Navigate / search

FAHAMU NJIA YA KUPATA FURSA YA KIPATO ZAIDI

11001795_1001050173257661_3906441546387189005_n

James Robertson(56) mkazi wa detroit Marekani amejikuta amebadilisha maisha yake ghafla baada ya kijana mmoja mwanafunzi Evan Leedy kuanzisha kampeni ya kumsaidia kupitia website aliyoianzisha kwa ajili yake ya GoFundMe.com.

James ambaye alikuwa anatembea takribani mile 21(takribani kilometa 33) ili kwenda kazini amejikuta ndani ya muda mfupi amechangiwa kiasi cha dola 351,000(Takribani 644,190,300) na watu walioguswa na juhudi yake ya miaka 15 kufanya kazi bila kulalamika.Waajiri wake wanasema

James alikuwa mwaminifu kuwahi kazini na alikuwa mfanyakazi mwenye bidii.

Hivi karibuni amekabidhiwa gari aina ya Ford Taurus ili kumsaidia kutotembea tena kwa miguu.

–Usikubali hali yoyote ile ikuzuie kufuatilia ndoto zako,unatakiwa uvishinde vikwazo vyote maishani.

–Usiwe mtu wa kulalamika bali fanya kazi yako ya sasa kwa uaminifu wa hali ya juu na bidii,ipo siku utatoka hapo ulipo.

–Msaada unakuja kwa wale tu wenye juhudi katika kidogo walichonacho.

-Ukidharau ulichonacho itakuwa ngumu kupata usichonacho.

-Ukitumia ulichonacho unafungua fursa kupata kile unachokihitaji.

USIDHARAU KAZI ULIYONAYO,

USIDHARAU ELIMU ULIYONAYO,

USIDHARAU MTAJI ULIONAO,

FANYA BIDII PALE ULIPO,ILI UFIKE KULE UTAKAKO.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website