Navigate / search

Hyvon ametufundisha tufanye nini kufikia kilele cha mafanikio!

hyvon

Hyvon Ngetich(29) aliushangaza ulimwengu na kutoa somo kubwa siku ya jumapili katika mbio za Austin bada ya kuamua kumaliza mbio kwa kutambaa baada ya mfumo wa mwili wake kugoma kabisa kufanya kazi.

Alikuwa anaongoza kwa muda mrefu lakini akiwa namebakiza mita kama hamsini kumaliza alishindwa kuendelea kukimbia.Madaktari walienda kumpa msaada na kumpelekea kiti cha kutembelea “Wheel chair” lakini alikataa na akaamua kutambaa.Alijua kuwa angekubali ingemaanisha amekuwa “disqualified”(angeondolewa mashindanoni).

Alisikika wakati wa mahojiano kuwa alijua kama angekubali kutumia wheel chair asingeshinda mbio hizo na pia volunteer mmoja alisikiaka akimwambia jitahidi uko karibu na kumaliza.

Katika ndoto tulizonazo tunatakiwa kuwa kama Hyvon; tusikubali jambo lolote litufanye tushindwe kuendelea mbele.Tusiruhusu visingizio vya aina yoyote ile vitunyime kufikia kilele cha mafanikio yetu.

Yako machache aliyotusaidia kuyaona kwa vitendo:

-Tusikubali kuruhusu changamoto zitukatishe tamaa
-Tufanye kila tunachoweza kufikia kilele cha ndoto zetu.
-Kuna wakati kukubali msaada ni kuruhusu kushindwa.

Leo–Amua kuishinda kila changamoto ili ufikie kilele cha ndoto yako,INAWEZEKANA.

TUJIFUNZE KWA Hyvon…

Hongera Hyvon!!!

Leave a comment

name*

email* (not published)

website