni kuwa kwa sababu wengi hawakujiunga ,nao pia walichelewa kufanikiwa ukilinganisha na wenzao wa maeneo mengine waliojiunga muda uliofanana na wao.

Kuna mambo makubwa mawili unatakiwa kufanya kila siku:

1)Kwa kila Fursa Fikiri juu ya Mtu mwingine

Kila siku tunakutana na fursa nyingi sana na kuna zingine pengine hatuzihitaji kabisa lakini wapo watu ambao wanaziota usiku na mchana.Kila fursa unayokutana nayo,jiulize-Je,kuna mtu anaweza kusaidika na fursa hii?Kama jibu ni ndio,basi ingia gharama ya muda na umtafute mtu huyo na kumpa taarifa.Wengi maisha yao yanaweza kubadilika kwa fursa ambazo wewe unaziona hazina maana.Mtumie mtu fursa ya kazi uliyoiona,ama ya biashara ama hata wazo jipya ulilolipata kwa kusoma kitabu ambnalo unafikiri litamsaidia.

2)Fikiria kutoa kwa wengine na sio kupokea tu

Umaskini hutokana na fikra na sio vile tulivyonavyo.Jiulize ,hivi katika maisha yako hauna kitu unachoweza kumsaidia mwingine?Usikae mkao wa kupokea tu kila wakati,jipange na uwe na mawazo ya kutoa kila wakati.Ukifanya hivyo utaongeza nguvu yako ya ubunifu na unatuma maelekezo kwenye sub-concious mind kuwa wewe ni mtu uliyeona tayari hatima yako.Angalia kama kuna nguo unaweza kuwasaidia wenye uhitajai,au viatu ama hata chakula ama pesa pia.

Kumbuka hakuna aliyeng’ara na kufikia ndoto yake duniani kwa kujilimbikizia mwenyewe na kuwa mchoyo.Unataka kung’ara Kama Messi alivyotufundisha leo;kabla haujapiga penalty leo: mtafute Suarez wako umpe pasi ya penalty atimize ndoto yake.

Endeleea kutembelea www.JoelNanauka.Com kujifunza Zaidi.

Comments

Grace J
Reply

Duuuuh!!! I lav it

JAPHETH LUTTASHOBYA
Reply

real pastor,,,,,,, selfish its not a good behavior

Alice M
Reply

Well said Noel

Leave a comment

name*

email* (not published)

website