Navigate / search

Hakuna Mafanikio Hadi Upate Majibu Ya Maswali Haya Mawili

images

Kuna maswali mawili muhimu sana katika maisha ambayo lazima kila mtu awe na majibu nayo,ukikosa majibu yake ni kizuizi tosha katika kuelekekea mafanikio yako.Maswali haya mawili yamekuwa ndio mwongozo kwa kila aliyefanikiwa maishani katika kila kile anachofanya.Baadhi ya watu hawayajui kabisa lakini baadhi huyajua ila hawako tayari kutumia muda wao kuyafanyia kazi katika kuyatafutia majibu yake.

1)Swali la Kwanza ni:nilizaliwa kwa KUSUDI gani

Kusudi la kitu ndio sababu iliyofanya kitu hiko kiundwe kwa namna kilivyoundwa.Ukiangalia muundo wa kijiko ulivyo unakuelekeza namna ya kutumia na ukitaka kukitumia kama kisu hautafanikiwa kabisa.Ukimwangalia ndege alivyoumbwa amepewa umbo na uwezo wa kuruka angani na ukijaribu kumuweka baharini mbwembe zote zitaisha na atakufa mara moja.
Kila mtu ameumbwa kwa kusudi maalumu la kuja kufanya hapa duniani na amepewa uwezo wa kipekee ndani yake ili kulitimiza kusudi hilo kwa mafanikio.

Ukijaribu kufanya jambo nje ya kusudi uliloletwa kulifanya duniani utafeli kila wakati.Ni kama ukijaribu kumshindanisha tai kuogelea pamoja na samaki papa,pamoja na sifa na uwezo wote alio nao tai maishani mwake atafeli kila wakati.

Tatizo sio kwamba hana uwezo ila ni kwa sababu umemshindanisha katika eneo ambalo hajazaliwa kwa kusudi hilo na hivyo hana uwezo na umbo la kumfanya awe mshindi wa kuogelea.

Watu wengi wamefeli maishani si kwa sababu hawana uwezo wa kuwafanya wafanikiwe bali ni kwa sababu wako sehemu ambazo sio kusudi la kuumbwa kwao.Ukimchukua golikipa ukamweka kuwa beki wa timu yenu,iusishangae kila wakati mkapigwa penalti kwenye lango lenu kwani badala ya kutumia miguu,utashangaa atakavyojisahau na kutumia mikono kuzuia mpira.
Leo,tumia muda kujiuliza,Je nimeumbwa kwa kusudi gani?Ninachofanya kinaendana na kusudi langu?

2)Swali la Pili:nakwenda wapi?

Kila mtu anaamka asubuhi na anaelekea kazini,shuleni,kwenye biashara n.k.Ingawa kila mtu anaonekana yuko bize lakini si kila mtu anajua anaelekea wapi katika maisha yake.Kuna watu wengi baada ya umri kwenda sana ndipo huja kugundua kuwa walipoteza muda wao kwa mambo ambayo hayakuwapeleka walikokuwa wanataka.Je,Unachofanya leo kinachangia kukupa mwelekeo wa unakokwenda?

Swali ni kuwa,jeUmeshawahi kufikiri kupitia unachofanya leo kesho utafika wapi?Kama haujui unakokwenda kila mahali ulipo patakuwa sahihi.Kama unaona unachofanya leo hakitakupeleka kule unakotaka kwenda ,tafuta namna ya kubadilisha.Hakuna maana yoyote ya kuishi maisha usiyoyapenda kisha kuja baadae uzeeni kugundua umepoteza muda wako.

Usihangaike kuwa bize tu,unaamka unaenda ofisini,biasharani,shuleni,Kisha unarudi nyumbani-Je unajua unakokwenda?baada ya Miaka 10 au 20 unataka uwe umefika wapi?

Leo,unapoianza siku yako anza kutafuta majibu ya Maswali haya,kwani Hakuna mafanikio bila kujua kusudi la maisha yako na kule unakokwenda.

Endelea Kutembelea ukurasa wangu wa facebook ili Kujifunza Zaidi.

Ndoto Yako Inawezekana,

See You At The Top.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website