Navigate / search

Hatua 3 Za Kuwa Mzungumzaji Mzuri Mbele Za Watu

Je ungependa kuwa mzungumazaji mzuri mbeloe ya watu.Kitu cha muhimu uanchotakiwa kufahamu ni kuwa,kuwa mzungumzaji mzuri mbele za watu ni jambo ambalo uanweza kujifunza na ukafanikiwa sana.Ukiendelea kufuatilia makala zangu utapata tangazo la darasa maalumu nitakaloanza kufundisha watu ambao wana kiu sana ya kuwa wazungumzaji wazuri.

Hata hivyo unachotakiwa kujua ni kuwa,kuwa na uwezo wa kuzungumza mbele za watu ni taaluma ambayo unaweza kuijenga kama unavyojena uwezo mwingine wowote ule.Leo ningependa nikushirikishe mambo matatu muhimu ya kukusaidia kuanza kutimiza ndoto yako hii kwa haraka.

Jambo la kwanza ni lazima uwe mtu ambaye kiu yako ni kuona watu wanabadilika ama wanafaidika na kile ambacho unazungumza.Nia kubwa ya kuzungumza mbeke za watu sio kuonyesha uwezo wako wa kujua mambo ama kujaribu kuzungumza mambo mengi sana,bali kusudi kubwa ni kuona watu wanabadilika na kuchukua hatua kutokana na mazungumzo yako uanyoyafanya.

Hivyo,unachgotakiwa kujiuliza ni kuwa-Hivi kweli ndani yangu wito mkubwa nilionao ni kubadilisha maisha ya watu?UKishapata jibu lka swali hili sasa ndio uanweza kujiingiza katika shughuli ya kuzungumza mbele za watu.Kwa ufupi ni kuwa kinachokusukuma kuzungumza hakitakiwi kuwa ni uwezo wako wa uzungumzaji vizuri bali inatakiwa iwe ni shauku ya kuona unachangia mabadiliko makubwa yanayohitajika katika maisha ya wale unaoongea nao.

Jambo la pili,ni lazima utambue ni eneo gani la maisha ambalo wewe una kiu nalo sana na una shauku nalo sana kuona watu wanafanikiwa na wanabadilika katka maisha yao.Kila mzungumzaji uanyemfahamu,lazima ana eneo fulani katika maisha yake ambalo ndio haswaa linamti hamasa na kufanya we na bidii katoka kuzungumza.Huwezi ukawa mzungumzaji wa kila eneo la maisha wakati wote.Inawezekana unao huo uwezo lakini ni lazima uwewe mwenyewe uamua kuwa mzungumzaji unayejikita katika eneo fulani.

Kadiri ambavyo uanjikita katika eneo fulani kwa haraka,ndivyo kadiri ambavyo unajijengea wafuasi wengi kwenye eneo hilo na pia kujenga uwezo mkubwa zaidi katika kuzungumza mbele ya watu.

Jambo la tatu,ni lazima uwekeza katika maarifa.Kumbuka kuwa kila anayekusikiliza anataka kusikia kitu amabcho hakijui-Hii inamaanisha kuzungumza mbeloe ya watu ni eneo ambalo linahitaji mtu ambaye anapenda sana kujisomea kila wakati ili aweze kuwa na maarifa mapya kila wakati.

Kwa eneo lolote ambalo umechagua katika maisha yako kuwa ndio utakuwa unalizungumzia zaidi,ni muhimu kujikita katika kutafuta maarifa ya eneo hilo bila kukata tama.

Katika darasa ambalo nitalianzisha mwezi wa tatu tutajifunza pia namna ya kufanya “corporate presentation” inayovutia ya kibaishara ama kazini kwako.Lakini kama wwewe unataka kwenda kiwango kingine cha mafanikio katika uwezo wa kuzungumza mebloe za watu na namna ya kujiandaa,mbinu na kanuni za kutumia kuzungumza n.k Kama uko dar uanweza kuwahi kujiandikisha mapema kabla darasa halijajaa.Unaweza kutuma meseji kwenda 0655 720 197.Utapewa utaratibu wa kozi itakavyokuwa na malipo kasha utajiunga na wenzako waliokusudia kuufanya mwaka 2017 kuwa mwaka wa matokeo makubwa.

See You At The Top

@JoelNanauka

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website