Navigate / search

Faida 4 Utakazopata Ukianza Kufanya Kitu Sahihi Maishani

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuishi ukifanya kitu ulichoumbiwa kukifanya na kuishi huku unafanya kitu ambacho sicho kilichomfanya Mungu akuumbe.Kila aliyefanikiwa  katika maisha yake kufika mbali sana na kufanya mambo makubwa,ni lazima aliamua kuishi kwa kufanya kitu ambacho amejengewa uwezo wa kipekee kukifanya kuloinganisha na watu wengine ambao wanafanya kitu kama hichohicho.

Watu wengin sana ukianza kuwaambia habari ya kuishi katika kusudi lao,huwa hawaoni kama ni jambo la muhimu sana katika maisha yao na wengi huwa wanapuuzia.Leo ningependa tuangalie kwa undani faida kubwa nne ambazo utazipata mara tu utakapoanza kuishi katika kusudi lililokufanya ujue duniani:

Faida ya kwanza ambayo utaipata ni kuridhika kwa dhati kutokea ndani ya moyo wako(satisfaction).Siku zote kumbuka hakuna kitu ambacho klitakupa furaha ya kweli na ridhiko la kweli la ndani yako kama kuishi ukifanya kitu ambacho hasa moyo wako ndio unakufurahia.Watu wengi sana wamezungumza walipofikian katika kilele cha maisha yao kuwa,hapo zamani walifikiri kuwa umaarufu ama pesa zingewapa furaha ya kweli lakini walikuja kugundua kuwa,havikuweza kuwapa furaha waliyokuwa wanaitafuta.Unachotakiwa kukumbuka siku zote ni kuwa,unapoanza kufanya kitu unachokipenda mwanzoni inaweza kuwa ni ngumu lakini baadaye utaishi maisha yako yote ukiwa na furaha.Watu ambao leo wanakwepa kuishi katika kitu ambacho waliumbiwa kukifanya huwa wanaishia kujutia maisha yao yote,usiwe mmoja wao.

Faida ya pili ni kuwa na nguvu endelevu katika kufanya kile ambacho umeumbiwa.Siku zote kumbuka kuwa utakapoanza kufanya jambo fulani utakutana na vikwazo vingi sana huko njiani na usipokuwa makini utakata tama.Kitu pekee ambacho huwafanya watu wasikate tamaa katika kufanya kile ambacho wanaendelea kukifanya ni ile hali ya kuwa na uhakika kuwa wanachofanya ni kitu sahihi kabisa kuhusiana na maisha yao.Kama wewe hauna uhakika na kile ambacho unakifanya,siku zote utakuwa mtu wa kukata tama mapema kila wakati ambako utakutana na changamoto fulani.Unapoanza kuishi katika kitu ulichoumbiwa basi utajikuta unapata nguvu za ziada kukabiliana na changamoto unazokutana nazo.

Faida ya tatu ni kuwa inakusaidia kujua namna ya kuweka vipaumbele katika matumizi ya rasilimali ulizonazo.Hii inakusaidia kujua namna ya kutumia muda wako,namna ya kutumia pesa zako n.k Mara unapojua mahali uanpotakiwa kuwepo na kufanya kitu ambacho umeumbwa kukifanya,utajikuta kila wakati unakuwa mtu ambaye uko makini kwenye matumizi ya muda na pesa zako-Utajitahidi utumie muda wako katika mambo ambayo yanakujenga na kukupeleka kule ambako unataka kwenda.Utatumia pesa zako kufanya mambo ambayo yatakuongezea thamani ya kile ambacho unataka kukifanya.Kama haujui au hauna uhakika na kitu ambacho umeamua kukiishi katika maisha yako basi utakuwa unajikuta unatumia muda wako katika mambo ambayo hayana mchango kabisa wa kesho yako.Vipaumbele katika maisha ni matokeo ya kujua hasa eneo ambalo umeumbwa kuliishi.

Faida ya nne ni kujua kwa hakika watu wa kuambatana nao.Watu ambao unatumia muda mwingi kukaa nao huwa wanajulisha kama utasogea hatua mbele zaidi ama utashindwa kuendelea mbele ama utaendelea kwa kasi ndogo.Kuna watu wengi sana wameshindwa kufikia hatima za maisha yao kwa sababu walliambatana na watu ambao hawakuwa msaada kwao,na kuna watu wengi sana ambao walifanikiwa kufika mbali kwa sababu waliambatana na watu sahihi.Uchaguzi wako wa watu wa kuambatana nao ni muhimu sana katika kujihakikishia unafika mbali.Namna bora ya kujua uambatane na nani na nani usiambatane naye ni kupitia kujua kusudi ambalo uliumbwa kulifanya na kuamua kuliishi.Kama wewe umekusudia kkuwa mfanyabiashara basi itabidi ujenge ukaribu na urafiki na wanaofanya biashara pia.

Siku zote kumbuka kuwa,kujua kusudi lako na nafasi yako katika ulimwengu huu ndio jambo la kwanza ambalo unalihitaji ili uweze kupata faida ambazo nimezisema hapo juu.Kama bado haujajua kusudi la kuzaliwa kwako,nashauri tafuta kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO na usome suran ya kwanza ama utafute CD yangu ya “HOW TO DISCOVER YOUR LIFE PURPOSE” itakusaidia sana.

See You At The Top

@JoelaNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website