Navigate / search

Ifahamu Mbinu Moja Inayowasaidia Watu Kufikia Kilele Cha Mafanikio

NBA_Game

Larry bird alijulikana kuwa mchezaji wa kawaida sana katika mpira wa kikapu hadi pale alipoamua kufanya kitu kisicho cha kawaida.Baada ya kujigundua kuwa yeye si mtu mwenye kipaji cha kipekee sana katika mpira wa kikapu,aliamua kufanya kitu cha ziada ili kuhakikikisha ndoto yake inatimia.
Aliamua kuwa kila siku asubuhi kabla hajaenda shule alikuwa anarusha mipira mara mia tano(500) akijaribu kufunga katika mazoezi yake binafsi.Baada ya muda,Larry alijulikana kama ni mchezaji hodari wa mitupo ya mipira(consistent free-throw shooter) na aliisaidia Boston Celtics kushinda taji la dunia mara tatu.Hivi ndivyo nidhamu na juhudi inavyoweza kumfanya mtu kufanikiwa.

Wengi wetu tunafikiri kuwa uwezo na mafanikio ya kipekee huja kwa sababu tuna kipaji Fulani,na hii imesababisha wengi kufikiri kuwa hawawezi kufanikiwa kwa sababu hawana kipaji kabisa.Kuna wengi wenye vipaji ila hawana nidhamu na wameshindwa kufanikiwa,kuna wengi vipaji vyao ni vidogo ila nidhamu yao imewawsaidia kufika mbali.Kuna wengi wenye sauti nzuri ila wamepitwa kwa mafanikio na wenye sauti za sizizo nzuri kama wao ila wana juhudi kubwa kuliko wao.

Mimi si mchambuzi hodari wa masula ya mchezo wa mpira wa miguu,ila katika majadiliano Fulani ya uchambuzi wa uwezo wa wachezaji nilisikia wakisema kuwa messi anang’ara kwa ajili ya Kipaji chake na Ronaldo anang’ara kwa ajili ya juhudi zake.Jambo la Msingi hapa ni kuwa mara unapogundua unapungukiwa uwezo Fulani,fanya juhudi mara mbili kuliko mtu wa kawaida.

Mambo matatu ya kuzingatia katika kujenga uwezo wako:

1)Tambua Uwezo wa Muhimu Unaouhitaji

Hebu jiulize,ni uwezo gani ambao ukiuongeza leo utafanya thamani yako iwe maradufu katika biashara yako,kazini kwako,shuleni etc.Ukishautambua uwezo huo.Anza kuufanyia kazi kila siku,utashangaa baada ya muda umekuwa “master” katika jambo hilo na mafanikio yako yanaanza kuonekana.

2)Usiache hadi umeona matokeo

Kumbuka kuwa uwezo tunaoutafuta hauwezi kujengeka kwa siku moja,ni mchakato wa muda mrefu,usiache kuuongeza uwezo wako hadi utakapoona matokeo ya kile unachokifanya.

3)Usihangaike Kutafuta kukubalika,toa matokeo.

Usiwe mtu wa kuhangaika kutaka kuonyesha na kuonekana kwa kile unachoweza kukifanya.Kubali kutoonekana kwa muda kidogo ili ujenge uwezo wako thabiti na siku ukija kuonekana basi uwezo wako utazungumza kwa niaba yako.

Watu wengi wamekufa wakiwa bado hawajafikia kiwango cha juu cha mafanikio yao kwa sababu hawakuwa tayari kufanya alichofanya Larry.Leo unapoanza siku yako,usikubali kuyumbishwa na jambo lolote,weka mkazo katika kujenga uwezo wako bila kukata tamaa.

Endelea Kutembelea www.JoelNanauka.Com Kujifunza Zaidi,na kama ujumbe huu umekuwa na manufaa zaidi,unaweza kushare na rafiki zako.Pia unayo fursa ya kujiunga na mtandao wa washindi ili kujifunza zaidi kupitia watsapp group bila gharama yoyote;Tuma neon “NDOTO YANGU”,Ikifuatiwa na jina lako kwenda namba 0655 720 197.

Ili kupata Makala za kila wiki za kujifunza jinsi ya kuifikia ndoto Yako,tafadhali nenda kwenye website yangu na chini upande wa kulia kwenye “weekly newsletter” andika email yako pale kisha itume.

Ndoto Yako Inawezekana,
See You At The Top.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website