Navigate / search

Hatua 3 Za kubadilisha KIPAJI Chako Kiwe AJIRA Yako

Jim Carrey alianza kuwa na maisha magumu sana tangu akiwa na umri wa miaka 10.Wakati huu maisha yakiwa ni magumu sana aliamua kuanza kufanya kazi ya masaa manane kwa siku kwenye kiwanda fulani ili aweze kupata pesa kidogo za kumsaidia kutimiza mahitaji yake ya kila siku.Alipofika umri wa miaka 14 baba yake ambaye angalau alikuwa ana kipato kidogo ambacho walipokuwa wanachanganya walikuwa wanapata kiasi fulani,alifukuzwa kazi,na hapa maisha yalizidi kuwa magumu sana katika familia.

Katika hali isiyo ya kawaida na akiwa anahangaika ili kupata msaada anaoutafuta aliamini sana katika kipaji chake na akaamua kutuma CV yake kwenye show ya The Carrol Burnet ili aweze kuchukuliwa kama mchekeshaji.Alipofikisha miaka 15 alifanikiwa kupata fursa ya kufanya onyesho la kwanza la uchekeshaji akivaa suti ambayo mama yake alimshonea.Hata hivyo show hii ilikuwa mbaya sana na hakufanya vizuri kabisa.Mwaka uliofuata akiwa na miaka 16 akaacha shule kabisa na akaamua kuanza kuwa mchekeshaji “full time”.

Baada ya kufanya uamuzi huu aliamua kuhamia Los Angeles kufanya makazi yake,ambapo baada ya kufika huko kila usiku alikuwa anapaki gari yake Mulholland Drive na anajenga picha ya mafanikio katika maisha yake.Siku moja usiku akiwa anaendelea kufikiria juu ya maisha yake na mafanikio yake ya baadaye aliamua kujiandikia hundi ya dola elfu 10 na akaandika jina lake kuwa amelipwa kwa kucheza movie na akaiweka mfukoni  na akaiwekea tarehe ya sikukuu ya shukrani ya marekani ya mwaka 1995 (Thanksgiving day).Cha ajabu kilichotokea ni kwamba kabla ya tarehe hiyo alifanikiwa kuigiza katika movie ya Dumb and Dumber akapata pesa nyingi kuliko hundi ambayo alijiandikia.

Hii ni kanuni ambayo inaweza kumsaidia mtu yoyote yule aweze kupata kitu ambacho anakitaka katika maisha yake.

Kwanza ni lazima uwe mtu ambaye hauko tayari kukatishwa tamaa na hali ngumu yoyote katika maisha yako.Bila kujali kuwa wazazi wake walikuwa maskini na aliishi katika mazingira magumu sana,aliamua kuamini kuwa anaweza kufanikiwa katika maisha yake.Ni lazima ufike sehemu ambayo hata wewe utaamini kuwa unao uwezo wa kubadilisha historia ya maisha yako bila kujali hali yako ya sasa.Inawezekana leo unaishi katika hali ya umaskini sana ama maisha ni magumu,lakini ukiamua kuamini kuwa unaweza basi maisha yako yatabadilika kwa kasi sana.

Jambo la pili la kujifunza ni kuhusu maamuzi.Kuna maamuzi mawili muhimu Jim aliyafanya.Maamuzi ya kwanza yalikuwa ni kuacha shule na maamuzi ya pili yalikuwa ni kuhama mji mwingine.Inawezekana kwa upande wako isiwe maamuzi ya namna hii lakini kwa kila mtu mwenye lengo kubwa katika maisha yake ni lazima afanye maamuzi fulani yasiyo ya kawaida.Inawezekana kwa upande wako ikawa ni maamuzi juu ya kuacha kazi yako ya sasa ili ukafanye nyingine ama ama ukajiajiri,inawezekana ni kuondoka kwenye mahusiano uliyopo kwa sasa,inawezekana ni kubadilisha taaluma yako uanze kitu kipya,inawezekana ikawa ni kuachana na aina fulani ya marafiki,inawezekana ikawa ni kuacha ulevi n.k kwa vyovyote vile lazima kuna maamuzi fulani unatakiwa kuyafanya kuhusiana na hatima yako.Usiogope kuchukua uamuzi muhimu kwenye maisha yako kwani hautaweza kupiga hatua moja mbele bila kufanya maamuzi kuhusiana na maisha yako.Chunguza na uone ni aina gani ya maamuzi unatakiwa kuyafanya kuanzia leo katika maisha yako.

Jambo la tatu ni Kujenga picha kuhusu ndoto na malengo uliyonayo.Kati ya vitu vinawafanya watu wakate tamaa sana ya kufuatilia ndoto zao ni kwa sababu kila wakati huwa wanajenga picha ya kushindwa na wanaona kama vile hawawezi.Watu wanaofanikiwa katika malengo makubwa ni wale ambao huwa kila wakati wanafikiria juu ya hatima yao kubwa na nzuri iliyo mbele yao.Jim aliamua hadi kujiandikia hundi ili kujenga picha ya mafanikio yake katika uigizaji.Kila siku alikuwa anapata muda wa kujenga picha yake ya kesho jinsi ambavyo atakuwa amefanikiwa.Na wewe pia,kila wakati jitahidi kujenga picha nzuri ya kesho yako-Usikubali kuruhusu kujijengea picha za kushindwa kwenye akili yako.Kumbuka kuwa picha unayoijenga leo ndiyo itaamua kesho yako itakuwaje.Usiruhusu kujiona hauwezi ama wewe si kitu wewe ni mtu muhimu na kesho yako ni kubwa sana.

See You At The Top

@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website