Navigate / search

Hatua 3 Muhimu Za Kufanya Wazo Lako La Biashara Kuwa Uhalisia.

Kadiri siku zinavyoenda ndivyo ambavyo utagundua kuwa tofauti kubwa kati ya wanaofanikiwa na wale ambao hawafanikiwi imejificha katika mambo wanayoyafahamu na kanuni wanazozitumia kufanya mambo katika maisha yao.

Mwaka 1966 kijana mmoja ambaye alikuwa na tatizo kubwa la kukumbuka mambo kwa haraka na kushidnwa kusoma kwa ufasaha,ambalo kitaalamu linaitwa (dyslexic) aliamua kuacha shule na kwenda kufanya biashara.Kwa sababu hakuwa na mtaji wa kutosha aliamua kuomba kutumia eneo la kanisa kama sehemu yake ya ofisi wakati anaanza.

Kwa kuwa alikuwa anajua soko la kwanza kubwa alilonalo ni wanafunzi,aliamua kuanzisha gazeti lilokuwa linajulikana kama “The Student” na akawa analigawa bure kwa wanafunzi ili awezae kutengeneza umaarufu kabla hajapata wadhamini wa kuweka matangazo.Ili kufanya hivyo ilimlazimu kugawa jarida hilo kopi 50,000 bure kwa kuanzia.Hata hivyo baadaye lilipokuwa maarufu aliweza kuvutia baadhi ya makampuni madogomadogo ambayo ilimsaidia kupanua zaidi biashara yake.

Baada ya kuwa amekusanya kiasi fulanicha pesa,aliamua kufungua “Record Label”yake na akapata kachumba kadogo ka kuanzia biashara hapo.Unajua nini kilikuja kumtoa?

Baada ya kuanza kurekodi alikuja mwanamuziki mmoja ambaye alikuwa hajulikani kabisa aliyekuwa anaitwa Mike Oldfield aliennd akurekodi hapo wimbo wake wa “Tubular Bells”-Cha ajabu ni kuwa wimbo huo uligeuka maarufu sana na alifanikiwa kuuza takribani kopi milioini 5 na kila msanii akatamani kurekodi katika studio hiyo,na hapo ndio ulikuwa mwanzo wa mafanikio yake.Hapa namzungumzia bilionea nambari moja wa nchini nuingereza,Richard Branson amabye kwa sasa anamiliki zaidi ya makampuni 40 yakiwemo ya ndege,makapuni ya simu,train n.k

 

Maisha ya Branson yanafanana sana na maishaya watu wengi ambao wamefikia mafanikio ya kiwango cha juu katika maisha yao.Kuna mambo ya msingi matatu ambayo ni lazima uyazingatie na kuyaishi kama kweli unataka kufanikiwa kwa haraka kwa kile ambacho unakifanya.

Kwanza ni kuhakikisha kuwa haukubali jambo moja usiloliweza likufanye uamini kuwa huwezi kila kitu.Ingawa Branson kwa takwimu za darasani alikuwa anaonekana hawezi chochote,cha kushangaza ni kuwa amekuwa na mafanikio makubwa sana katika biashara anazozifanya.Kila mtu kuna eneo fulani la maisha yetu ntunaweza kuonekana kuwa hatuwezi,ila hilo lisikufanye kuamini kuwa hakuna kitu kingine ambacho uanweza kufanya.

Kuna watu wameshidnwa kuendelea mbele katika maisha yao kwa sababu huko nyuma kuna kitu walishidnwa katika maisha yao.Kuna wengine walifeli darasani,kuna wengine walifukuzwa kazi,kuna wengine mahusiano yao yalivunjiika,kuna wengine walifeli katika biashara wanazofanya-Na kwa sababu ya kuflei katika jambo moja walijikuta hawajiamini tena na wameshidnwa kusogea hatua moja mbele kabisa.Amua kuwa kama Branson,ingawa alionekana hawezi kitu kwa wakati huo ila aliamua kuiamini  ndoto yake na leo maisha yake yamebadilika kabisa.

Pili ni kuhakikisha kuwa unaanza na kile ulichonacho na unaanza pale ulipo.Kama Branson angeamua kujionea huruma na kuona kuwa hana kitu,pengine hadi leo angekuwa ni mtu wa kawaida sana.Lakini jambno moja ambalo Branson alilolijua ni kuwa huwezi kupata kitu ambacho hauna hadi pale utakapotumia kile ambacho unacho.

Kama wewe ni mtu ambaye unasema hauanzi kwa sababu hauna kitu,ujue uko mbali na mafanikio.Watu ambao wanafanikiwa ni wale ambao kila wakati wanajaribu kutumia kitu walichonacho bila kujali ni kidogo kiasi gani.Hebu fikiria,mtu anakosa ofisi hadi anaamua kwenda kuomba atumie eneo la kanisa ili kuanza kufanya biashara?Hii ni kuonyesha kuwa hakuwa tayari kuona kitu chochote kinamzuia kufikia malengo aliyokluwa nayo.

Hiki ndicho kitu uantakiwa kukifanya kwa mwaka huu;usikubali hata siku moja kuishi bila kufanya kile amabcho umeamua kukiishi katika maisha yako.Kwa namna yoyote ile unayoweza basi hakikisha unafanya kitu kuhusiana na ndoto uliyonayo katika maisha yako.Hebu leo jiulize,kuna kitu chochote ambacho unafanya kuelekea katika ndoto yako kubwa ama wewe ni mmoja wa wale ambao wanasubiri wawe na vingi?

Jambo la tatu ni ufahamu ambao uantakiwa siku zote ujengeke ndani yako ya kuwa;kuna siku utapata upenyo usio wa kawaida kama utakuwa king’anga’nizi na mtu asiyekata tamaa.Kwneye mafanikio kuna kitu kinaitwa “Pressing the Right Button”-Hii inamaanisha kufanya kitu ambacho ghafla kitabadilisha maisha yako.Jambo la kujua ni kuwa kitu hiki hakiwezi kukufuata bali utakutana nacho uanpokuwa bize kufanya kile unachokiamini.

Kwa Branson “Right Button” ulikuwa ni wimbo  wa Tubbular Bells,kwako inaweza kuwa ni kukutana na mtu atakayekupa mtaji uliokuwa unautafuta,ama kuunganishw ana fursa kubwa sana itakayobadilisha maisha yako n.k

Huwezi kutimiza ndoot yako bila kuiishi ndoto yako.Unatakiwa kila siku uwe unachukua hatua kuelekea mbele ili ukaribie kukutana na “Right Button” yako.Kwa sababu haujui utakutana nayo lini,wapi na kupitia kwa nani-Hii ni sabbau tosha ya kukufanya wewe uishi maisha ya kufanya kwa ubor akila kitu ambacho unakifanya katika maisha yako.Hivyo basi kila fursa uanyoipata katika maisha yako kuanzia leo ifanye kwa ufanisi na ubor akwani ndani yake,imebeba fursa kubwa zaidi kuliko uanvyoweza kuona kwa sasa.

Ili kujifunza zaidi nakushauri uagize kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO kinachochambua mbinu 60 ambazo watu maarufu huwa wanazitumia ili kufanikisha malengo yao(0655720197).

Unaweza pia kumshirikisha mtu ujumbe huu ama kushare kwenye account zako za social media kwa kubonyeza kitufe hapo chini.

See You At The Top

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website